Nimeona niwapatie chanzo cha hasira za Rostam Aziz kwa Mch Mtikila kama ujumbe huu mzito ulivyoandikwa na Mch Mtikila mwenyewe uliogawiwa kwa waandishi wa habari wote na wabunge wote.
KAMATI YA KUPAMBANA NA UPORAJI WA NCHI
PUBLIC INTEREST LITIGATION COMMITTEE
(PILCOM)
Kamati hii ilianza kujiunda tangu mwaka 2006 na wahanga wa ukombozi wa nchi yetu, kutoka katika Vyama vya siasa, taasisi za kidini, makampuni ya wanasheria mahiri, Taasisi huru za wananchi, na mshikamano mtakatifu wa wazalendo ndani ya Bunge letu, ambalo katika Ibara ya Nane ya Katiba ya Nchi yetu ndilo linaloitwa Wananchi. Ni mbinu yetu ya vita kutowaweka wazi wahanga wetu kwa sasa.
Kazi ya Kamati ni kuwafikisha mbele ya Sheria watu wote walioshiriki katika wizi wa matrilioni ya mapesa ya Nchi yetu katika Benki Kuu na Hazina ya Taifa letu, na kurejesha mapesa yote waliyoyaiba pamoja na riba na gharama, kutoka kila walikoyaweka nje na ndani ya nchi.
Tunawahakikishia wananchi kwamba kama isemavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano hakuna mwizi aliye juu ya Sheria awe rais mstaafu au aliye madarakani, waziri, kigogo wa CCM au gabacholi jeupe au jeusi, mradi ameshiriki katika :
* Wizi wa zaidi ya Shilingi bilioni 216 za Import Support Fund,
zilizokombwa kwa sehemu kubwa na marehemu Mehboob na mwanawe
Yusuf Manji, kwa ushirikiano na vigogo wa Hazina na Tanzania
Investment Bank,
* Wizi wa matrilioni ya mapesa ya EPA, DCP, OGL,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yanayoporwa kwa hila ya
Richmond/Dowans,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa ya yaliyoporwa kwa hila Meremeta na
Tangold,
* Wizi wa matrilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hujuma za I.P.T.L,
SONGAS, AGGREKO, NETGROUP SOLUTIONS,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hila ya TICTS Bandarini,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hila ya ununuzi wa radar
na mtumba wa ndege ya rais,
* Uporaji wa shirika la TTCL kwa hila ya uwekezaji wa kampuni ya MSI,
Celtel na SIMU 2000,
* Uporaji wa Benki ya Taifa ya Biashara nyuma ya mgongo wa makaburu
wa ABSA,
* Uporaji wa madini yetu yote ya Tanzanite nyuma ya mgongo wa
makaburu wa AFGEM
* Uporaji wa migodi yetu ya dhahabu nyuma ya migongo ya akina James
Sinclair, Barrick Gold, Ashanti Gold na wengine,
* Uporaji wa majumba ya serikali ya matrilioni ya fedha kuwa mali za
Vigogo wa CCM na wezi wenzao,
Kwa vile Rais Kikwete anahusika katika uporaji huu ambao ulimnufaisha hata katika hila za mtandao wake za kumwingiza Ikulu, na kutokana na udhaifu wake mkubwa wa kujali zaidi maslahi ya kibinafsi na maswahiba kuliko hatima ya nchi na walalahoi, tulifahamu kabla ya tamko lake kwamba atamtumia Mkurugenzi wa Mashitaka (Director of Public Prosecution) kuwalinda wote waliohusika katika uporaji wa Nchi pamoja na mtuhumiwa mkuu Benjamin William Mkapa.
Ndiyo maana Kamati hii ilianza kazi yake mwaka 2006 kwa kufungua kesi ya Katiba Nambari 86/2006 ili kumwondolea Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka makubwa mno kupita matakwa ya Katiba ya Nchi, yaliyompa uwezo wa kuwalinda maharamia wote ambao Rais hatataka washitakiwe na kufungwa na kufilisiwa. Ndipo unaposimama ujasiri wa Kikwete wa kutamba kwamba atayalinda majizi ya mapesa yetu ya EPA, Richmond/Dowans yasifikishwe mahakamani! Tunataka haki ya wananchi ya kujiendeshea mashitaka wao wenyewe wasipokuwa na imani na DPP.
Swali zito ni Kwanini Mahakama Kuu haitoi hukumu ya kesi hii nyeti ya hatima ya Nchi yetu na uhuru wetu?
Bunge na serikali ni mali ya wananchi, mahakama pia ni mali ya wananchi. Ni mwiko kuingilia uhuru wa Mahakama, lakini ni lazima tupambanue kati ya uhuru na usaliti wa Mahakama. Waheshimiwa Majaji wetu wote ni raia wa nchi yetu, kwahiyo wanafungwa pamoja na raia wenzao wote na Ibara ya 27 ya Katiba ya Nchi kwamba wanao wajibu wa:
kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na kwamba wanatakiwa kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.
Kwa uzalendo huu walioapa mbele za Mwenyezi Mungu na watu wote wa Nchi hii kuufanyia kazi, kesi nyeti namna hii ilitarajiwa kupewa kipaumbele inavyopasa, hata kama waheshimiwa Majaji wana milundikano mikubwa kiasi gani ya makesi mbele zao. Mungu waliyemwapia hataki kabisa kiburi na majigambo ya vigogo wa CCM kwamba eti mahakama ni yao, kwa sababu ni yake Yeye na haki ni utukufu wake Yeye.
Ndiyo maana baada ya kudhalilishwa majaji wake pamoja na wanahabari pale Mahakama Kuu, katika makufuru ya kesi ya mauaji ya kikatili ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, Mungu alishindwa kuchukuliana na uovu ule akamtwaa mtuhumiwa kuwa ishara! Unabii unaonya kwamba kama Kikwete atajifanya hakumwelewa Mungu, basi katika uporaji huu wa kutisha ataambiwa kwa herufi kubwa.
Kamati hii inangoja uamuzi wa Mahakama Kuu katika Kesi ya Katiba Nambari 86/2006, na tayari imewataka Gavana wa Benki Kuu na Mheshimiwa Spika wa Bunge letu waipatie taarifa muhimu za wizi wote uliofanywa na wahusika wote, ili Sheria ichukue mkondo wake dhidi yao wote.
Aidha Kamati inamtaka Rais Kikwete amwondoe maramoja Mustafa Mkullo katika Wizara ya Fedha, baada ya kudhihirika bayana kwamba ni mtu mwovu na wa hatari kwa maslahi ya Nchi kupita kiasi. Hata mwendawazimu hawezi kumkabidhi chui mwenye njaa amtunzie mbuzi wake.
Waziri Mkuu Mizengo K. Peter Pinda aliweka nadhiri kwa Mungu, kwamba kama atajihusisha katika ufisadi Mwenyezi Mungu amnyanganye roho aitupe hukumuni. Hivyo ni lazima ahakikishe kwamba wote waliohusika na wizi wa mapesa ya EPA/DCP/OGL, Richmond/Dowans n.k. wanashitakiwa maramoja na mapesa yanarejeshwa pamoja na riba. Mungu hachezewi!
Ikiwa watuhumiwa wamefanya uporaji kama chama yaani CCM, basi lazima genge lote litokomezwe. La sivyo damu itamwagika vibaya sana katika nchi hii kwa uporaji huu, kama Bunge halitaachiwa kutekeleza kazi ya wananchi ipasavyo, na Mahakama kufanya kazi yake!
HATIMA YA MWAJEMI SAKARIR (ROSTAM) AZIZ
Kiini cha ufisadi wa kutisha na uporaji wa Nchi yetu, unaofanywa kama vile Watanganyika wote ni mataahira, ni kutoweka kwa uraia wa kweli wa kuipenda nchi yetu na kuwa na uchungu nayo wa kiwango cha uhanga kwa ajili yake. Kwa sababu ya utaahira wetu nchi yetu imekamatwa na mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliuofanyika katika Benki Kuu na Hazina ya Nchi yetu, ambaye ni Mwajemi yaani raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya mataahira kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la Rostam. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ngombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.
Nilipoanza kuzungumzia uraia wa Rostam Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo, ingawa alisahau kwamba Premji wa Kigoma alizaliwa hapa lakini hakuwa raia kwa sababu wazazi wake hawakuwa wameukana uraia wa kwao, wala yeye Premji hakuwa ameomba uraia kwa mujibu wa Sheria, hata kama aliweza kujipatia Passport ya nchi hii kwa njia za ufisadi kama alivyofanya yeye. Rostam amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli.
Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya Nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu.
Kwa ufupi Sakarir alipofika nchini mwetu baada ya masomo yake Uingereza, aliunganishwa na viongozi watatu wa CCM waliokuwa marafiki sana ambao ni pamoja na Rais Kikwete. Rostam alipata nguvu ya kisiasa kwa kutumia mapesa mengi ya mfuko maalum wa nchi yao wa Iranians in Diaspora, aliyoyapata kama raia mwaminifu wa Iran, aliye na shughuli zenye maslahi kwa nchi yao katika nchi ya nje. Nguvu hii ndiyo iliyomtia Benjamin Mkapa mkononi mwake na kuwa msingi wa uhuni na jeuri yote aliyonayo leo.
Mafisadi walionufaika na mtaji huo wa Sakarir Aziz ndio waliofanya uhaini wa kumpa Ubunge wa Igunga alipofariki hayati Charles Kabeho. Wazee wa Kiajemi waliolowea hapa, Hussein Heidari na Hassan nduguye ndio waliompokea kijana Sakarir Aziz kule Igunga, kwa sababu wanao uhusiano na mkewe Aziz yaani mama yake Sakarir au Rostam.
Hawa wazee ndio waliomnadi huyu Mwajemi kwa wazee wa Igunga katika kuiba Ubunge wa Nchi ya watu ambao anawachukulia kuwa mataahira. Sakarir Aziz anao nduguze wa kiume wawili yaani Jahangir Aziz ambaye alipigana kizalendo kabisa ile vita ya nchi yao dhidi ya Iraq, na wa pili ni Akram Aziz.
Kamati yetu imejitolea kuwasaidia wananchi wa Igunga wanaotaka kufungua kesi dhidi ya Sakarir Aziz na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa kuwanyima uwakilishi Bungeni tangu Mbunge wao hayati Charles Kabeho alipofariki. Kwani Mwajemi wa Jamhuri ya Kiislamu, Rostam Aziz hawajali kabisa wananchi wa Jimbo lile, hata katika maafa kama ya kukosa kabisa usafiri baada ya madaraja ya mto Mbutu kuzolewa na mafuriko, au machafuko yaliyotokana na masuala ya ushirikina.
Rostam Aziz anashirikiana katika kupora Nchi yetu na gabacholi mwingine aitwaye Yusuf Manji, ambaye pia si raia wa nchi hii na akibisha ushahidi utatolewa. Bilashaka Wabunge safari hii watataka kujua ni nani hasa waliotoa Passports za Tanzania kwa Rostam Aziz, Jahangir Aziz na Akram Aziz na kwa misingi gani.
Wezi hawa wanaipora nchi hii bila huruma, na ndio wanaowaambia watawala wa CCM cha kufanya ili wakombe mapesa yetu B.O.T na Hazina, na kutumia matrilioni yetu kuwatia viongozi wetu ndani ya mifuko ya makoti yao, ambamo wanalishwa masazo yao na kuchomoza vichwa kuchungulia nje kama vindege kuwasanifu wananchi, na kurudi mifukoni mwao wakidhani wanakula kumbe wanaliwa wao na Nchi yao! Hatutaki Rais wetu wala Wabunge wetu wawe vindege ndani ya mifuko ya makoti ya Rostam Aziz na Yusuf Manji!
Rostam na yusuf Manji wapo Dodoma na shehena ya mapesa ya EPA, kwa kazi ya kuwanunua wabunge wanaowadharau kwamba eti ni mataahira, wawe karatasi ya msalani (toilet paper) ya kuwasafisha uchafu wao halafu na yenyewe itokomee pamoja na uchafu, kwani haiwi safi tena baada ya kutumiwa!
Tunaitaka Serikali iwakamate hawa wahalifu hatari wa Taifa letu huko Dodoma na kuwapokonya makaratasi yao yote ya kusafiria na kuwaleta kizimbani maramoja kwa uharamia wote walioifanyia Nchi yetu.
Saa ya ukombozi ni sasa!
Mchungaji C. Mtikila
MWENYEKITI WA KAMATI
26/6/2008