Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts


Kama alikuwa hawajui Richmond, basi anawajua Dowans! maana kama wewe ni Mkandarasi na hawa jamaa wanakujwa kusema tunatafuta mkandarasi, yeye Rostam si aliona kuwa kuna pesa za kujiengenezea kwa kuwasilisha maombi kwenye tenda?

Je hakukutana na Wakuu wa Dowans kuwashawishi kuwa Kampuni yake ya Caspian ina uwezo wa kufanya kazi za kikandarasi ambazo Dowans walikuwa wanahitaji mkandarasi mahiri?

Je kuna mtu yeyote anayejua hawa Dowans ni kina nani? sijasoma Ripoti ya Mwakyembe na nakumbuka vizuri Sitta aliwaambia wasichunguze chochote kuhusu Dowans.

Swali ni who are these Dowans folks? Ikiwa hata google haina information hata moja zaidi ya magazeti ya Tanzania na Jambo Forum kama reference points, then Rostam has an obligation to tell Taifa who are these cats!
 

NAONA KAMANDA UMEAMUA KUTUNGA SWALI NA KUJIBU MWENYEWE, KAMA UMESOMA VITABU VYOTE VYA MWAKIEMBE NA HITIMISHO LA MWAKIEMBE HAKUNA SEHEMU ANASEMA ANAMUHUSISHA ROSTAM AZIZ NA HASARA HIYO KWAHIYO USIPELEKE HOJA SEHEMU AMBAYO HAIPO.

PILI KAMA MSOMAJI ALIYOYAJIBU YAKO WAZI HAKUNA HOJA AMBAYO HAJAJIBU KIFASAHA ISISPOKUA YALE AMBAYO AMESEMA ATAJIBU BUNGENI,PIA NIMEPITIA HOJA ZA WENGI KTK HUU MJADALA NIMEJIFUNZA WENGI WALIOCHANGIA HATA ES ANATUMIA HISIA KAMA WALIVO WAANDISHI WETU WA KITANZANIA WAPO WANAO AMINI KUA RICHMOND ILILIPWA PESA NA SEREKALI HATA MWAKIEMBE KASEMA HIVO BUT HAKUNA EVIDENCE KUA WALILIPWA NA KISHERIA RICHMOND IS NOT DOWANS MWAKIEMBE KTK RIPOTI YAKE ANAONYESHA MARA RICHMOND IMELIPWA MARA DOWANS HAELEWEKI.

WANA JF NIMESOMA RIPOTI YA MWAKIEMBE FROM PG ONE MPAKA PAGE 137 MPAKA LEO KUNA MAPUNGUFU MENGI SANA NA TATIZO NI KUA ALIFANYA UCHUNGUZI AKIWA TAYARI NA JIBU AMESHINDWA KUJUA MKATABA ULIANDALIWA NA TANESCO,WIZARA YA MADINI,OFISI YA MWANASHERIA MKUU etc,

NIKIRUDI KTK MADA ROSTAM HAJAJIBU YALE ANAYOTAKIWA KUJIBU BUNGENI NA RIPOTI HAIONYESHESHI WAPI AMEHUSIKA KTK HASARA HII.
 

Siyo wewe pekee yako uliyesoma ripoti, maana mimi hadi vielelezo na hansard!
Rostam Aziz ametajwa na si mwingine bali na mshikaji wake Salva Rweyemamu. (una bahati sina kitabu chenyewe hapa cha hansard nikupe mpaka ukurasa). Salva amesema yeye alikuwa hawajui akina Gire bali alitambulishwa na Rostam. Yaani Rostam alimpigia Salva kwamba aongee na akina Gire. Salva alikuwa anaongea nao kuhusiana na PR company yake na Richmond walikuwa wanahitaji 'positive PR' na walimwomba Rostam awasaidie na aliwaelekeza kwa Salva. Sasa haya yalisemwa na Salva mbele ya kamati chini ya kiapo. Je Salva aliidanganya kamati chini ya kiapo? Rostam hakwenda alipoitwa leo anajitetea kwenye vyombo vya habari.
Sasa ukitaka kujua kwamba siku zake zimekaribia hebu anagalia Spika 6 alivyoamua kutumia kamati ya maadili ili wabunge hao (EL, RA, Karamagi) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwani wameenda kupayukia nje ya bunge wakati walikuwa na uwezo wa kujitetea bungeni!
Narudia tena, kama wanajiamini hivyo waende bungeni kuongea utumbo wao!
 
Chuki za kibanfsi hizo na ndio zinawafanya msiwe na maendeleo. Kajibu hoja zote kiufasaha kabisa sasa tungoje tume na tungoje bungeni atsema nini, wewe unalalama tu.

Hivi maendeleo unayapimaje? inaonekana definition ya maendeleo huijui.
 
Eti Dowans wanamiliki mgahawa uk ujulikanao kama "The Dowans Hotel ulioko Aberlour, Banffshire, Scotland AB38 9LS" hizi habari nizakweli?
 


Mkuu Susuviri,

Ubarikiwe sana mkuu!
 
Kwani SK inangoja nini kuwashtaki waliohusika na kashfa ya EPA, mikataba ya madini, Richmonduli, ununuzi wa rada, magari na helikopta za jeshi, waliojipatia KCM katika mazingira ya kutatanisha? Hebu twambie wanangoja lipi kuwashtaki hawa?

Unashitaki unapokuwa na ushahidi wa kutosha tu, ukishitaki kipuuzi ndio unajikuta unashindwa kesi na unalipa madeni kama ilivyokuwa kwa IPTL au hujui kuwa serikali ilishindwa kesi? kwa kukurupuka tu.

Ndio maana unaona tume zinaundwa.
 

Ndio mbishi sana tena, hujajibu maswali, jibu maswali wacha kupayuka bila mpango.
 
Kama Mwana Wa Mungu Nabii Issa Alikanwa Na Petro How Easy Cant It Be For Caspian Inc Kuikana Richmound Inc

Na ndio huyo huyo Nabii issa atakuja kuwapinga wanaomwita Mungu.
 
Unashitaki unapokuwa na ushahidi wa kutosha tu, ukishitaki kipuuzi ndio unajikuta unashindwa kesi na unalipa madeni kama ilivyokuwa kwa IPTL au hujui kuwa serikali ilishindwa kesi? kwa kukurupuka tu.


Mkuu Dar-Es-Saalam,

Heshima mbele, kwenye nchi ya kusadikika hakuna kukurupuka maana mafisadi are very good at making things like IPTL looks like serikali ilikurupuka, no way kila ishus inapangwa kwa mkao wa kula, off course somebody knew kuwa watashindwa kesi, hivyo kufainiwa na kwenye kulipa hiyo fine mlo utaendelea, maana kama fine ni millioni 2, basi ujue zinalipwa tano, maana kama ushaidi ni mali hapa kusadikika basi Ditopile asingekuwa anaendelea na biashara ya asali Tabora.

Ahsante Kaka.
 
Na bado hajasema vizuri...lets wait for aprils bunge na yeye asulubiwe kama EL!!!
Naona analeta masihara huyu jamaa...

hapo umenena tungoje bunge april na tusishabikie kwa ushabiki tu.
 
http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=84561#post84561

Hiyo ilikuwa moja ya post zangu za mwezi wa nane mwaka jana wakati scandal hii ilipofumuka.
Go back to the point, Huyo manager wa Dowans ni huyo mshikaji nilimuelezea hapo juu kabla report ya Mwakyembe haijatoka. Sasa huyu Mr Saleh alikuwa member wa board ya madairector ya TANESCO na yeye alikuwa mshikaji kabisa na Gire, wanajuana for years.

Huyu mzee Mwanae kaolewa na body wa Jakaya kabisa, mshikaji wake tangu mambo ya nje. Sasa ukiniambia Jakaya alikuwa hajui kama hii ni scum nashindwa kuelewa. Tangu mwanzo nilisema sina uhakika Lowassa kahusika vipi, sema Jakaya nina 100% anajua hili deal zima.

Insider wangu tulifahamu hii deal kabla haijafunikwa, na ndio kisa cha Endrew Daraja kuhamishwa ubalozini hapa US na mheshimiwa. Kusema kweli hii nightmare JK anaifahamu lakini analeta kiburi. I wish wamkamate huyu mkurugenzi wa DOWAS ajibu mashitaka ya kununua nyumba US, where did he got the $$$
 

Kutokana na ile post ya leo asubuhi iliyofutwa haraka haraka naogopa hata kukujibu Mkuu.
 
Mahangaiko ya nini? kadiri wanavyobwabwaja ndivyo wanavyoendelea kujianika. Sasa Yonah kasema anawajua Richmond (rejea mahojiano yake na TVT)huyu anahitaji kubanwa atueleze Richmond ni nani.
 

Kusadikika
 
Anyoyaeleza mh.Rostam Aziz(mb) yana ukweli kinadharia lakini sio katika uhalisia ambao unadhihirika kwa hiyo kama mtu mwenye akili timamu anaweza kujua maana.Richmond ni moja ya sehemu ya ufisadi ndani ya nji hii katika kipindi cha miaka 46 ya uhuru wake.
Nakumbuka hata Petro aliwahi kumkana Yesu lakini matendo yalidhihirisha kuwa yeye ni mfuasi wake sitaki kumkashifu mheshimiwa lakini pia vigezo alivyotupa havitoshi kwa mamilioni ya watanzania pamoja na anaowawakilisha katika jimbo lake la Igunga. Anatakiwa aende zaidi ya hapo na huo utajiri ameupata wapi kama sio migongoni mwetu kwa kutumia rasilimali zetu.
 

Unaushahidi uweke wazi, kwani hata nawe ukiongea bila ushahidi inakuwa ni nadharia tu.
 
Unaushahidi uweke wazi, kwani hata nawe ukiongea bila ushahidi inakuwa ni nadharia tu.

Ushahidi namba moja ni kwamba Rostam anafanya nao biashara.Je unaweza kufanya biashara na watu usio wajua ? Salva alisema mengi na kuthibitisha hili kwamba RDC wana connection nzito na RA
 
Ushahidi namba moja ni kwamba Rostam anafanya nao biashara.Je unaweza kufanya biashara na watu usio wajua ? Salva alisema mengi na kuthibitisha hili kwamba RDC wana connection nzito na RA

Wewe unasema hayo, aliyeanzisha hii thread hapo mwanzo anam-qoute Rostam akisema hivi:

“Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho,” alisema Rostam."

Upo hapo ulipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…