Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam: Siwajui Richmond

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MFANYABIASHARA na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), amesema hana uhusiano wowote, na wala haijui Kampuni ya Richmond Development Company LLC ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura baada ya kuingia mkataba wenye utata na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

“Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho,” alisema Rostam.

Wakati akikana kuifahamu Richmond na wamiliki wake, Rostam, alikiri kuwahi kutaka kufanya kazi na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ambako Kampuni ya Richmond ililazimika kuhamishia mkataba wake huko, baada ya kushindwa kuutekeleza kwa muda uliowekwa.

“Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi,” alisema Rostam.

Matamshi haya ya Rostam yanatokana na shaka iliyojitokeza baada ya Kamati Teule ya Bunge kueleza katika ripoti yake kwamba, iligundua kuwa Dowans iliwahi kutumia anwani ya barua pepe ya Kampuni ya Caspian Construction Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa huyo.

Akifafanua kuhusu hilo, Rostam alisema alilazimika kuacha anuani yake kwa Dowans baada ya kuomba kazi kwa kampuni hiyo.

“Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani,” alisema kwa ufupi.

Kama alikuwa hawajui Richmond, basi anawajua Dowans! maana kama wewe ni Mkandarasi na hawa jamaa wanakujwa kusema tunatafuta mkandarasi, yeye Rostam si aliona kuwa kuna pesa za kujiengenezea kwa kuwasilisha maombi kwenye tenda?

Je hakukutana na Wakuu wa Dowans kuwashawishi kuwa Kampuni yake ya Caspian ina uwezo wa kufanya kazi za kikandarasi ambazo Dowans walikuwa wanahitaji mkandarasi mahiri?

Je kuna mtu yeyote anayejua hawa Dowans ni kina nani? sijasoma Ripoti ya Mwakyembe na nakumbuka vizuri Sitta aliwaambia wasichunguze chochote kuhusu Dowans.

Swali ni who are these Dowans folks? Ikiwa hata google haina information hata moja zaidi ya magazeti ya Tanzania na Jambo Forum kama reference points, then Rostam has an obligation to tell Taifa who are these cats!
 
Nakuhurumia Dar-es-salaam,yaani hadi sasa hujaelewa watu wanamlalamikia Rostam kwa lipi?Rostam kama kiongozi wa umma anahusishwa na kuliingizia taifa hasara na ufisadi hizo ndizo tuhuma zake kwenye richmond na mambo mengine.Hayo mambo yote ni ya kijinai,mwananchi wa kawaida hawezi kushtaki sijui nikuwekee hapa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ndio uelewe,au tu nikupe link kwa faida yako tembelea www.parliament.go.tz sehemu ya documents,click acts,halafu tafuta hiyo sheria,ndiyo inayoongoza mashtaka nchini.Usibwabwaje kama hauna research.DPP ndiye mkuu wa mashtaka hata ukianzisha private prosecution bado yeye ana uwezo wa ku-continue au kudiscontinue proceedings.Pia kasome katiba ya Tanzania mabadiliko ya kumi na nne halafu ndio uje hapa.Kutokana na legal technicality ya kifungu cha 190 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,mwananchi wa kawaida hawezi practically kufungua hayo mashtaka ya jinai na ndio maana wewe ukienda kushtaki polisi,mahakamani unageuka kuwa shahidi(PW1) na jamhuri ndio inatakeover kila kitu. Kama kuna mtu anakushauri basi anakushauri vibaya,usiiingilie professional.Tulia tukueleze wenye field.
Kama Rostam angekuwa amemdhulumu mwananchi yeyote mbuzi shamba au jogoo ungeshaona kesi pale kisutu,lakini kwa kuwa suala ni wizi na udanganyifu kwenye mali ya umma,linarudi palepale kwenye penal code cap.16 chini ya DPP.Mi nakupa shule ya bure tu hulipii wala nini hivyo usikonde leta maswali yako tu,umekutana na reseacher.Wote tunangoja sheria zifuate mkondo wake lakini kwakuwa zimekuwa hazifuati huo mkondo na ndio maana tunatumia uhuru na haki yetu inayolindwa na ibara ya 18 ya katiba,ibara ya 8 ya katiba na ibara ya 27 ya katiba na kukusaidia tu nitakunukulia hapa ibara ya 8 na ya 27 manaake najua ibara ya 18 unaijua.
8.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.

mwenzetu ibara ya 8(b) unaielewaje? au ustawi unaozungumziwa hapo ni ustawi wa ninyi mafisadi wachache? basi wafute hapo waseme mafisadi.na wanaposema serikali itawajibika kwa wananchi wana maana gani?hujui nyamaza
27.-(1) Kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri
ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote
inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na pia kuiheshimu mali
ya mtu mwingine.
(2) Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya
mamlaka ya nchi
na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu
na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama
watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao
.
Ibara ya 27(1) unaielewa? kama ndiyo wajibu wako wewe ni nini chini ya ibara hiyo?hebu nenda mbele zaidi angalia ibara ya 27(2)
katiba inaposema wananchi ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao ina maana gani?

Kwa hakika wewe unasema unampenda jk kwa kweli humpendi kabisa kwani anayempenda jk atamwambia ukweli.He need to be told the truth,hata kama unamuuna.Yupo jaji mmoja kule Uganda anaitwa kanyeihamba ni jaji pekee anayeweza kumface m-7 na kumwambia unayofanya sio,m-7 alimchukia sana lakini,siku moja alipomwita ili amponde mbele ya waandishi wa habari kutokana na hukumu yake aliyoitoa dhi ya besigye Kanyeihamba alikuwa wa kwanza kuchangia mada ya Rais na kumwambia, "Mhe.umeongea vizuri sana na wasikilizaji wako kukupigia makofi,lakini hawahawa waliokupigia makofi leo,ndio hao hao walinipigia makofi mimi hadi ukaniteua kuwa jaji,lakini leo wanakupigia makofi wewe kwa kuiponda hukumu yangu kwakuwa ilikuwa dhidi yako,Mhe.Rais kati ya mimi na hawa nani anakupenda zaidi? mimi nayekwambia ukweli au hawa wanafiki?
M-7 alikosa cha kuongea,matokeo yake,M-7 anamheshimu sana kanyeihamba.
Hivyo hata kikwete yapo mambo mengi sana ya kumjadili yeye kama yeye,yapo tunayompongeza,yapo tunayomponda na yapo ambayo tunamwonesha njia.Kiongozi mzuri ni yule anayekubali kukosolewa sio wewe Dar-es-salaam.

NAONA KAMANDA UMEAMUA KUTUNGA SWALI NA KUJIBU MWENYEWE, KAMA UMESOMA VITABU VYOTE VYA MWAKIEMBE NA HITIMISHO LA MWAKIEMBE HAKUNA SEHEMU ANASEMA ANAMUHUSISHA ROSTAM AZIZ NA HASARA HIYO KWAHIYO USIPELEKE HOJA SEHEMU AMBAYO HAIPO.

PILI KAMA MSOMAJI ALIYOYAJIBU YAKO WAZI HAKUNA HOJA AMBAYO HAJAJIBU KIFASAHA ISISPOKUA YALE AMBAYO AMESEMA ATAJIBU BUNGENI,PIA NIMEPITIA HOJA ZA WENGI KTK HUU MJADALA NIMEJIFUNZA WENGI WALIOCHANGIA HATA ES ANATUMIA HISIA KAMA WALIVO WAANDISHI WETU WA KITANZANIA WAPO WANAO AMINI KUA RICHMOND ILILIPWA PESA NA SEREKALI HATA MWAKIEMBE KASEMA HIVO BUT HAKUNA EVIDENCE KUA WALILIPWA NA KISHERIA RICHMOND IS NOT DOWANS MWAKIEMBE KTK RIPOTI YAKE ANAONYESHA MARA RICHMOND IMELIPWA MARA DOWANS HAELEWEKI.

WANA JF NIMESOMA RIPOTI YA MWAKIEMBE FROM PG ONE MPAKA PAGE 137 MPAKA LEO KUNA MAPUNGUFU MENGI SANA NA TATIZO NI KUA ALIFANYA UCHUNGUZI AKIWA TAYARI NA JIBU AMESHINDWA KUJUA MKATABA ULIANDALIWA NA TANESCO,WIZARA YA MADINI,OFISI YA MWANASHERIA MKUU etc,

NIKIRUDI KTK MADA ROSTAM HAJAJIBU YALE ANAYOTAKIWA KUJIBU BUNGENI NA RIPOTI HAIONYESHESHI WAPI AMEHUSIKA KTK HASARA HII.
 
Siyo wewe pekee yako uliyesoma ripoti, maana mimi hadi vielelezo na hansard!
Rostam Aziz ametajwa na si mwingine bali na mshikaji wake Salva Rweyemamu. (una bahati sina kitabu chenyewe hapa cha hansard nikupe mpaka ukurasa). Salva amesema yeye alikuwa hawajui akina Gire bali alitambulishwa na Rostam. Yaani Rostam alimpigia Salva kwamba aongee na akina Gire. Salva alikuwa anaongea nao kuhusiana na PR company yake na Richmond walikuwa wanahitaji 'positive PR' na walimwomba Rostam awasaidie na aliwaelekeza kwa Salva. Sasa haya yalisemwa na Salva mbele ya kamati chini ya kiapo. Je Salva aliidanganya kamati chini ya kiapo? Rostam hakwenda alipoitwa leo anajitetea kwenye vyombo vya habari.
Sasa ukitaka kujua kwamba siku zake zimekaribia hebu anagalia Spika 6 alivyoamua kutumia kamati ya maadili ili wabunge hao (EL, RA, Karamagi) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwani wameenda kupayukia nje ya bunge wakati walikuwa na uwezo wa kujitetea bungeni!
Narudia tena, kama wanajiamini hivyo waende bungeni kuongea utumbo wao!
 
Chuki za kibanfsi hizo na ndio zinawafanya msiwe na maendeleo. Kajibu hoja zote kiufasaha kabisa sasa tungoje tume na tungoje bungeni atsema nini, wewe unalalama tu.

Hivi maendeleo unayapimaje? inaonekana definition ya maendeleo huijui.
 
Eti Dowans wanamiliki mgahawa uk ujulikanao kama "The Dowans Hotel ulioko Aberlour, Banffshire, Scotland AB38 9LS" hizi habari nizakweli?
 
Sasa haya yalisemwa na Salva mbele ya kamati chini ya kiapo. Je Salva aliidanganya kamati chini ya kiapo? Rostam hakwenda alipoitwa leo anajitetea kwenye vyombo vya habari.
Sasa ukitaka kujua kwamba siku zake zimekaribia hebu anagalia Spika 6 alivyoamua kutumia kamati ya maadili ili wabunge hao (EL, RA, Karamagi) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwani wameenda kupayukia nje ya bunge wakati walikuwa na uwezo wa kujitetea bungeni!
Narudia tena, kama wanajiamini hivyo waende bungeni kuongea utumbo wao!

Mkuu Susuviri,

Ubarikiwe sana mkuu!
 
Kwani SK inangoja nini kuwashtaki waliohusika na kashfa ya EPA, mikataba ya madini, Richmonduli, ununuzi wa rada, magari na helikopta za jeshi, waliojipatia KCM katika mazingira ya kutatanisha? Hebu twambie wanangoja lipi kuwashtaki hawa?

Unashitaki unapokuwa na ushahidi wa kutosha tu, ukishitaki kipuuzi ndio unajikuta unashindwa kesi na unalipa madeni kama ilivyokuwa kwa IPTL au hujui kuwa serikali ilishindwa kesi? kwa kukurupuka tu.

Ndio maana unaona tume zinaundwa.
 
Yote uliosema lakini hujajibu hata swali langu moja? ngoja niyarudie kukupa faida? maana naona masikini umechapa sana key board yako lakini maswali yangu umeya-miss kabisa:

Kama ni hivyo basi tungoje sheria zifate mkondo, kuna tume zimeundwa, au na hizo serikali haikufuata sheria?

Halafu hili la mtu binafsi kushindwa kuishitaki serikali, naomba katazame tena sheria au waulize wataalam wakueleze, linawezekana kabisa ila lina njia zake.

Halafu ngoja nikukumbushe, hapa watu hawaongelei kuhusu serikali, wanaongelea kuhusu Rostam Aziz na vielelezo vyote wanavyo dhidi yake, wanangoja nini kumshitaki?

Upo hapo ulipo? masikini augostooons, naona haupo kabisaaa

Nilichogundua wewe ni mbishi,hutaki kuelewa kwa hiyo dawa yako ni ama kukuacha kama ulivyo au kuendelea kukupa darasa kila napopata nafasi.Manaake hata nikikuambiu mwezi huzunguka dunia utabisha du,hata kama ipo scientifically proved.Ni swali gani ambalo hujajibiwa? ukisoma maelezo yangu na reference nilizokupa utapata majibu yako yote labda uniambie wewe mvivu wa kusoma.
Labda nikwambie tu,hakuna tume iliyoundwa kuhusu mikataba ya madini,ile ni kamati tu ya Rais na wala haina nguvu ya kisheria(legal backing) kama ilivyokuwa kamati ya mwakyembe.Kisheria kila kitu kina enabling provision,ndio maana utasikia sheria shirika fulani limeundwa kwa mujibu wa sheria fulani n.k Ile ya benki kuu,ndiyo yenye mamlaka kisheria kwani inachokipengele cha kisheria.Hizo nyingine zilizoundwa hapo kabla baadhi zilikuwa na nyingine hazikuwa na mamlaka kisheria.Na kwa mantiki hiyo tume nyingi sana zimeshaundwa na kutoa ripoti nchi hii lakini matokeo yake hayafanyiwi kazi.Aidha hakukuwa na sababu ya kuunda tume ya BOT wakati Ernest and Young wameshabainisha kila kitu kwenye ripoti yao,nani suspect na nani sio suspect.Kama kulikuwa na haja ya kuwa na tume nyingine ya uchunguzi,basi balali hakutakiwa kutanguliwa uteuezi wake,ilipaswa asimamishwe awe suspended pending uchunguzi wa hiyo tume nyingine.
Na tunachotaka pale si kusikia pesa zimerudi,zilikuwa wapi na hao waliozirudisha wamefanywa nini? huo mkao wa kula.Suala la richmond limekwisha halihitaji tume tena tunataka utekelezaji na ndio mada hapa.
Swali la pili na la tatu nimeshakujibu,mvivu wa kusoma siwezi kurudia hapa.Kasome kwanza reference nilizokupa afu urudi hapa tuendeleee na kama sijakujibu jf members wengine watasema.

Ndio mbishi sana tena, hujajibu maswali, jibu maswali wacha kupayuka bila mpango.
 
Kama Mwana Wa Mungu Nabii Issa Alikanwa Na Petro How Easy Cant It Be For Caspian Inc Kuikana Richmound Inc

Na ndio huyo huyo Nabii issa atakuja kuwapinga wanaomwita Mungu.
 
Unashitaki unapokuwa na ushahidi wa kutosha tu, ukishitaki kipuuzi ndio unajikuta unashindwa kesi na unalipa madeni kama ilivyokuwa kwa IPTL au hujui kuwa serikali ilishindwa kesi? kwa kukurupuka tu.

Mkuu Dar-Es-Saalam,

Heshima mbele, kwenye nchi ya kusadikika hakuna kukurupuka maana mafisadi are very good at making things like IPTL looks like serikali ilikurupuka, no way kila ishus inapangwa kwa mkao wa kula, off course somebody knew kuwa watashindwa kesi, hivyo kufainiwa na kwenye kulipa hiyo fine mlo utaendelea, maana kama fine ni millioni 2, basi ujue zinalipwa tano, maana kama ushaidi ni mali hapa kusadikika basi Ditopile asingekuwa anaendelea na biashara ya asali Tabora.

Ahsante Kaka.
 
Na bado hajasema vizuri...lets wait for aprils bunge na yeye asulubiwe kama EL!!!
Naona analeta masihara huyu jamaa...

hapo umenena tungoje bunge april na tusishabikie kwa ushabiki tu.
 
I know the whole deal in US side, i don't know in Tanzania who does what.
In US the key player alikuwa aliyekuwa balozi wetu, and some other fox in Houston, Texas. However, Richmond owner get this deal through one of the TANESCO top leader. I believe EL didn't know this ex Tanzanian citizen who i know him personal. However i can't prove kwamba EL was part of the deal.

Richmond owner (once a houstonian Millioner) knows one of TANESCO top management leader, and he influance the deal to be assigned to Richmond. However, huyu meneja wa TANESCO aliweza kutumia influance ya mmoja wa watu wake wa karibu ambaye anajuana na JK personal, na maongezi ya kumshawishi JK kuwapa Richmond tender yalifanyika mwaka jana JK alipokuja US kwenye UN summit. I recently conect the dots and say shi*****
http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=84561#post84561

Hiyo ilikuwa moja ya post zangu za mwezi wa nane mwaka jana wakati scandal hii ilipofumuka.
Go back to the point, Huyo manager wa Dowans ni huyo mshikaji nilimuelezea hapo juu kabla report ya Mwakyembe haijatoka. Sasa huyu Mr Saleh alikuwa member wa board ya madairector ya TANESCO na yeye alikuwa mshikaji kabisa na Gire, wanajuana for years.

Huyu mzee Mwanae kaolewa na body wa Jakaya kabisa, mshikaji wake tangu mambo ya nje. Sasa ukiniambia Jakaya alikuwa hajui kama hii ni scum nashindwa kuelewa. Tangu mwanzo nilisema sina uhakika Lowassa kahusika vipi, sema Jakaya nina 100% anajua hili deal zima.

Insider wangu tulifahamu hii deal kabla haijafunikwa, na ndio kisa cha Endrew Daraja kuhamishwa ubalozini hapa US na mheshimiwa. Kusema kweli hii nightmare JK anaifahamu lakini analeta kiburi. I wish wamkamate huyu mkurugenzi wa DOWAS ajibu mashitaka ya kununua nyumba US, where did he got the $$$
 
Mkuu Dar-Es-Saalam,

Heshima mbele, kwenye nchi ya kusadikika hakuna kukurupuka maana mafisadi are very good at making things like IPTL looks like serikali ilikurupuka, no way kila ishus inapangwa kwa mkao wa kula, off course somebody knew kuwa watashindwa kesi, hivyo kufainiwa na kwenye kulipa hiyo fine mlo utaendelea, maana kama fine ni millioni 2, basi ujue zinalipwa tano, maana kama ushaidi ni mali hapa kusadikika basi Ditopile asingekuwa anaendelea na biashara ya asali Tabora.

Ahsante Kaka.

Kutokana na ile post ya leo asubuhi iliyofutwa haraka haraka naogopa hata kukujibu Mkuu.
 
Mahangaiko ya nini? kadiri wanavyobwabwaja ndivyo wanavyoendelea kujianika. Sasa Yonah kasema anawajua Richmond (rejea mahojiano yake na TVT)huyu anahitaji kubanwa atueleze Richmond ni nani.
 
http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=84561#post84561

Hiyo ilikuwa moja ya post zangu za mwezi wa nane mwaka jana wakati scandal hii ilipofumuka.
Go back to the point, Huyo manager wa Dowans ni huyo mshikaji nilimuelezea hapo juu kabla report ya Mwakyembe haijatoka. Sasa huyu Mr Saleh alikuwa member wa board ya madairector ya TANESCO na yeye alikuwa mshikaji kabisa na Gire, wanajuana for years.

Huyu mzee Mwanae kaolewa na body wa Jakaya kabisa, mshikaji wake tangu mambo ya nje. Sasa ukiniambia Jakaya alikuwa hajui kama hii ni scum nashindwa kuelewa. Tangu mwanzo nilisema sina uhakika Lowassa kahusika vipi, sema Jakaya nina 100% anajua hili deal zima.

Insider wangu tulifahamu hii deal kabla haijafunikwa, na ndio kisa cha Endrew Daraja kuhamishwa ubalozini hapa US na mheshimiwa. Kusema kweli hii nightmare JK anaifahamu lakini analeta kiburi. I wish wamkamate huyu mkurugenzi wa DOWAS ajibu mashitaka ya kununua nyumba US, where did he got the $$$

Kusadikika
 
Anyoyaeleza mh.Rostam Aziz(mb) yana ukweli kinadharia lakini sio katika uhalisia ambao unadhihirika kwa hiyo kama mtu mwenye akili timamu anaweza kujua maana.Richmond ni moja ya sehemu ya ufisadi ndani ya nji hii katika kipindi cha miaka 46 ya uhuru wake.
Nakumbuka hata Petro aliwahi kumkana Yesu lakini matendo yalidhihirisha kuwa yeye ni mfuasi wake sitaki kumkashifu mheshimiwa lakini pia vigezo alivyotupa havitoshi kwa mamilioni ya watanzania pamoja na anaowawakilisha katika jimbo lake la Igunga. Anatakiwa aende zaidi ya hapo na huo utajiri ameupata wapi kama sio migongoni mwetu kwa kutumia rasilimali zetu.
 
Unaushahidi uweke wazi, kwani hata nawe ukiongea bila ushahidi inakuwa ni nadharia tu.
 
Unaushahidi uweke wazi, kwani hata nawe ukiongea bila ushahidi inakuwa ni nadharia tu.

Ushahidi namba moja ni kwamba Rostam anafanya nao biashara.Je unaweza kufanya biashara na watu usio wajua ? Salva alisema mengi na kuthibitisha hili kwamba RDC wana connection nzito na RA
 
Ushahidi namba moja ni kwamba Rostam anafanya nao biashara.Je unaweza kufanya biashara na watu usio wajua ? Salva alisema mengi na kuthibitisha hili kwamba RDC wana connection nzito na RA

Wewe unasema hayo, aliyeanzisha hii thread hapo mwanzo anam-qoute Rostam akisema hivi:

“Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho,” alisema Rostam."

Upo hapo ulipo?
 
Back
Top Bottom