Rose Muhando: Nafikiria kurudi kwenye Uislamu

Rose Muhando: Nafikiria kurudi kwenye Uislamu

NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.

“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.

Chanzo: GPL

Porojo @ work
 
Alivyokua anakata viuno vyake bora arudi huko nao akawakatikie mauno yake

Tena huko kwao anakotaka arudi dhabi hukemewa mwezi mmoja tu.....huku kila siku anakemewa ndiyo maana ameshindwa
 
pole zake, imani ni mahusiono ya mtu binafsi na Mungu, asidhani hao watu ndio watakuwa kisingizio cha yeye kutokuokoka.
Kama ametapeli pesa arudishe tu hakuna masihara kwenye pesa za watu hata uwe mtumishi wa Mungu...
na pia ajue makwazo hayana budi kuja
 
Kama ni kweli basi mi naona ni bora aanzishe dini yake yenye Mungu anayekubali matapeli maana hata dini ya kiislam haikubaliani na utapeli.Hata wapagani wenye mioyo safi hawakubaliani na utapeli.
 
Arudi kwenye dini ya kweli na haki!
dini inayomtambua mungu mmoja tu,
Mungu asiyekuwa na mshirika hata,
muhammad ni mjumbe wake,
Mungu asiyezaliwa wala kuumbwa,munguasiyezaa,

Mungu ambae anasamehe,ukitubu kwa dhati
 
Hivi ile mimba yake ilikuwaje? Yaani huwa anahama imani kwa kuangalia watu wanamfanyia nini sio kumtafuta mungu, huwezi kufanikiwa kwa kusubolo huruma ya mwanadamu

Mkuu kusubolo ndio nn?
 
Arudi kwenye dini ya kweli na haki!
dini inayomtambua mungu mmoja tu,
Mungu asiyekuwa na mshirika hata,
muhammad ni mjumbe wake,
Mungu asiyezaliwa wala kuumbwa,munguasiyezaa,

Mungu ambae anasamehe,ukitubu kwa dhati

Hata akirudi hatawafaa kitu maana yeye anaangalia maslahi tu.
 
Huy u Rozi alipofikia akipewa Bomu akajilipue hashindwi. Serikali imuangalie kwa ukaribu.
 
Inamaana alivyohama aliambiwa kuwa atapendwa na watu wote au? Yesu peke yake ndio anaempenda hao wengine watafataa na pia huwez kuchukiwa na dunia asikilize nyimbo zake Mara ya pili ujumbe aliokuwa anautoa kwa watu na yeye aufuate
 
ameichumaa,alikua kibiarshara zaidi,aondoke akanengue kwenye madanguro,aibu tu madhabahuni safari njema
 
ameichumaa,alikua kibiarshara zaidi,aondoke akanengue kwenye madanguro,aibu tu madhabahuni safari njema

Aibu ya kwenye madhabahu ni kunengua tu ila kufungisha ndoa za jinsia moja ni busara sio? Kama leo anatangaza kuondoka ndo unasema aibu, kipindi yupo ulikuwa unashangilia! Dumb nut!
 
hatapata show tena toka kwa wakristo,akapige kaswida
 
NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.

“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.

Chanzo: GPL

Nakupa hela Unasema bahati mbaya umeshindwa kufika?maniner zake
 
Back
Top Bottom