mwanaizaya
Senior Member
- Apr 26, 2008
- 133
- 1
Kuna swali moja ambalo ameulizwa mwisho na waandishi kuhusu Richmond na ambalo jibu lako ukilisikia kwa wengine linaridhisha lakini kwa mtu anayesikiliiza makini atagundua Rostam amefanya kitu gani katika jibu hilo.
Ndani ya nusu saa zijazo mtamsikia wenyewe akielezea mambo haya.
Nina mashaka kwamba wale wanaomsema Rostam Aziz, kuna siku wanaweza kutafuta sehemu ya kujificha... maana mpaka leo hakuna tangible evidence za uchafu wa Rostam Aziz zaidi ya kwamba jamaa wa watu utajiri wake labda ndio unamponza ikiwa ni pamoja na Rangi yake... Lakini wananchi anaowawaklisha angalau bado wako naye.
Hili la Watanzania miongoni mwetu kuendelea kuwasupport mafisadi linasikitisha sana. Mafisadi wanaiba mabilioni ya pesa wakitoa vimilioni vichache hapa na pale basi wanaonekana ni watu wa maana sana!!!
Mtu ukiwa safi kamwe hutashindwa kutetea jinsi ulivyoupata utajiri wako kwa njia za halali, ukishindwa kufanya hivyo basi huo utajiri umepatikana kwa njia za haramu. Asitake kuhamisha burden of the proof kwa Watanzania.
Hii hoja kwamba RA anaponzwa na rangi kamwe haiwezi kuwa na nguvu yeyote. Je, umesoma hapa jinsi wachangiaji mbali mbali walivyowakalia kooni mafisadi wengine akiwemo Mkapa, Mramba, Chenge, Karamagi, Mkono, Mzindakaya n.k. je hawa no wanaponzwa na rangi zao!!!!? π
jamani huo waraka wake huko wapi? na nitawezaje kusikia kupitia KLH news?nafungua mtandao sioni dalili ya hayo mahojiano somebody HELP
Si ninyi mliosema kwamba Chenge wa watu alionekana kwenye Kamera... sasa imekua je tena...
Kama una uthibitisho kwamba mimi nilichangia chochote kuhusu hili la Chenge kuonekana Bungeni akinyunyizia alivyonyunyizia kwenye viti vya wabunge, basi uweke uthibitisho huo hapa hadharani
QUOTE=Kasheshe;246194]Mimi naona kama tunapaza sauti tu kama za uumini kwenye imani fulani...
Kwa hiyo JK aingilie suala hili kama nani, Rais ama rafiki?
Nina uhakika RA ana marafiki wengi, tena anaowaheshimu zaidi ya Rais wetu! Sasa kwanini tuanze kufikiri kuwa ni JK pekee anayeweza kusuluhisha hili.