Mtikila na deni lake... hajasema alitakiwa arudishe lini? Jamaa ni msaniii
Mtikila ameeleweka vya kutosha kabisa na Rostama hamwezi Mtikila hata kwa dawa.
Kwanza ushauri wangu ni kwamba naona RA aachiwe Mtikila kwenye siasa......Na kisheria pia kama utawala ukishindwa...Basi coalition yao nayo ipo...Na hawa watu wananweza kuchukuwa nchi.
Rostama mwenyewe kapewa muda wa kutosha na swahiba wake lakini nawasikitikia sana kwani hawajuwi Mtikila ni mtu mwenye Principle na ama kweli jamaa anaongea kwa makini na kila sentensi yake ni NONDO.
Mtikila kama ni kweli alikataa milioni mia nne basi huyu mtu anaona mbele.
Na pia tunajuwa alikuwa anafanya kazi kwenye mazingira magumu sana yeye kama mpinzani na kama kweli kashfa yake ni kukopa milioni tatu...Basi HUYU BADO NI SHUJAA!
Pia nilimwelewa vizuri sana pale aliposema kuwa urafiki wao haina maana kuwa asiseme mambo yanayomtia uchungu ambayo ni ya maslahi ya Kitaifa. Hapo alisema kuwa misimamo yake imepelekea kukosa marafiki ama kuwapoteza...HUYU NI KIONGOZI.
Tunaomba watanzania wamsikilize pia.
Tunaomba pia na yeye ashirikiane na wazalendo wenzake.
Tunataka pia sheria ya DPP ibadilishwe.
Pia alikumbushia yale ambayo kuna watu wengine humu ndani kama Kasheshe ambao kweli wame amua kuyafungia macho kwasababu zao binafsi.....Ama za kifisadi ama za kiitikadi...Ukweli kwamba kulikuwa na ushaidi wa kutosha kuwapiga pingu hawa watuhumiwa bila hata na haja ya kuunda kamati ya kina Mwema.
Utaratibu kwamba eti mtandao ni mkubwa na inabidi uchunguzi wa kamati uwe makini ni danganya toto ili kutaka kuimaliza issue.
Ushaidi wote wa kaguzi zote ulitosha na bado unatosha kuwafikisha mahakamani.
Kama alivyosema mchungaji Mtikila ni kuwa Rostam alifanya vibaya pale alipotoa Hotuba ya kujisafisha sambamba na utowaji wake wa sadaka.
Na ni kweli kuwa sasa hakuwa na mahali pengine pa kuendeleza vijembe vyake vya kisiasa na mbinu zake za kujisafisha zaidi ya kanisani kwani Bungeni ni mbaya na kesi inataka ifunguliwe so the noose is obviously tightening.
Ni wazi kuwa RA alikuwa na long term plans na ndio maana bila ya aibu anathubutu kutaja milioni tatu alizomkopa Mtikila.
Je kweli hata kama alimpa bure hizo milioni tatu...Hiyo je ndiyo pesa ya kumfanya Mtikila anyamaze?
Mtikila kweli angeamuwa kuwa kama kina Marando na Lamwai angeshindwa?
Na kwa maana hiyo basi...Mtikila anaona mbele na ni mtu wa Mungu pia.
Tunamuomba asigeuke wenzake tena...Aelewe pia kuwa TOGETHER WE CAN.