Kati ya wabunge ambao inadaiwa wana ushawishi sana kwenye serikali na nje ya serikali ni Mbunge wa Igunga Mhe. Rostam Aziz (CCM) Siyo tu Bungeni lakini pia jina lake limekuwa likitajwa katika mambo mbalimbali na hivyo kumfanya kuwa ni miongoni mwa wabunge wenye "ushawishi" wa aina fulani na wenye nguvu ya aina fulani. Kuna watu wanaomini kuwa yeye ndiyo "King Maker" wa Tanzania. Je ushahidi ukoje. Ufuatao ni wasifu wa Mhe. Aziz ambao licha ya kutojibu maswali, unazua maswali mengi zaidi na kubwa zaidi ambalo binafsi ningependa kusaidiwa majibu yake ni "Mchango mkubwa wa Bw. Rostam kwa taifa letu ni nini"?
Je, ni ajira, kuanzisha vyombo vya habari n.k Je yawezekana kuwa kule Bungeni kwa miaka miwili Bw. Aziz hajawahahi kusema kitu chochote? Na kama amewahi imekuwaje kuwa tovuti ya Bunge haionyeshi mchango wake hata mmoja? Kwanini miaka miwili baadaye hata wasifu wake wameshindwa kuumalizia? Mbunge huyu mwenye utata, kweli anazo nguvu anazodaiwa kuwa nazo au ni uonevu wa wapinzani wake wa kisiasa?. Binafsi sina jibu. wewe unalo?