Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Habarini Za Asbh
Mhe R.aziz Leo Hi Ametoa Dukuduku Lake Na Kusema Yale Yote Yanaongolewaa Ni Kutokana Na Wivu Juu Yake Na Wengine Ni Kuona Yeye Anawabania Ili Biashara Zao Zisifanikiwe,,
Akitoa Mawazo Yake Amesema Kumekuwa Na Pepo Mchafu Kwa Baadhi Ya Watu ,,na Katika Hili Kuna Baadhi Ya Watu Walio Madarakani Ambao Hawaridhiki Na Vyeo Alivyokuwa Nao Na Wengine Kuona Kama Rosta Anawazibia Kwenye Biashara Zao....
Mwisho Akaawaasa Viongozi Wa Dini Kutaka Kutumiwa Na Hawa Watu Wanaojiita Watakatifu Na Kuchafua Hekalu Kupitia Mgongo Wa Watu Mwisho Wa Kunukuu
Ahsanten
 
Kuna swali moja ambalo ameulizwa mwisho na waandishi kuhusu Richmond na ambalo jibu lako ukilisikia kwa wengine linaridhisha lakini kwa mtu anayesikiliiza makini atagundua Rostam amefanya kitu gani katika jibu hilo.

Ndani ya nusu saa zijazo mtamsikia wenyewe akielezea mambo haya.

Una yako!!! maana pamoja na kumwandika huyu jamaa mara nyingi kwenye post zako.. lakini hakuna tangible evidence ... hata moja!!! Tunasubiri another spin...
 
Kaka acha kupotosha ukweli na heading yako.hajasema kuwa wivu na uwezo wa vyeo unawasumbua watanzania bali kasema kuwa unawasumbua watu wachache ambao wanamtungia majungu...acha kupotosha habari hapa kwa faida yako.
 
Last edited by a moderator:
JMushi1,

Simba mla nyama za watu ni SERIKALI yenyewe!... kesi zote toka Rada, Ujenzi wa BoT, EPA, U name it zote zimekwisha fikishwa hoja bungeni na kila ushihidi uliotolewa umetupwa kapuni kupitia vyombo vyake iwe Takukuru, bunge, Ikulu na hata Bunge limegeuzwa kuwa kikao cha Simba hawa... Kumbuka tu siku zote Simba hawindi peke yake huwa ktk makundi makundi ambayo wao hujuana..watu kama kina Dr. Slaa wamefanywa mafisi waliovizia mabaki ya mifupa na amtumbo ambayo bado hayawezi kudhihirisha ni mnyama gani aliyeuawa (Ushahidi)..
Kina Rostam wanafuta meno tu na vijiti chini ya kivuli baada ya kula saaafi..na mawindo bado yanaendelea unajua tena Simba ni lazima awinde kila siku... Maisha yake yote swala kubwa ni KULA tu...
Maadam mnyama huyu USHAHIDI wanaye wao na ushahidi wetu sisi ni macho ya mtazamaji sii rahisi kwetu kushinda mahala popote kwani kuona kwetu sii contrete evidence..uta present vipi kitu ulichokiona kwa macho!
Mkuu, kutokana na maelezo ya Rostam ambayo ndio lugha kubwa ya wanasiasa nchini.
My take, Something is seriously wrong in how our government determines who and what constitutes Grand Corruption!...Inatisha sana!
Sheria zetu zimeshindwa kumtetea mwananchi maskini ambaye hana ufunguo wa nyaraka za serikali...yet anadaiwa kuzionyesha ili apate kuaminiwa.
 
Nina mashaka kwamba wale wanaomsema Rostam Aziz, kuna siku wanaweza kutafuta sehemu ya kujificha... maana mpaka leo hakuna tangible evidence za uchafu wa Rostam Aziz zaidi ya kwamba jamaa wa watu utajiri wake labda ndio unamponza ikiwa ni pamoja na Rangi yake... Lakini wananchi anaowawaklisha angalau bado wako naye.

Hili la Watanzania miongoni mwetu kuendelea kuwasupport mafisadi linasikitisha sana. Mafisadi wanaiba mabilioni ya pesa wakitoa vimilioni vichache hapa na pale basi wanaonekana ni watu wa maana sana pamoja na kuwa ufisadi wanaoufanya dhidi ya nchi yetu unawaangamiza wengi na kufanya tusiwe na maendeleo yoyote.

Mtu ukiwa safi kamwe hutashindwa kutetea jinsi ulivyoupata utajiri wako kwa njia za halali, ukishindwa kufanya hivyo basi huo utajiri umepatikana kwa njia za haramu. Asitake kuhamisha burden of proof kwa Watanzania.

Hii hoja kwamba RA anaponzwa na rangi kamwe haiwezi kuwa na nguvu yeyote. Je, umesoma hapa JF jinsi wachangiaji mbali mbali walivyowakalia kooni mafisadi wengine akiwemo Mkapa, Mramba, Chenge, Karamagi, Mkono, Mzindakaya n.k. je hawa nao wanaponzwa na rangi zao!!!!? 😕
 
Rostam ni mmojawapo wa political think-tanks wa Tanganyika. Ninaumia moyoni ninapousoma waraka wake kwa waandishi habari kwamba mtu kama huyu, ukijumuisha na political think-tanks wengine kama akina Makamba, Kingunge et al, ndio wanaotathmini mustakabali wa nchi yetu. Minds zao zimejaa maneno ya uswahilini na udaku-udaku tu badala ya kuzungumza maneno yenye ku-make sense kulingana na nyadhifa zao kubwa kitaifa. Kikwete na washikaji wake kwa mara nyingine wanatuonesha kwamba wao ni watu wa aina gani.

Tanganyika ina strategic thinkers wengi tu ambao wangeweza kuliondoa taifa katika shimo hili la giza. Tunahitaji watu wenye kuelewa maana ya uongozi kwamba kuongoza watu si lele mama. We need a change.

Kitu cha maana ni sisi kuanzisha strategies zenye kueleweka ambazo zitakifundisha hiki kikundi cha kishkaji a good lesson..... That is, kuwabwaga ngwara ya uhakika kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2010.
 
jamani huo waraka wake huko wapi? na nitawezaje kusikia kupitia KLH news?nafungua mtandao sioni dalili ya hayo mahojiano somebody HELP
 
Hili la Watanzania miongoni mwetu kuendelea kuwasupport mafisadi linasikitisha sana. Mafisadi wanaiba mabilioni ya pesa wakitoa vimilioni vichache hapa na pale basi wanaonekana ni watu wa maana sana!!!

Mtu ukiwa safi kamwe hutashindwa kutetea jinsi ulivyoupata utajiri wako kwa njia za halali, ukishindwa kufanya hivyo basi huo utajiri umepatikana kwa njia za haramu. Asitake kuhamisha burden of the proof kwa Watanzania.

Hii hoja kwamba RA anaponzwa na rangi kamwe haiwezi kuwa na nguvu yeyote. Je, umesoma hapa jinsi wachangiaji mbali mbali walivyowakalia kooni mafisadi wengine akiwemo Mkapa, Mramba, Chenge, Karamagi, Mkono, Mzindakaya n.k. je hawa no wanaponzwa na rangi zao!!!!? 😕

Si ninyi mliosema kwamba Chenge wa watu alionekana kwenye Kamera... sasa imekua je tena...

Mtu hawezi kuwa na Hisa kwenye Dowans, Richmond, sijui nini ishindikane kuonekana wazi hapa...

Mimi naona kama tunapaza sauti tu kama za uumini kwenye imani fulani...

Mpaka sasa mimi sijaona kitu ambacho kinanifanya... ni mwone huyu jamaa ni mwizi... other than kwamba najua watanzania wanachukia watu matajiri... hili liko wazi...

I'm still struggling to see those evidences... siamini kama kweli mtu anaweza kuitwa fisadi, mwizi etc... bila clear evidence beyond any doubt!!!

Sasa Mtikila amemsema kumbe jamaa alishachukua mshiko kabla... siwaamini tena... i'm sorry!!!
 
jamani huo waraka wake huko wapi? na nitawezaje kusikia kupitia KLH news?nafungua mtandao sioni dalili ya hayo mahojiano somebody HELP

Kalenge, ingia pale KLH upande wa kulia chini kuna mahali panasema "Listen LIve" kuna option ya "High Bandwidth" na "Low Bandwidth". Chagua Low.
 
Rostam Aziz Amerithi biashara kutoka kwa familia yake... ambayo ilikuwa ya biashara tangu miaka ya 1852!!!

Mwenye ushahidi apeleke mahakamani!, maana kama Serikali ni rafiki yake... Je walioko mahakamani pia ni marafiki zake!
 
Si ninyi mliosema kwamba Chenge wa watu alionekana kwenye Kamera... sasa imekua je tena...

Kama una uthibitisho kwamba mimi nilichangia chochote kuhusu hili la Chenge kuonekana Bungeni akinyunyizia alivyonyunyizia kwenye viti vya wabunge, basi uweke uthibitisho huo hapa hadharani

QUOTE=Kasheshe;246194]Mimi naona kama tunapaza sauti tu kama za uumini kwenye imani fulani... [/QUOTE]

Hatupazi sauti tu kaka, kuna ushahidi wa kutosha kwamba katika mwaka mmoja tu 2005/2006 Shilingi bilioni 288 (133 bilioni za EPA na 155 billioni za Meremeta) zilichukukuliwa katika mazingira ya kifisadi. Nyingine zinasemekana zilingia CCM lakini hakuna hata mmoja anayekubali kuwa mweka hazina wa CCM wakati michuzi hiyo ilipotapeliwa. Kumbuka huo ni mwaka mmoja tu. Kama uchunguzi ungefanywa tangu 1995 Mkapa alipoingia madaraka labda ingegundulika kwamba wameiba mara 10 au hata ishirini ya kiasi hicho cha shilingi bilioni 288.

QUOTE=Kasheshe;246194]Mpaka sasa mimi sijaona kitu ambacho kinanifanya... ni mwone huyu jamaa ni mwizi... other than kwamba najua watanzania wanachukia watu matajiri... hili liko wazi...[/QUOTE]

Kwa taarifa yako Watanzania hatuchukii matajiri walioupata utajiri wao kwa njia za halali. Si huyo Mengi amekuwa tajiri miaka chungu nzima lakini husikii Watanzania wakimsakama kwamba ni fisadi. Kwa hiyo hakuna ukweli wowote kwamba Watanzania wanawachukia matajiri. Tunawachukia matajiri wanaoiba rasilimali zetu, misaada tunayopewa na nchi wafadhili n.k. ili kujitajirisha wao na familia zao na kuacha Watanzania walio wengi wakiishi maisha ya dhiki kubwa, badala ya utajiri huo kutumika katika kuinua maisha ya Watanzania hao.

QUOTE=Kasheshe;246194]I'm still struggling to see those evidences... siamini kama kweli mtu anaweza kuitwa fisadi, mwizi etc... bila clear evidence beyond any doubt!!![/QUOTE]

Hivi unafikiri mtu kama Mengi akiulizwa ameupata vipi utajiri wake atashindwa kujieleza!? 😕
Utajiri wa Mengi kaupata kihalali na mtu ukipata utajiri kihalali hata siku moja hutasahau au kupata kigugumizi cha kuelezea jinsi ulivyokuwa tajiri.

RA utajiri wake umepatikana kiharamu ndiyo maana hana maelezo ya kuturidhisha Watanzania. Hivi unashindwa kweli kuelezea ni biashara gani unayoifanya na umeifanya kwa miaka mingapi mpaka ikakuwezesha kuwa tajiri mkubwa wa kupindukia? Hivi wewe huoni walakini wowote kampuni inayojidai HQ ziko Houston, US kumbe ni ya kariakoo halafu inalipwa shilingi 152 millioni kwa siku pamoja na kushindwa kutimiza mkataba waliosaini wa kuzalisha umeme!!!? Ama kweli mvunja nchi ni mwananchi!!!!

Mimi na kama sikosei Watanzania walio wengi bado tunamweka RA kwenye kundi la mafisadi. Miaka michache iliyopita alikuwa mtu wa kawaida kabisa asiye na utajiri wowote ghafla bin vu kaibuka na kuwa tajiri wa kupindukia na wakati huo huo anapata kigugumizi cha kuelezea utajiri wake. Waswahili walisema panapofuka moshi hapakosi moto
 
Du! nimesikiliza... uandishi wetu bado wa makanjanja!!! inaonyesha jinsi gani waandishi wetu hawafuatilia mambo ya bunge etc.
 
Kama una uthibitisho kwamba mimi nilichangia chochote kuhusu hili la Chenge kuonekana Bungeni akinyunyizia alivyonyunyizia kwenye viti vya wabunge, basi uweke uthibitisho huo hapa hadharani

QUOTE=Kasheshe;246194]Mimi naona kama tunapaza sauti tu kama za uumini kwenye imani fulani...

Hatupazi sauti tu kaka, kuna ushahidi wa kutosha kwamba katika mwaka mmoja tu 2005/2006 Shilingi bilioni 288 (133 bilioni za EPA na 155 billioni za Meremeta) zilichukukuliwa katika mazingira ya kifisadi. Nyingine zinasemekana zilingia CCM lakini hakuna hata mmoja anayekubali kuwa mweka hazina wa CCM wakati michuzi hiyo ilipotapeliwa. Kumbuka huo ni mwaka mmoja tu. Kama uchunguzi ungefanywa tangu 1995 Mkapa alipoingia madaraka labda ingegundulika kwamba wameiba mara 10 au hata ishirini ya kiasi hicho cha shilingi bilioni 288.

QUOTE=Kasheshe;246194]Mpaka sasa mimi sijaona kitu ambacho kinanifanya... ni mwone huyu jamaa ni mwizi... other than kwamba najua watanzania wanachukia watu matajiri... hili liko wazi...[/QUOTE]

Kwa taarifa yako Watanzania hatuchukii matajiri walioupata utajiri wao kwa njia za halali. Si huyo Mengi amekuwa tajiri miaka chungu nzima lakini husikii Watanzania wakimsakama kwamba ni fisadi. Kwa hiyo hakuna ukweli wowote kwamba Watanzania wanawachukia matajiri. Tunawachukia matajiri wanaoiba rasilimali zetu, misaada tunayopewa na nchi wafadhili n.k. ili kujitajirisha wao na familia zao na kuacha Watanzania walio wengi wakiishi maisha ya dhiki kubwa, badala ya utajiri huo kutumika katika kuinua maisha ya Watanzania hao.

QUOTE=Kasheshe;246194]I'm still struggling to see those evidences... siamini kama kweli mtu anaweza kuitwa fisadi, mwizi etc... bila clear evidence beyond any doubt!!![/QUOTE]

Hivi unafikiri mtu kama Mengi akiulizwa ameupata vipi utajiri wake atashindwa kujieleza!? 😕
Utajiri wa Mengi kaupata kihalali na mtu ukipata utajiri kihalali hata siku moja hutasahau au kupata kigugumizi cha kuelezea jinsi ulivyokuwa tajiri.

RA utajiri wake umepatikana kiharamu ndiyo maana hana maelezo ya kuturidhisha Watanzania. Hivi unashindwa kweli kuelezea ni biashara gani unayoifanya na umeifanya kwa miaka mingapi mpaka ikakuwezesha kuwa tajiri mkubwa wa kupindukia? Hivi wewe huoni walakini wowote kampuni inayojidai HQ ziko Houston, US kumbe ni ya kariakoo halafu inalipwa shilingi 152 millioni kwa siku pamoja na kushindwa kutimiza mkataba waliosaini wa kuzalisha umeme!!!? Ama kweli mvunja nchi ni mwananchi!!!!

Mimi na kama sikosei Watanzania walio wengi bado tunamweka RA kwenye kundi la mafisadi. Miaka michache iliyopita alikuwa mtu wa kawaida kabisa asiye na utajiri wowote ghafla bin vu kaibuka na kuwa tajiri wa kupindukia na wakati huo huo anapata kigugumizi cha kuelezea utajiri wake. Waswahili walisema panapofuka moshi hapakosi moto
[/QUOTE]

Unaongea upupu mtupu!!!. familia iliyokuwa ya kibiashara tangu 1852... hiyo haikutoshi... ni uzembe na upuuzi mtu... ni mamlaka gani imemutaka aseme utajiri wake... acha...mambo yasiyokuwa na maana mtu mzima hawezi ropoka tu ati nimepata vipi utajiri wangu wakati hakuna chombo ambacho kina mamlaka kimeniuliza...

Ninyi si mnajua kuvuatilia mambo nenda kwa tume ya maadili ya viongozi utuletee alichoandika...
 
QUOTE]Unaongea upupu mtupu!!!. familia iliyokuwa ya kibiashara tangu 1852... hiyo haikutoshi... ni uzembe na upuuzi mtu... ni mamlaka gani imemutaka aseme utajiri wake... acha...mambo yasiyokuwa na maana mtu mzima hawezi ropoka tu ati nimepata vipi utajiri wangu wakati hakuna chombo ambacho kina mamlaka kimeniuliza...

Ninyi si mnajua kuvuatilia mambo nenda kwa tume ya maadili ya viongozi utuletee alichoandika...[/QUOTE]

Matusi ya nini tena kaka!!!, Inawezekana ni upupu kwako wewe lakini kwa wengine si upupu. Ufanye biashara tangu 1852 na ushindwe kuitaja hiyo biashara unayoifanya ni ipi!!!!? 😕

Kufanya biashara tangu 1852 hakuna maana ndiyo kutakufanya uwe tajiri. Hiyo biashara tangu 1852 alikuwa anaifanya Tanganyika au nchi nyingine!? Bado kuna utata mwingi tu dhidi ya huyu fisadi!!!
 
Bubu ataka kusema,

Hoja zako ni dhaifu sana! Maana ni kama hizo fedha zote... zimeenda kwa Rostam... kama huo ndio ushahidi kweli mnaongea upupu mtupu!!!>.. Poleni sana... kama ndio ushahidi wenu!
 
Kwa hiyo JK aingilie suala hili kama nani, Rais ama rafiki?

Nina uhakika RA ana marafiki wengi, tena anaowaheshimu zaidi ya Rais wetu! Sasa kwanini tuanze kufikiri kuwa ni JK pekee anayeweza kusuluhisha hili.

Mkuu huwezi kuwa Rais wa Jamhuri ukaruhusu haya madudu, mifano tunayo tena iko wazi sana,

muulize Idd Simba kilichomaliza career yake ya siasa, alipojaribu kutumia platform ya vurugu ya Mwembe Chai kutafuta urais, akaambiwa wazi na CC kuwa wewe ni M-Rundi tutakurudisha kwenu sasa hivi usituletee balaa hapa,

Muulize Kitine, naye alijaribu kutumia platform ya udini sijui mpaka leo yuko wapi, enzi za Mwalimu tunajua alikuwa akiwafanya nini watu kama huyu Rostam, taifa zima jana lilikuwa alert kusikiliza atasema nini huko na waandishi, wananchi wastaarabu tukidhani atasema kuhusu Global Energy crisis na effect zake kwetu Tanzania, badala yake anaenda kusema maneno ya taarabu na more nonesense!

Angekuwa Mwalimu yupo hapa huyu angempigia simu kuwa anahitaji kumuona Ikulu Jumatatu, wallahi angemlamba viboko mwenyewe Ikulu, kama Mwabulambo, mengine bwana Mwalimu alikuwa right hawa kina Rostam hawa ni kulamba viboko tu Ikulu yanaishia hapo hapo!
 
RA anasema yeye anaweza kutoa free lunch kwa akina Mtikila tu ambao hataki watoe uvundo wake; atafanya kila kinachowezekana kumwaga pesa, leo kamwaga pesa kwa waandishi wake ili waandike upupu na wengine wako hapa hapa wakiendeleza libeneke.

Je hizi pesa anaokota? Biashara anazojisifia ni za wizi tu kama alivyokuwa EL na michango yake, kwani anatumia hiyo kama nyenzo ya kuficha maovu yake.

Kama yeye ana uwezo kwa nini analialia kama kasuku? RA kama wewe ni kweli twambie unapata income kiasi gani kwenye makampuni yako? Unalipa kodi kiasi gani? Je kwa nini umpe pesa Mtikila wakati wananchi wako wa Igunga wana matatizo zaidi kuliko ya Mtikila? Ulikuwa unaogopa nini?

Utawadangaya unaowapa bahasha lakini ukweli ni kwamba wewe unatumia pesa uliyopata kwa njia haramu kuwarubuni viongozi ili ujinufaishe binafsi. Janja ya nyau tikisa makia!

Kwenye kamati ya bunge ulipoitwa ulifyata mkia leo kono juu na kimbele mbele chako biashara ya Igunga toka 1952 ni ipi hiyo? And of all places Igunga ikupe huo utajiri acha hadaa.
 
Hii kesi itafunua uozo mwingine zaidi.
 
Back
Top Bottom