Kama Kiingereza changu hakinipi kiwi ya macho; nikisoma katikati ya mstari naelewa hivi:
1. Rostam anatuhumiwa na This Day kuwa alihusika kwa kuwa alikuwa ndani ya kamati ya watu 22 ya kampeni ya uchaguzi ya mwaka 2005.
2. Yeye anasema hakuwa mweka hazina wa CCm mwaka 2005, bali marehemu mama Mbatia.
3. no 3 hapo juu halina ugomvi kwasababu nafasi anayosemwa nayo sio ya uweka hazina bali ya kwenye kamati ya kampeni ua uchaguzi.
4. kumuingiza marehemu kwenye hili ni kutaka kuizika hoja dhidi yake.
5. This Day sio wajinga; naamini wanajua wanachoandika, na naamini Rostam kwa kujibu alivyojibu kajiingiza mtegoni.
6. Jibu la Rostam linarudisha mjadala wa kifo cha huyo mama. pengine ilishanukia kuwa iko sooo, kama wanavyosema This Day kuwa wengi wa watuhumiwa wanasingizia kampeni; kama ndivyo, marehemu peke yake ndiye alijua ukweli kama zilitumika kwenye kampeni au la; au kama ziliingia kwenye account ya CCM au la; ndio maana kifo chake ni ahueni kwa wengi. Si ajabu baada ya kifo chake kuna mafaili hayapo ofisini kwake.
7. Guys, lets read between the lines and digest the information. Iko habari nzito hapa