Mkuu nadhani haujafuatilia sakata zima namna lilivyokwenda.
Embu angalia hiyo video ya sakata kisha sikiliza video ya Ummi, mganga mkuu pamoja na mwanamke fulani mweny cheo hapo hosipitalini.
Ukishawasikiliza wote hao ndiyo utagundua stori na namna ya kubalansi maelezo ya pande zote.
Mimi nimeona kama mchezo mchafu huo uliandaliwa na mtu wa maabara kwa nia ovu.
Sitetei uozo wao isipokuwa yule boss wao wa kike aliyelitolea ufafanuzi sakata hilo, kasema expiry yake ipo ndani ya muda wa kutumika mpaka mwezi April na ni kawaida ya dawa zote kutotupwa siku hiyo hiyo ya expire iliyoandikwa kwenye kifungashio, huwa kuna muda wa mbele kitaalamu wanaoujua wafamasia.
Na kwamba walikubaliana kuendelea kutumia ili isije ikafika tarehe ya mwisho kabisa waka destroy.
Kwa hiyo huyo mfamasia anaufahamu muongozo huo, sasa kwanini aende kuvimba dirishani akizikataa dawa hizo kwa staff mdogo kabisa asiye na mamlaka yoyote?
Halafu tusi la nyo nyo nyo ni la kiuhawara zaidi, watani au ni kwa watu wanaodharauliana sana na kutafutiana kuharibiana.
Mwisho wa sakata hili waweza kuwa ni wa aibu kwa Lab tech aliyerusha.