Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Rostam: Siwajui Richmond
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MFANYABIASHARA na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), amesema hana uhusiano wowote, na wala haijui Kampuni ya Richmond Development Company LLC ambayo ilishinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura baada ya kuingia mkataba wenye utata na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Siijui hata kidogo, siwatambui na siwafahamu. Mimi ni mfanyabiashara, sina sababu ya kuficha, kama ingekuwa ni kampuni yangu, nisingeshindwa kutekeleza mradi huo. Leo hii kutokana na kuwepo kwa mawasiliano ya kutosha, si rahisi mmiliki wa kampuni hiyo asijulikane. Mimi sidhani kama imekuwa ni ngumu kiasi hicho, alisema Rostam.
Wakati akikana kuifahamu Richmond na wamiliki wake, Rostam, alikiri kuwahi kutaka kufanya kazi na Kampuni ya Dowans Holdings S.A ambako Kampuni ya Richmond ililazimika kuhamishia mkataba wake huko, baada ya kushindwa kuutekeleza kwa muda uliowekwa.
Mimi ni mkandarasi. Nina kampuni inaitwa Caspian. Sina uhusiano na Dowans ingawa niliomba kupatiwa kazi ya ukandarasi, alisema Rostam.
Matamshi haya ya Rostam yanatokana na shaka iliyojitokeza baada ya Kamati Teule ya Bunge kueleza katika ripoti yake kwamba, iligundua kuwa Dowans iliwahi kutumia anwani ya barua pepe ya Kampuni ya Caspian Construction Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara na mwanasiasa huyo.
Akifafanua kuhusu hilo, Rostam alisema alilazimika kuacha anuani yake kwa Dowans baada ya kuomba kazi kwa kampuni hiyo.
Nilipoomba kazi kama mkandarasi, nilitakiwa kuacha anuani, unapoomba kazi lazima uache anuani, alisema kwa ufupi.
Kama alikuwa hawajui Richmond, basi anawajua Dowans! maana kama wewe ni Mkandarasi na hawa jamaa wanakujwa kusema tunatafuta mkandarasi, yeye Rostam si aliona kuwa kuna pesa za kujiengenezea kwa kuwasilisha maombi kwenye tenda?
Je hakukutana na Wakuu wa Dowans kuwashawishi kuwa Kampuni yake ya Caspian ina uwezo wa kufanya kazi za kikandarasi ambazo Dowans walikuwa wanahitaji mkandarasi mahiri?
Je kuna mtu yeyote anayejua hawa Dowans ni kina nani? sijasoma Ripoti ya Mwakyembe na nakumbuka vizuri Sitta aliwaambia wasichunguze chochote kuhusu Dowans.
Swali ni who are these Dowans folks? Ikiwa hata google haina information hata moja zaidi ya magazeti ya Tanzania na Jambo Forum kama reference points, then Rostam has an obligation to tell Taifa who are these cats!