Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

mbona tangu wiki iliyopita nilishawamegea kilichomo kwenye maeelezo hayo... ? kweli mnasubiri kitu kipya...
 
Hakuna chochote ni kutaka kucheza mechi ili mambo yaishie kimya kimya tu,hawa walikuwa waswekwe jela huko ndio ingejulikana wanachokisema kina kaukweli flani flani lakini kwenda kusemea hapo barazani si ndio maskani yao hao ,wakiondoka hapo kila mmoja anatanua kivyake maana hakuna anaeweza kumfanya kitu mwenzake ni kulindana tu.
 
na Happiness Katabazi

MAELEZO binafsi ya maandishi ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz yanayolenga kutoa utetezi kuhusu kuhusishwa kwake katika sakata la mkataba wa kufua umeme wa dharura kati ya Kampuni ya Richmond na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), yanaonekana kuwashtua Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Dodoma zinaeleza kuwa, Rostam aliwasilisha maelezo yake binafsi kwa Spika juzi jioni majira ya saa 12:30, saa chache baada ya kupewa maelekezo yaliyokuwa yakimtaka afanye hivyo, siku moja kabla hajapewa fursa ya kujibu Azimio la Bunge.

Hata hivyo pamoja na kukidhi maelekezo hayo ya kikanuni, Rostam alishindwa kutoa maelezo yake hayo binafsi bungeni jana kutokana na sababu ambazo hadi hivi sasa gazeti hili halijaweza kuzithibitisha.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya Bunge zinaeleza kuwa, maelezo hayo ya Rostam yanaonekana dhahiri kubeba ujumbe unaoweza kusababisha kutokea kwa mtikisiko mwingine ndani ya Bunge, baada ya ule wa Richmond ambao ulisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari hizo, uzito wa maelezo hayo ya Rostam ambayo kwa kiwango kikubwa yanaonekana kukilemea chama tawala, ulisababisha mapema jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alazimike kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya CCM muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa jana mchana.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Rostam kuhusu maelezo yake binafsi jana, mbunge huyo hakuwa tayari kueleza lolote kwa undani zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na ofisi za Bunge kwani yeye alikuwa ameshatekeleza maelekezo ya Spika.

“Nadhani mimi sina lolote la kusema la zaidi. Ninachoweza kukwambia ndugu yangu ni kwamba, niliwasilisha maelezo yangu ya maandishi kwa Spika jana jioni (Jumatano). Nasubiri kupangiwa muda wa kuyasema ndani ya Bunge kama nilivyoelekezwa katika mkutano uliopita wa Bunge. Watafuteni wahusika,” alisema Rostam huku akikataa kutoa maelezo mengine yoyote ya ziada.

Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na Spika Sitta jana mchana, alikiri kupokea maelezo ya mbunge huyo kwa maandishi juzi majira ya saa 12:00 jioni na akasema tayari alikuwa ameshaanza kuyafanyia kazi.
Alisema baada ya kukabidhiwa maelezo hayo, jana asubuhi aliyapeleka kwa washauri wake ambao ni maofisa wa Bunge ili waweze kuyachambua kitaalam na kisha kumpatia ushauri unaofaa, kabla ya kumruhusu Rostam kuwasilisha utetezi wake huo.

“Mimi ni Spika, nina washauri wangu, hivyo nimewakabidhi maelezo (ya Rostam) ili wayachambue kitaalam na wakimaliza watakuja kunishauri, na ushauri huo ndiyo utakaoniruhusu nimpangie tarehe ya kuwasilisha maelezo yake bungeni au la,” alisema Spika Sitta.

Alipotakiwa kueleza iwapo kikao cha Kamati ya Uongozi cha CCM kilichoitishwa jana kinahusu maelezo hayo ya Rostam, Sitta alisema aliyekiitisha ni Waziri Mkuu na si yeye.

Pamoja na kukiri kuwa katika kikao hicho cha Kamati ya Uongozi ya CCM kilichoketi jana hiyo, suala hilo la Rostam lilikuwa moja ya mambo yaliyojadiliwa, Spika alisema kililenga kuzungumzia ajenda mbalimbali ambazo zimeibuka ndani ya Bunge hilo katika siku za karibuni.

Alipotakiwa kueleza nini kilikuwa kimejiri ndani ya kikao hicho kuhusu hatima ya maelezo binafsi ya Rostam, alisema yeye binafsi alishindwa kuhudhuria kwa kuwa, wakati kikifanyika alikuwa na ugeni wa Balozi wa Uingereza hapa nchini, aliyekwenda ofisini kwake kumuaga.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba, hoja ya Rostam ilijadiliwa kwa zaidi ya saa moja, na kwamba baadhi ya wajumbe walifikia hatua ya kumtaka aiondoe, pendekezo ambalo hadi jana jioni mbunge huyo alikuwa amelikataa.

Mbunge mmoja wa CCM aliyezungumza na gazeti hili jana jioni ambaye alikiri kuyaona maelezo hayo binafsi ya Rostam, anasema kikubwa kinacholeta wasiwasi ni nini kinachoweza kutokea iwapo mbunge huyo wa Igunga ataruhusiwa kutoa utetezi wake bungeni.

“Mambo yamekuwa mazito, wakubwa wamejadili hoja hii kwa zaidi ya saa nzima. Tumeambiwa kuwa wamemtaka ayaondoe maelezo yake yanayoeleza mambo mengi mapya kuhusu Kamati Teule ya Richmond iliyoongozwa na Dk. (Harrison) Mwakyembe. Mimi nimeyasoma maelezo hayo ya Rostam, tunasubiri tuone nini kitatokea ingawa naamini ni mambo mazito,” alisema mbunge huyo.

Alisema, katika maelezo yake hayo, Rostam anatarajia kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu namna Kamati ya Mwakyembe ilivyofanya kazi, kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri wengine wawili, na namna yeye mwenyewe alivyohusishwa katika sakata hilo.

Hali hii imefikia hapo baada ya juzi, Sitta kumzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni akimtaka kwanza atimize masharti ya kanuni za Bunge yanayomtaka kuwasilisha kwake (Spika) hoja yake kabla hajaitoa bungeni.

“Nilimwambia haiwezekani akawasilishe maelezo yake kabla hajawasilisha kwa Spika kwa maandishi na nimemwelekeza arudi akayaandike maelezo yake, kisha ayawasilishe kwangu, angalau siku moja kabla, ndipo nitamruhusu asimame bungeni na kutoa maelezo yake.

“Baada ya kumwelekeza hivyo, Rostam alinielewa na akaniaidi kwamba atafanya kama nilivyomwelekeza, hivyo akileta kesho (jana Alhamisi) maelezo yake, basi kesho kutwa (leo) nitamruhusu ayatoe,” alisema Sitta alipozungumza na gazeti hili juzi.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Na.50 (1), mbunge yeyote anaweza kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii.
Hata hivyo kanuni hiyo ya 50 (2) inaonyesha dhahiri kutoa unafuu kwa mbunge mwenye maelezo binafsi, ambayo akishayatoa katika muda usiozidi dakika 15, basi hakutakuwa na mjadala kuhusu jambo hilo.

Uamuzi wa Rostam kutoa maelezo yake binafsi unatokana na Azimio la Bunge lililofikiwa baada ya ombi lililotolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wenye utata wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, iliyoingia na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alilazimika kutoa hoja ya kulitaka Bunge lidai maelezo binafsi kutoka kwa Rostam, baada ya mbunge huyo wa Igunga, ambaye jina lake lilitajwa katika ripoti ya kamati teule ya Bunge likimhusisha na mkataba huo wenye utata wa Richmond, kuipinga ripoti ya kamati teule.

Rostam katika mchango wake wa kujadili ripoti hiyo ya kamati teule, alikanusha kuhusika katika na kampuni hiyo, na akaeleza wasiwasi wake kwamba, kamati hiyo iliendelea kufanya kazi nje ya muda wake ambao ulimalizika Desemba 31, mwaka jana.
 
[media]http://www.youtube.com/watch?v=ps_0X06ItqY[/media]

its only a matter of time kabla hatujaanza taifisha mali zako!!
 
get your dancing shoes... the game is about to begin.. Rostam ajiandaa kujibu mapigo..
 
bimdogo, habari za mpango wa Rostam tuliziweka hapa na contents za hicho anachoandaa kinajulikana.. naona mada ikatupwa kwenye hoja binafsi lakini siku hizi chache magazeti yako "Rostam Rostam"... wangerudi kwenye "Agenda 21"...
 
Jamani mnaona jinsi kenya wanavyowapeleke hawamafisadi court bila blah blah oooh wana hela etc etc...
 
Jamani mnaona jinsi kenya wanavyowapeleke hawamafisadi court bila blah blah oooh wana hela etc etc...

Kapinga

Ni muda tu ngoja akina Kikwete waanguke kwenye chaguzi maana kadri hali inavyokwenda lolote laweza kutokea mbele ya safari, kila siku atakuwa anapelekwa FISADI mmoja mmoja.

Hao hao wanaolinda hii MIFISADI ndio watasaidia kuipeleka baada ya kuondoka wanaowakingia kifua.
 
Kapinga

Ni muda tu ngoja akina Kikwete waanguke kwenye chaguzi maana kadri hali inavyokwenda lolote laweza kutokea mbele ya safari, kila siku atakuwa anapelekwa FISADI mmoja mmoja.

Hao hao wanaolinda hii MIFISADI ndio watasaidia kuipeleka baada ya kuondoka wanaowakingia kifua.

Kwa KATIBA tuliyonayo hakuna atakaezurika wote wataiba na kuyoyomea kusikojulina wakiona mnawakera sana.
 
mie nilizani tayari mkuu keshatapika kile kilichomo kifuani mwake.

leo ndio ijumaa vipi huyu bw mdodo au mkubwa kwa wengine keshaongea ?
 
Aruhusiwe kusema yake mbona anazibwa mdomo? Kwani si kila mtu ana haki ya kujieleza na kusikilizwa? Sisi tunapenda kusikia upande wake unasemaje na kama ni pumba tutaziona na kama nimchele tutauona; Mzee Sita acha uhuru wa kikatiba ufanye kazi hapo.
 
Ndio maana wengine tulikuwa tunatetea Lowasa kupewa nafasi ya kusema nje na ndani ya bunge, lakini kwa msaada wa pundits, wanasheria na intellectuals wa Tanzania akazimwa. Tuendelee kukumbushana kuwa uhuru wa kusema na kusikilizwa ni pamoja na kumpa mtu nafasi ya kusema hata yale usiyotaka kuyasikia. Basi tupige baragumu angalau huyu ndugu yetu apewe nafasi ya kusema.

Kadri siku zinavyokwenda tutamkumbuka sana ndugu yetu Pundit ( wa hapa JF) aliyesema kuwa ripoti ya kamati ya Mwakyembe imekaa mkao wa kumalizana na kujengana kisiasa zaidi kuliko kutafuta ukweli kuhusu Richmond. As days go by, it seems like Pundit will be "vindicated" and others will be proven to have been utterly wrong!
 
Jamani wats the difference between the the Goldenberg Scandal in Kenya in the early 1990's and EPA 2005 Tanzania???

is Richmond paying back the money taken from EPA??

Embu someni chini hapa...alafu tuambieni tofauti ya Pattni Kenya na Rostam Tanzania ni IPI???

Understanding Kamlesh Patni's Goldenberg Scandal
Goldenberg And Kamlesh Patni's Idea That Solved A Short-term Problem…

…But Created Another That Our Great Grand Children Will Still Be Grappling With decades from now

In the early hours of this morning I switched on my TV to the Trinity Broadcasting Network (TBN) channel, only to be greeted by a site that brought tears to my eyes.

American inspirational preacher Bishop T.D. Jakes was distributing food to Kenyans desperately scrambling for it. The people whose hands were reaching out in pleas for the Bishop's handouts were not children but older, once respectable mostly middle aged Kenyans who have now obviously reached the end of themselves.

The Bishop's words to the sponsors of his ministry in the United States made my tears flow faster. He said, "All these people need is a chance…"

I quickly switched off the TV and sat down to write my blog entry for today, determined to tell the story of how exactly those poor Kenyans screaming and begging for handouts ended up where they are today. It can all be traced back to mega-scandals like Anglo Leasing and Goldenberg.

During The John Githongo BBC interview, he was asked a question that is difficult to answer in one brief comment. The question was, "what is the impact of corruption on the ordinary Kenyan?"

I appreciate that not all readers of this blog are Economics majors from some university so I will tell you a story to illustrate exactly what happened to those poor Kenyans and many like them all over the country. Heck, even to you and me.

Once upon a time there was a peaceful village where every villager had a fighting chance. All they did at this village was rear goats, thousands of them. They ate the meat and drank the milk from goats. Goats were so important that they were the currency or legal tender for trading at this village.

One day the wise old chief of the village died and after they buried him under the mango tree (as he had requested), a new leader took over the reigns of power at this goat village. Somebody advised the new village chief that he would grow popular with the people by abolishing taxes. He was advised go into business for himself using all the vast resources already at his disposal. Since nobody knew any other business at this village, he naturally opted to go into the business of rearing goats.

Within no time, the king had a much larger herd of goats than all the villagers put together. In other words, the number of goats at this village had increased by more than 100 per cent virtually overnight. And surely this was a good thing because there was more wealth at the village and besides villagers no longer needed to pay any taxes to the chief.

However soon the villagers realized that they were facing a serious crisis. The goats were the only currency used at this village. People exchanged goat milk for small items and if they wanted to make a big purchase like buying land, they exchanged several goats for it.

Because there were suddenly too many goats in the village without an increase in other resources, the value of this goat currency fell dramatically. Land that people would often ask 10 goats for, they now asked for 30 or 35 goats. And they still ended up getting a buyer. Usually it was the chief himself who now actively purchased vast tracts of land to graze his rapidly growing goat population, or sometimes it was a member of his family.

So, guess what happened? Prices were raised even higher to 65 to 70 goats for land that was purchased the previous day for only 35 goats. Actually prices were now climbing at an uncontrollable rate. The villagers were simple people and they never really understood what hit them but they noted that their wealth was wiped out overnight, even as their leader and his immediate family got wealthier by the day and ended up owning vast tracks of land.

They had wildly cheered the new chief when he had announced the abolition of taxes. But then shortly after that, everything had suddenly started getting too expensive. Now they longed for the village to go back to the good old days when they paid taxes but were prosperous.

The sad ending to this tale is that the once prosperous villagers all ended up with no goats and were forced to go to work on their chief's vast tracks of land in exchange for food.

The evil chief had no problem with the new state of affairs. He was now the richest chief ever and his subjects were so poor that all of them virtually worked for him. His political advisors were delighted. It meant that it was unlikely that anybody would oppose him.

Inflation is a complex subject, but this is a simple illustration that illustrates it. Some economists call it the situation where too much money is chasing too few goods. It is important to understand inflation so as to fully grasp and understand the impact of Goldenberg, Anglo leasing and all the other scandals that have conspired to bring ordinary Kenyans down to their knees. Government promoted economic crimes that have turned a once prosperous people into beggars fit only to labor for food on land they no longer own, even as their leaders and his close associates get richer by the day.

Kamlesh Patni's Business Idea

Those who have been following the Goldenberg saga closely will not have missed Kamlesh Patni's arrogance. The chief architect of the Goldenberg scandal seems to believe that he is innocent and that he in fact did the country a great favor.

There are those who would agree with him although this blogger is not one of them. Still it is important to understand why Patni believes what he believes.

The World Bank's decision to cut off Aid to Kenya in the late 80s was just one of the reasons that caused a serious foreign exchange crunch at Treasury. The other reasons were a serious decline of the coffee industry that was politically motivated to neutralize and reduce the financial power of the politically aware Kikuyu tribe. Especially those who had been close to the previous Kenyatta regime and whose stolen wealth was mostly invested in huge coffee plantations purchased from white settlers. Tourism had also slowed down due to increased international competition as previously Eastern European countries started to open up. Actually a combination of many factors almost brought down the Moi government financially.


Kamlesh Pattni: A business idea that cost many Kenyan lives

Kamlesh Pattni was then nothing more than an ambitious young entrepreneur who dared to dream big. One day Patni got what he saw as a brilliant idea to deal with the foreign exchange problem. Why not go into the business of supplying foreign currency to the government? In dealing with precious stones finding their way into the country from places like the Democratic Republic of Congo, Patni had been amazed at the sums of US dollars available in the local black market. He knew that there were enough dollars already in the country to ease the foreign exchange crisis at the treasury.

Using his contacts, his idea soon reached the corridors of power and just in time for a government now desperate for foreign currency.

The idea was simple, Patni would buy the foreign exchange in the local black market and supply it to the government at a handsome profit. The government would have its' badly needed foreign exchange and Patni would have his billions. The wananchi would not suffer the consequences of no foreign exchange, which would have been very grave indeed. Like not having paraffin to put in their stoves for cooking or petrol to run the matatus that got them to work. So everybody would be happy.

There was just one little problem. The rate of exchange in the black market was much higher than the official rate in true black market tradition. To solve that problem, the now infamous export compensation scheme was used. In this scheme the government paid out a certain percentage to exporters (in local currency) as an incentive to continue exporting more and thus earning Kenya valuable foreign currency.

We now know that Goldenberg was used to raise funds for the first multi-party elections President Moi's Kanu faced in 1992. It is said that during those memorable elections money was being distributed in cartons from a building near the University of Nairobi. So rather than the guy calling the shots saying, give so and so so much money, instead they would say give this person 10 cartons, give that other guy 100 cartons. It is said that these cartons of cash were stacked high to the roof and filled a huge un-partitioned office space. All the money was in crisp newly printed 500 notes that came to be aptly known as Patnis'.

The inflationary consequences and magnitude of this stunt and the Goldenberg scum were colossal (please refer to the story on the goat village). Some experts believe that the damage will never really be repaired.

Now you can understand the need to use the term ‘economic crimes' and ‘economic sabotage' when describing the Goldenberg and Angle leasing scandals. But then you also need to understand that Goldenberg-like and Anglo-leasing like scandals started at independence. Only that in those days, you would lose your life, if you dared try to expose them. Many brave, patriotic Kenyans including one famous one called JM Kariuki ended up dead in places like Ngong Forest with dismembered genitals.


As terrible as that was, it comes nowhere near the suffering ordinary Kenyans have gone through since independence, all because of corruption in high places.

So what is the effect of corruption on ordinary Kenyans?

Answer; Too tragic to explain in words. Hopelessness, lost opportunities and a situation where working hard and honestly no longer pays. Little wonder that so many youngsters in Kenya today have now opted for a life in serious violent crime. Corruption results in deaths and irreversible damage and suffering to the lives of millions of citizens. It is a great injustice that those who kill one person are hanged and yet those who kill millions by practicing corruption continue to enjoy life and hire expensive lawyers every time their names are mentioned adversely.

Corruption in Kenya has been a great injustice to the ordinary person who wants nothing more than a chance. A chance to fend for themselves and fight for a better tomorrow.
 
Back
Top Bottom