Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

"Man is conceived in sin and born in corruption and he passeth from the stink of the didie to the stench of the shroud. -- Willie Stark in All the King's Men"
 
exactly lakini kuna faidia gani?
Faida ipo,

1.Mtikila ana kazi ya maana,hanahata Ruzuku ataishi vipi
2.Mtikila ni Msanii ,tena kama angeenda Ze comedy ingekuwa sawa.
3.Mtikila yupo kama kibanda cha kuwasidia wageni wenye shid
4.Ubongo wa Mtikila ni Nyumba ya kulala sera za kuchafuana za CCM
 
Kuna haja ya kumfuatilia kwa kina na kummulika kwa kina sana ili kuweza kujua huyu jamaa.

Ila mimi namuona naye ni fisadi tuu,tufuatilie lile Benzi lake kalipata kutoka fedha gani?

Huenda kalipata kupitia fedha za EPA kwani kalinunua baada ya issue za EPA kufanyika.

...its time kumweka wazi huyu jamaa once and for all ili kukomesha wenye tabia kama hizi,mwenye data atumwagie hapa..JEE MTIKILA KAPATA VIPI LILE BENZ LAKE? naona kule Kipanya kaamua kumbana mbavu tayari
 
Mtikila hakuanza leo (2008) kuchota pesa kwa RA, ebu mwangalie Mtikila wa kipindi cha uchaguzi mwaka 2005 hii ilikuwa Oktoba, 2005.

Dkt. Mvungi amcharukia Mchungaji Mtikila

MGOMBEA urais kupitia NCCR-Mageuzi, Dkt.Sengondo Mvungi , amekasirishwa na hatua ya Mchungaji Christopher Mtikila kuwashawishi wakazi wa Majengo mjini hapa wasimchague kuwa Rais wao Oktoba 30 mwaka huu.

Akionekana kukerwa na matamshi ya Mchungaji Mtikila, Dkt. Mvungi alidiriki hata kukataa kumuita kwa jina la Mchungaji, ambaye naye anawania urais kupitia chama cha DP.

Dkt. Mvungi aliingiwa na jazba hiyo muda mfupi tu mara baada ya kukaribisha maswali kwa wakazi wa mjini Songea na mtu mmoja alijitokeza kwenda kumuuliza swali.

Mtu huyo aliuliza, "Hivi karibuni alikuja Mchungaji Mtikila hapa na akaongea maneno yaliyonikasirisha sana kwamba tusikuchague kwa sababu ulikataa kumsaidia kisheria mahakamani na kwamba NCCR-Mageuzi, CUF na CHADEMA ni vyama mamluki na ndivyo anavyochukia kuliko vyama vyote hapa nchini kwa usaliti, je ni kweli?."

Akijibu swali hilo, kwanza Dkt. Mvungi alisema kuwa hapendelei kabisa kulumbana na wagombea wenzake wa upinzani na akamtaka Bw.Mtikila akome kumfuatafuata.

Dkt. Mvungi ambaye hapo awali hakujua kama kuna baadhi ya wagombea wanapita kwenye mikutano na kumharibia kampeni zake, alionesha dhahiri kukerwa na tabia hiyo ya Bw.Mtikila.

Huku akishangiliwa, Dkt.Mvungi alimcharukia Mtikila na kumtaka asiingilie fani za watu na alimtaka akasomee sheria kama anaweza, badala ya kupita na kuanza kuharibu majina ya watu.

Dkt. Mvungi alisema kuwa anawajua vilivyo wagombea wote wa urais, lakini hawezi kuwasema vibaya kwa sababu yeye ni mwanamageuzi wa kweli ambaye amepania kuwaletea maendeleo Watanzania ambayo alisema kuwa hayajaonekana kwa miaka 44 sasa.

Source: Majira; Oktoba, 2005
 
mtikila anafaa kuanzishiwa thread yake "mjue mtikila"....ili tupate kuona ukweli wake, manake jamaa kagubikwa na kiza kinene, hatujui yupo upande gani wa senyenge
 
Tarehe Ya Kufungua Kesi Ya Mch Mtikila Siku Hiyo Siyo Kweli Na Kesi Haikufunguliwa Kwa Mwanahalisi Peke Yake Hata Tanzania Daima Nalo Limeshitakiwa Pia.chadema Ndio Wanaoongoza Kutoa Hela Ya Kumchafua Mwenyekiti Wa Dp Kwa Mwanahalisi Na Tanzania Daima.
 
mhhhhhhhh..............huyu nani kamtuma ? Huyu mtikila si alienda kuchukua 3 milioni yeye mwenyewe ama CHADEMA pia wanamchafua ?

Nilisema kuwa alilishitaki mwanahalisi siku hiyo na pia walifungua kesi wote wawili yaani Rostam na Mtikila wakisema kuwa wamechafuliwa majina the same day.

Pili nilisema pia kuwa huyu Mtikila amefungua kesi mahakama kuu kipindi hicho hicho dhidi ya Tanzania Daima.

Mtikilaaaaaaa? Benzi lake tunalimulika kwa tochi kali sana mpaka sasa tumeona alilinunua wapi ,sasa tunafuatilia nani alilipa fedha hizo ama alilipata bure.

Kazi inaendelea japo nikiwa huku nje ya Dunia ndani ya ardhi napata taabu kidogo.
 
Nimeona niwapatie chanzo cha hasira za Rostam Aziz kwa Mch Mtikila kama ujumbe huu mzito ulivyoandikwa na Mch Mtikila mwenyewe uliogawiwa kwa waandishi wa habari wote na wabunge wote.
KAMATI YA KUPAMBANA NA UPORAJI WA NCHI
PUBLIC INTEREST LITIGATION COMMITTEE
(PILCOM)

Kamati hii ilianza kujiunda tangu mwaka 2006 na wahanga wa ukombozi wa nchi yetu, kutoka katika Vyama vya siasa, taasisi za kidini, makampuni ya wanasheria mahiri, Taasisi huru za wananchi, na mshikamano mtakatifu wa wazalendo ndani ya Bunge letu, ambalo katika Ibara ya Nane ya Katiba ya Nchi yetu ndilo linaloitwa “Wananchi”. Ni mbinu yetu ya vita kutowaweka wazi wahanga wetu kwa sasa.

Kazi ya Kamati ni kuwafikisha mbele ya Sheria watu wote walioshiriki katika wizi wa matrilioni ya mapesa ya Nchi yetu katika Benki Kuu na Hazina ya Taifa letu, na kurejesha mapesa yote waliyoyaiba pamoja na riba na gharama, kutoka kila walikoyaweka nje na ndani ya nchi.

Tunawahakikishia wananchi kwamba kama isemavyo Katiba ya Jamhuri ya Muungano hakuna mwizi aliye juu ya Sheria awe rais mstaafu au aliye madarakani, waziri, kigogo wa CCM au gabacholi jeupe au jeusi, mradi ameshiriki katika :

* Wizi wa zaidi ya Shilingi bilioni 216 za Import Support Fund,
zilizokombwa kwa sehemu kubwa na marehemu Mehboob na mwanawe
Yusuf Manji, kwa ushirikiano na vigogo wa Hazina na Tanzania
Investment Bank,
* Wizi wa matrilioni ya mapesa ya EPA, DCP, OGL,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yanayoporwa kwa hila ya
Richmond/Dowans,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa ya yaliyoporwa kwa hila Meremeta na
Tangold,
* Wizi wa matrilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hujuma za I.P.T.L,
SONGAS, AGGREKO, NETGROUP SOLUTIONS,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hila ya TICTS Bandarini,
* Wizi wa mabilioni ya mapesa yaliyoporwa kwa hila ya ununuzi wa radar
na mtumba wa ndege ya rais,
* Uporaji wa shirika la TTCL kwa hila ya “uwekezaji” wa kampuni ya MSI,
Celtel na SIMU 2000,
* Uporaji wa Benki ya Taifa ya Biashara nyuma ya mgongo wa makaburu
wa ABSA,
* Uporaji wa madini yetu yote ya Tanzanite nyuma ya mgongo wa
makaburu wa AFGEM
* Uporaji wa migodi yetu ya dhahabu nyuma ya migongo ya akina James
Sinclair, Barrick Gold, Ashanti Gold na wengine,
* Uporaji wa majumba ya serikali ya matrilioni ya fedha kuwa mali za
Vigogo wa CCM na wezi wenzao,

Kwa vile Rais Kikwete anahusika katika uporaji huu ambao ulimnufaisha hata katika hila za mtandao wake za kumwingiza Ikulu, na kutokana na udhaifu wake mkubwa wa kujali zaidi maslahi ya kibinafsi na maswahiba kuliko hatima ya nchi na walalahoi, tulifahamu kabla ya tamko lake kwamba atamtumia Mkurugenzi wa Mashitaka (Director of Public Prosecution) kuwalinda wote waliohusika katika uporaji wa Nchi pamoja na mtuhumiwa mkuu Benjamin William Mkapa.

Ndiyo maana Kamati hii ilianza kazi yake mwaka 2006 kwa kufungua kesi ya Katiba Nambari 86/2006 ili kumwondolea Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka makubwa mno kupita matakwa ya Katiba ya Nchi, yaliyompa uwezo wa kuwalinda maharamia wote ambao Rais hatataka washitakiwe na kufungwa na kufilisiwa. Ndipo unaposimama ujasiri wa Kikwete wa kutamba kwamba atayalinda majizi ya mapesa yetu ya EPA, Richmond/Dowans yasifikishwe mahakamani! Tunataka haki ya wananchi ya kujiendeshea mashitaka wao wenyewe wasipokuwa na imani na DPP.

Swali zito ni Kwanini Mahakama Kuu haitoi hukumu ya kesi hii nyeti ya hatima ya Nchi yetu na uhuru wetu?

Bunge na serikali ni mali ya wananchi, mahakama pia ni mali ya wananchi. Ni mwiko kuingilia uhuru wa Mahakama, lakini ni lazima tupambanue kati ya uhuru na usaliti wa Mahakama. Waheshimiwa Majaji wetu wote ni raia wa nchi yetu, kwahiyo wanafungwa pamoja na raia wenzao wote na Ibara ya 27 ya Katiba ya Nchi kwamba wanao wajibu wa:

“kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi, na kwamba wanatakiwa kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Kwa uzalendo huu walioapa mbele za Mwenyezi Mungu na watu wote wa Nchi hii kuufanyia kazi, kesi nyeti namna hii ilitarajiwa kupewa kipaumbele inavyopasa, hata kama waheshimiwa Majaji wana milundikano mikubwa kiasi gani ya makesi mbele zao. Mungu waliyemwapia hataki kabisa kiburi na majigambo ya vigogo wa CCM kwamba eti mahakama ni yao, kwa sababu ni yake Yeye na haki ni utukufu wake Yeye.

Ndiyo maana baada ya kudhalilishwa majaji wake pamoja na wanahabari pale Mahakama Kuu, katika makufuru ya kesi ya mauaji ya kikatili ya Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, Mungu alishindwa kuchukuliana na uovu ule akamtwaa mtuhumiwa kuwa ishara! Unabii unaonya kwamba kama Kikwete atajifanya hakumwelewa Mungu, basi katika uporaji huu wa kutisha ataambiwa kwa herufi kubwa.

Kamati hii inangoja uamuzi wa Mahakama Kuu katika Kesi ya Katiba Nambari 86/2006, na tayari imewataka Gavana wa Benki Kuu na Mheshimiwa Spika wa Bunge letu waipatie taarifa muhimu za wizi wote uliofanywa na wahusika wote, ili Sheria ichukue mkondo wake dhidi yao wote.

Aidha Kamati inamtaka Rais Kikwete amwondoe maramoja Mustafa Mkullo katika Wizara ya Fedha, baada ya kudhihirika bayana kwamba ni mtu mwovu na wa hatari kwa maslahi ya Nchi kupita kiasi. Hata mwendawazimu hawezi kumkabidhi chui mwenye njaa amtunzie mbuzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo K. Peter Pinda aliweka nadhiri kwa Mungu, kwamba kama atajihusisha katika ufisadi Mwenyezi Mungu amnyang’anye roho aitupe hukumuni. Hivyo ni lazima ahakikishe kwamba wote waliohusika na wizi wa mapesa ya EPA/DCP/OGL, Richmond/Dowans n.k. wanashitakiwa maramoja na mapesa yanarejeshwa pamoja na riba. Mungu hachezewi!

Ikiwa watuhumiwa wamefanya uporaji kama chama yaani CCM, basi lazima genge lote litokomezwe. La sivyo damu itamwagika vibaya sana katika nchi hii kwa uporaji huu, kama Bunge halitaachiwa kutekeleza kazi ya wananchi ipasavyo, na Mahakama kufanya kazi yake!

HATIMA YA MWAJEMI SAKARIR (ROSTAM) AZIZ

Kiini cha ufisadi wa kutisha na uporaji wa Nchi yetu, unaofanywa kama vile Watanganyika wote ni mataahira, ni kutoweka kwa uraia wa kweli wa kuipenda nchi yetu na kuwa na uchungu nayo wa kiwango cha uhanga kwa ajili yake. Kwa sababu ya “utaahira” wetu nchi yetu imekamatwa na mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliuofanyika katika Benki Kuu na Hazina ya Nchi yetu, ambaye ni Mwajemi yaani raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya “mataahira” kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la “Rostam”. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ng’ombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.

Nilipoanza kuzungumzia uraia wa “Rostam” Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo, ingawa alisahau kwamba Premji wa Kigoma alizaliwa hapa lakini hakuwa raia kwa sababu wazazi wake hawakuwa wameukana uraia wa kwao, wala yeye Premji hakuwa ameomba uraia kwa mujibu wa Sheria, hata kama aliweza kujipatia Passport ya nchi hii kwa njia za ufisadi kama alivyofanya yeye. “Rostam” amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli.

Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya Nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu.

Kwa ufupi Sakarir alipofika nchini mwetu baada ya masomo yake Uingereza, aliunganishwa na viongozi watatu wa CCM waliokuwa marafiki sana ambao ni pamoja na Rais Kikwete. Rostam alipata nguvu ya kisiasa kwa kutumia mapesa mengi ya mfuko maalum wa nchi yao wa “Iranians in Diaspora”, aliyoyapata kama raia mwaminifu wa Iran, aliye na shughuli zenye maslahi kwa nchi yao katika nchi ya nje. Nguvu hii ndiyo iliyomtia Benjamin Mkapa mkononi mwake na kuwa msingi wa uhuni na jeuri yote aliyonayo leo.

Mafisadi walionufaika na mtaji huo wa Sakarir Aziz ndio waliofanya uhaini wa kumpa Ubunge wa Igunga alipofariki hayati Charles Kabeho. Wazee wa Kiajemi waliolowea hapa, Hussein Heidari na Hassan nduguye ndio waliompokea kijana Sakarir Aziz kule Igunga, kwa sababu wanao uhusiano na mkewe Aziz yaani mama yake Sakarir au Rostam.

Hawa wazee ndio waliomnadi huyu Mwajemi kwa wazee wa Igunga katika kuiba Ubunge wa Nchi ya watu ambao anawachukulia kuwa “mataahira”. Sakarir Aziz anao nduguze wa kiume wawili yaani Jahangir Aziz ambaye alipigana kizalendo kabisa ile vita ya nchi yao dhidi ya Iraq, na wa pili ni Akram Aziz.

Kamati yetu imejitolea kuwasaidia wananchi wa Igunga wanaotaka kufungua kesi dhidi ya Sakarir Aziz na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kwa kuwanyima uwakilishi Bungeni tangu Mbunge wao hayati Charles Kabeho alipofariki. Kwani Mwajemi wa Jamhuri ya Kiislamu, “Rostam” Aziz hawajali kabisa wananchi wa Jimbo lile, hata katika maafa kama ya kukosa kabisa usafiri baada ya madaraja ya mto Mbutu kuzolewa na mafuriko, au machafuko yaliyotokana na masuala ya ushirikina.

“Rostam” Aziz anashirikiana katika kupora Nchi yetu na gabacholi mwingine aitwaye Yusuf Manji, ambaye pia si raia wa nchi hii na akibisha ushahidi utatolewa. Bilashaka Wabunge safari hii watataka kujua ni nani hasa waliotoa Passports za Tanzania kwa “Rostam” Aziz, Jahangir Aziz na Akram Aziz na kwa misingi gani.

Wezi hawa wanaipora nchi hii bila huruma, na ndio wanaowaambia watawala wa CCM cha kufanya ili wakombe mapesa yetu B.O.T na Hazina, na kutumia matrilioni yetu kuwatia viongozi wetu ndani ya mifuko ya makoti yao, ambamo wanalishwa masazo yao na kuchomoza vichwa kuchungulia nje kama vindege kuwasanifu wananchi, na kurudi mifukoni mwao wakidhani wanakula kumbe wanaliwa wao na Nchi yao! Hatutaki Rais wetu wala Wabunge wetu wawe vindege ndani ya mifuko ya makoti ya “Rostam” Aziz na Yusuf Manji!

“Rostam” na yusuf Manji wapo Dodoma na shehena ya mapesa ya EPA, kwa kazi ya kuwanunua wabunge wanaowadharau kwamba eti ni mataahira, wawe karatasi ya msalani (toilet paper) ya kuwasafisha uchafu wao halafu na yenyewe itokomee pamoja na uchafu, kwani haiwi safi tena baada ya kutumiwa!

Tunaitaka Serikali iwakamate hawa wahalifu hatari wa Taifa letu huko Dodoma na kuwapokonya makaratasi yao yote ya kusafiria na kuwaleta kizimbani maramoja kwa uharamia wote walioifanyia Nchi yetu.

Saa ya ukombozi ni sasa!

Mchungaji C. Mtikila
MWENYEKITI WA KAMATI
26/6/2008
 
Mtikila ni kichaa.Nimetoka na mambo mengi ila haya yameniacha hoi

1.wabunge wanaowadharau kwamba eti ni mataahira
2.utaahira

Nini maana ya maneno haya?
 
Kweli anamtayarisha jamaa fulani pale wizara ya madini achukue kiti chake cha Igunga, kama vile anaitwa Kafumu
Ubaya watu wengi hawamjui na wanaodai kumjua wanasema ni kibaraka wake

Acha kupre-empt ujinga huo! hakuna anayeandaliwa.kama rostam hatagombea thats all, wapo watu potential Igunga na nia ya dhati watapenda kugombea.sio lazima kafumu.
 
Ujumbe mzuri. Naona umeingia kwa kasi sana humu kumtetea Mtikila. Kama unajua waliomtuma waambia nawaambie wamemfanya mwenzao ang'ate mkono uliokuwa ukimlisha lakini pia amejianika vile alivyo! mtupu kabisa. Mpe shukrani kwa kujifunga mabomu na kujilipua. Amesaidia kumshughulikia FISADI Rostam Aziz ila na yeye amekufa. Mwenzie bado anatapa tapa ila na yeye lazima amaliziwe. Mtikila is not a pastor, he is an impositor. Hoja zake kwenye huo waraka zina maana lakini yeye mwenyewe haya maana kabisa. Na hoja zake za ufisadi zina maana, lakini hoja zake za ubaguzi hazina maana kabisa! Tell him, shame on him!

Asha
 
IFUATAYO NI TAARIFA YA MCH MTIKILA KWA WAANDISHI WA HABARI KATAIKA MKUTANO WAKE TRAVERTINE HOTEL JANA 14th JULY 2008

+ KAMATI YA WAKRISTO YA KUITETEA IMANI+
(Wafilipi 1: 27-30, Yuda 1: 3-4, 1Petro 3: 14-16)
P.O. Box 3885 Simu 0755 885095 au 0713 430516

“ROSTAM” AMEHARIBIKIWA?

Kabla ya kuwaelezeni uhuni wake kuhusu mkopo wangu wa shilingi milioni tatu, nafurahi kwamba taarifa ya Sakarir Aziz au Rostam aliyoitoa jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, imethibitisha jinsi alivyoharibikiwa akili kwa kufishwa malengo yake machafu, ya kulitumia Kanisa nchini kama tissue ya kumsafisha wizi na ufisadi wake.

Makanisa anayodai kuyachangia yalipokea sadaka yake kabla ya kudhihirishwa na Mungu kuwa yeye ndiye fisadi mkuu wa uporaji wa Nchi, na Makanisa ndiyo yaliyomlilia Mungu kwamba awaweke wazi mafisadi wote wanaomaliza nchi yetu na kusababisha mateso makali ya walalahoi yanaowachunga. Tena Makanisa hayo hayakuthubutu kumpa madhabahu ainajisi kama alivyokufuru KKKT Kinondoni, watumishi wa Mungu wakawajibika ipasavyo!

Sadaka ya mtu yeyote inakubalika, mradi iwe kwa utukufu wa Mungu, na siyo kama ile dhahabu na fedha iliyotolewa na mfalme Balaki kwa nabii Balaam ili alaani watu wa Mungu, kama Sakarir alivyotaka Kanisa limsaidie kulaani wazalendo wanaopambana na mafisadi waliomaliza Nchi yetu!

Rostam amepagawa kwangu mimi kwa sababu amekuwa akifanikiwa kuziba midomo ya watu wote kwa rushwa anapoipora nchi, na kuabudiwa tangu na marais wa nchi mpaka watu wa chini katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu, kwa nguvu ya ufisadi wake inayoua uzalendo wao kwa mapesa yetu wenyewe aliyotuibia. Lakini Rostam alikuwemo katika njama ya ile rushwa ya shilingi 450 milioni ya Yusuf Manji niliyoikataa, na hata shilingi 150 milioni za karibuni za kunitaka nifute kesi ya kunikashifu Bwana Manji, nilizokataa pia kwa sababu ni dharau!

Kadhalika leo nafurahia ushuhuda wa Rostam mwenyewe kwamba ingawa alinipa mkopo wa shilingi milioni tatu, bado napambana na ufisadi wake, yaani sinunuliki, na siwezi kamwe kuchanganya masuala (issues) na uhusiano wa kibinafsi, kwa sababu kufanya hivyo ni ufisadi.

Na kama Mungu alivyomtumia Farao kugharamia maandalizi ya Musa ili hatimaye ampokonye watumwa wake, mkopo alionipa Rostam ulitusaidia sana hata katika maandalizi mazito ya kuwashitaki walioifilisi nchi yetu, yaani yeye Sakarir Aziz na wenzake wote, na kurejesha mapesa yetu yote kokote walikoyaficha. PILCOM inahitaji uzalendo na mshikamano wa Watanganyika wote.

Mkopo wangu wa shilingi milioni tatu:

Vyombo vya habari vilipata kutunukuu mimi na yeye Sakarir kwa usahihi kwamba ni marafiki, na mimi nikasisitiza kwamba siwezi kuisaliti nchi yangu kwa ajili ya urafiki na mtu.

Ndiyo maana nilipopungukiwa hizo pesa nilijua kwamba ningezipata kwa Sakarir, ambaye angefurahi kupata mwanya wa kunitumia kwa kiasi chochote cha pesa kama ningekuwa msaliti, mradi nijilinde. Ndiyo maana kwa matarajio ya kupata fedha yangu baadaye za kumlipa nilimwendea anikopeshe, siyo mchango au sadaka yenye masharti ya kiroho kama alivyogushi stakabadhi, ili aitumie kwa kisasi cha kupoza majeraha ya kisaikolojia aliyopata kwa kulinajisi Kanisa la Mungu la KKKT Kinondoni!

Mimi ndiye niliyemsisitizia kuwa anisainishe mkopo huo kwa uhakika kwamba nitamrudishia. Na mkopo ni mkataba kama biashara, hivyo hauna dhambi, na tunautafuta kwa mtu yeyote yule mradi masharti yasiwe mabaya. Lakini stakabadhi aliyoitumia katika vyombo vya habari siyo yenyewe, imegushiwa. Stakabadhi niliyosaini mimi ilikuwa na Payment Vaucher Number lakini hii haina kwa maana kwamba siyo valid kabisa!

Tena karatasi hii inadanganya kwamba malipo ni sadaka kwa Kanisa bila hata kusema ni Kanisa gani, kinyume cha ukweli kwamba nilikopa mimi binafsi! Sote tunajua kuwa Payment Vaucher ni source document
Ambayo uhalali wake ni kuwa na:
• Jina kamili la anayelipwa
• Maelezo sahihi ya sababu ya malipo
• Tarehe ya malipo
• Saini za mlipaji na mlipwaji
• VAUCHER NUMBER
Baada ya malipo hufanyika posting, yaani kuingiza PVaucher katika Cash book, VAUCHER NUMBER yake ikiwa ndiyo reference rasmi kutokana na mlolongo wa malipo mbali mbali tofauti unaoendelea katika cash book. Baada ya hapo malipo yanaingizwa kwenye Ledger kwa reference ya Vaucher numbers zake, hivyo kwamba mhasibu akiona hitilafu anaitisha apewe Vaucher namba husika aipitie.

Mhasibu hawezi kugonga muhuri (ku-certify) Payment Vaucher ambayo haina namba kwa sababu hayo ni malipo hewa, kwani haimo katika cash book wala katika Ledger! Na P.V. hii ya fisadi huyu imekuwa certified ingawa haina namba, yaani ni takataka tu au forgery, uhuni! Ameitengeneza kwa ajili ya kuzidi kulinajisi Kanisa la Mungu, kwa kung’ang’aniza kwamba makufuru aliyoyafanya KKKT Kinondoni yalikuwa halali, kwa kigezo cha karatasi hii, ili ajihalalishie pia kunivurumishia matusi kama alivyofanya jana.

Sakarir Aziz hakuzungumzia uraia wake, lakini kama alivyojitabiria mwenyewe hilo litammaliza mahakamani. Kuja Waajemi hapa mwaka 1852 si hoja, kwani David Livingstone pia alikuja hapa zamani lakini wajukuu zake ni raia wa kwao. Suala ni kwamba wazazi wake hawajawahi kuishi hapa, wako kwao na biashara yao ya nyama na ng’ombe, na Sakarir walimzaa huko huko Iran, akasoma kwao na kumalizia masomo ya juu Uingereza wanakoishi ndugu zao.

Premji alizaliwa hapa, lakini kwavile wazazi wake walikiri kutoukana uraia wa kwao na uraia wa mtoto unasimama katika uraia wa wazazi, na kwa vile yeye mwenyewe Premji hakuwa ameomba rasmi uraia na kutangazwa magazetini, Mahakama Kuu ilimvua Ubunge kwa vile si raia. Lakini Premji ni afadhali kuliko Sakarir Aziz ambaye wazazi wake hawajawahi kuishi hapa, wala yeye mwenyewe hajawahi kuomba uraia wa Tanzania wala kuukana uraia wa kwao, badala yake kwa ufisadi wake alijaribu kutungisha sheria ya kumruhusu kuwa na uraia wa Tanzania na kwao Iran, kwa sababu akithubutu kuchezea utaifa wa Iran anaweza kukatwa kichwa chake, hivyo anachezea utaifa wetu sisi anaotudharau kuwa “mataahira”. Amepataje passport ya nchi yetu, na amejipatiaje Ubunge wa Igunga, atajieleza Mahakamani!

Rostam ameropoka kwamba apelekwe Mahakamani kwa kuikomba nchi yetu kwa hila ya Richmond/Dowans, mapesa ya EPA kwa kampuni feki ya Kagoda Agriculture Limited, kuifilisi Bandari kwa kampuni ya TICTS na uharamia mwingine wote alioifanyia nchi yetu, hakika huko ndiko atakakoishia tu!

Kifo cha Daudi Balali si dawa, na wananchi wana haki ya kujua Rostam alikwenda kufanya nini Marekani katika kifo hicho? Wala Kikwete hana uwezo wa kumlinda, na hata yeye amekwishaona ndiyo maana sasa anaanza kupagawa. Hajakanusha tahadhari za vyombo vya habari kwamba amejizatiti kutoroka. Lakini hata akikikimbilia huko alikolimbikiza matrilioni ya fedha aliyoikomba nchi yetu atakamatwa, hata akikimbilia kuzimu atarudishwa hapa.

Aidha kwavile hata watoto wadogo mitaani wanalia naye nchi nzima kwamba ndiye fisadi anayeimaliza nchi yao, basi hata yeye atangulie mahakamani kama alivyoshitaki MwanaHALISI, kiyama kitamfuata tu. Saa ya ukombozi ni sasa!

Matusi kwamba Mtikila hana heshima ya kustahili kujibiwa na yeye (ingawa ndicho alichokuwa anafanya) ni ile dharau yake iliyokithiri kwa watu wa nchi hii kwamba ni taka tu kwake, hawana akili kabisa, eti hata Rais wetu ni yeye aliyemwingiza Ikulu, Lowasa ndiye aliyempa uwaziri mkuu, Spika wa Bunge alimweka yeye, viongozi wa nchi na hata majaji anawapa ulaji yeye n.k ndiyo majigambo ya huyu mwizi na fisadi, hasa akilewa!

Sakarir Aziz amepiga vijembe Wakristo aliodai kuwa wanachangia misikiti na shughuli zingine za Waislamu. Lakini kama wapo basi wasingekubalika kama wangethubutu kutoa masharti ya kuitumia misikiti hiyo kama toilet paper zao za kuwasafisha ufisadi kama alivyofanya yeye.

Isitoshe, amezungumzia biashara za madawa ya kulevya, wakati yeye ni mshirika wa Yusuf Manji na Mohamed Dewji, ambao wote ni waovu wa hatari. Wala Rostam si mtu wa kunyooshea kidole mafuska wanaozini na vitoto, kwa sababu yeye mwenyewe mkewe ni mgonjwa mahututi kwa siku nyingi sasa, na badala ya kumuuguza yeye alijiletea kisichana kama hivyo kutoka kwao! Rostam ameharibikiwa.

Mchungaji C. Mtikila
KAIMU MWENYEKITI
14/7/2008
 
Kweli anamtayarisha jamaa fulani pale wizara ya madini achukue kiti chake cha Igunga, kama vile anaitwa Kafumu
Ubaya watu wengi hawamjui na wanaodai kumjua wanasema ni kibaraka wake
Kwa taarifa yako, na kuanzia leo ukae ukijua, ccm hawako tyr kusimamisha mgombea ambaye kabla ya kugombea ni mtumishi wa serikali(ie afisa mwandamizi serikalin) au mfanyabiashara.watatafuta mtu yeyote asiye na sifa hizo mbili, sababu ni kuepuka kashfa za kupika! serikalin kuna mambo mengi ya kutuhumiana the same hata kwa wafanya biashara.
 
Nilipoanza kuzungumzia uraia wa "Rostam" Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo, ingawa alisahau kwamba Premji wa Kigoma alizaliwa hapa lakini hakuwa raia kwa sababu wazazi wake hawakuwa wameukana uraia wa kwao, wala yeye Premji hakuwa ameomba uraia kwa mujibu wa Sheria, hata kama aliweza kujipatia Passport ya nchi hii kwa njia za ufisadi kama alivyofanya yeye. "Rostam" amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli.

Karibu Mtikila kwenye forum hii, ila jua kuwa kama umekula za kifisadi na wewe waweza kuwa fisadi pia hata ukawa fisadi wa kimaadili.

Rudisha na Benzi pia .
 
Kweli anamtayarisha jamaa fulani pale wizara ya madini achukue kiti chake cha Igunga, kama vile anaitwa Kafumu
Ubaya watu wengi hawamjui na wanaodai kumjua wanasema ni kibaraka wake

mfano mzuri ni uchaguzi mdogo wa jimbo latunduru na simanjiro, tafuta profile ya Mtutura na Ole Nangoro utaelewa ninachokisema.
 
Mtikila na siasa zake za kibaguzi na kusingizia wengine sio raia ndio anatisha kuliko hao mafisadi,assume angekuwa raisi akikuchukia tuu basi wewe sio raia...haya mambo ya kumpakazia RO sio raia wakati wapo TZ tangu 1800 huko tabora inanisikitisha sana...waatu kama kina Zitto wa mipakani under Mtikila leo mngekuwa mko Burundi
 
IFUATAYO NI TAARIFA YA MCH MTIKILA KWA WAANDISHI WA HABARI KATAIKA MKUTANO WAKE TRAVERTINE HOTEL JANA 14th JULY 2008

+ KAMATI YA WAKRISTO YA KUITETEA IMANI+
(Wafilipi 1: 27-30, Yuda 1: 3-4, 1Petro 3: 14-16)
P.O. Box 3885 Simu 0755 885095 au 0713 430516

“ROSTAM” AMEHARIBIKIWA?

Kabla ya kuwaelezeni uhuni wake kuhusu mkopo wangu wa shilingi milioni tatu, nafurahi kwamba taarifa ya Sakarir Aziz au Rostam aliyoitoa jana katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, imethibitisha jinsi alivyoharibikiwa akili kwa kufishwa malengo yake machafu, ya kulitumia Kanisa nchini kama tissue ya kumsafisha wizi na ufisadi wake.

Makanisa anayodai kuyachangia yalipokea sadaka yake kabla ya kudhihirishwa na Mungu kuwa yeye ndiye fisadi mkuu wa uporaji wa Nchi, na Makanisa ndiyo yaliyomlilia Mungu kwamba awaweke wazi mafisadi wote wanaomaliza nchi yetu na kusababisha mateso makali ya walalahoi yanaowachunga. Tena Makanisa hayo hayakuthubutu kumpa madhabahu ainajisi kama alivyokufuru KKKT Kinondoni, watumishi wa Mungu wakawajibika ipasavyo!

Sadaka ya mtu yeyote inakubalika, mradi iwe kwa utukufu wa Mungu, na siyo kama ile dhahabu na fedha iliyotolewa na mfalme Balaki kwa nabii Balaam ili alaani watu wa Mungu, kama Sakarir alivyotaka Kanisa limsaidie kulaani wazalendo wanaopambana na mafisadi waliomaliza Nchi yetu!

Rostam amepagawa kwangu mimi kwa sababu amekuwa akifanikiwa kuziba midomo ya watu wote kwa rushwa anapoipora nchi, na kuabudiwa tangu na marais wa nchi mpaka watu wa chini katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu, kwa nguvu ya ufisadi wake inayoua uzalendo wao kwa mapesa yetu wenyewe aliyotuibia. Lakini Rostam alikuwemo katika njama ya ile rushwa ya shilingi 450 milioni ya Yusuf Manji niliyoikataa, na hata shilingi 150 milioni za karibuni za kunitaka nifute kesi ya kunikashifu Bwana Manji, nilizokataa pia kwa sababu ni dharau!

Kadhalika leo nafurahia ushuhuda wa Rostam mwenyewe kwamba ingawa alinipa mkopo wa shilingi milioni tatu, bado napambana na ufisadi wake, yaani sinunuliki, na siwezi kamwe kuchanganya masuala (issues) na uhusiano wa kibinafsi, kwa sababu kufanya hivyo ni ufisadi.

Na kama Mungu alivyomtumia Farao kugharamia maandalizi ya Musa ili hatimaye ampokonye watumwa wake, mkopo alionipa Rostam ulitusaidia sana hata katika maandalizi mazito ya kuwashitaki walioifilisi nchi yetu, yaani yeye Sakarir Aziz na wenzake wote, na kurejesha mapesa yetu yote kokote walikoyaficha. PILCOM inahitaji uzalendo na mshikamano wa Watanganyika wote.

Mkopo wangu wa shilingi milioni tatu:

Vyombo vya habari vilipata kutunukuu mimi na yeye Sakarir kwa usahihi kwamba ni marafiki, na mimi nikasisitiza kwamba siwezi kuisaliti nchi yangu kwa ajili ya urafiki na mtu.

Ndiyo maana nilipopungukiwa hizo pesa nilijua kwamba ningezipata kwa Sakarir, ambaye angefurahi kupata mwanya wa kunitumia kwa kiasi chochote cha pesa kama ningekuwa msaliti, mradi nijilinde. Ndiyo maana kwa matarajio ya kupata fedha yangu baadaye za kumlipa nilimwendea anikopeshe, siyo mchango au sadaka yenye masharti ya kiroho kama alivyogushi stakabadhi, ili aitumie kwa kisasi cha kupoza majeraha ya kisaikolojia aliyopata kwa kulinajisi Kanisa la Mungu la KKKT Kinondoni!

Mimi ndiye niliyemsisitizia kuwa anisainishe mkopo huo kwa uhakika kwamba nitamrudishia. Na mkopo ni mkataba kama biashara, hivyo hauna dhambi, na tunautafuta kwa mtu yeyote yule mradi masharti yasiwe mabaya. Lakini stakabadhi aliyoitumia katika vyombo vya habari siyo yenyewe, imegushiwa. Stakabadhi niliyosaini mimi ilikuwa na Payment Vaucher Number lakini hii haina kwa maana kwamba siyo valid kabisa!

Tena karatasi hii inadanganya kwamba malipo ni sadaka kwa Kanisa bila hata kusema ni Kanisa gani, kinyume cha ukweli kwamba nilikopa mimi binafsi! Sote tunajua kuwa Payment Vaucher ni source document
Ambayo uhalali wake ni kuwa na:
• Jina kamili la anayelipwa
• Maelezo sahihi ya sababu ya malipo
• Tarehe ya malipo
• Saini za mlipaji na mlipwaji
• VAUCHER NUMBER
Baada ya malipo hufanyika posting, yaani kuingiza PVaucher katika Cash book, VAUCHER NUMBER yake ikiwa ndiyo reference rasmi kutokana na mlolongo wa malipo mbali mbali tofauti unaoendelea katika cash book. Baada ya hapo malipo yanaingizwa kwenye Ledger kwa reference ya Vaucher numbers zake, hivyo kwamba mhasibu akiona hitilafu anaitisha apewe Vaucher namba husika aipitie.

Mhasibu hawezi kugonga muhuri (ku-certify) Payment Vaucher ambayo haina namba kwa sababu hayo ni malipo hewa, kwani haimo katika cash book wala katika Ledger! Na P.V. hii ya fisadi huyu imekuwa certified ingawa haina namba, yaani ni takataka tu au forgery, uhuni! Ameitengeneza kwa ajili ya kuzidi kulinajisi Kanisa la Mungu, kwa kung’ang’aniza kwamba makufuru aliyoyafanya KKKT Kinondoni yalikuwa halali, kwa kigezo cha karatasi hii, ili ajihalalishie pia kunivurumishia matusi kama alivyofanya jana.

Sakarir Aziz hakuzungumzia uraia wake, lakini kama alivyojitabiria mwenyewe hilo litammaliza mahakamani. Kuja Waajemi hapa mwaka 1852 si hoja, kwani David Livingstone pia alikuja hapa zamani lakini wajukuu zake ni raia wa kwao. Suala ni kwamba wazazi wake hawajawahi kuishi hapa, wako kwao na biashara yao ya nyama na ng’ombe, na Sakarir walimzaa huko huko Iran, akasoma kwao na kumalizia masomo ya juu Uingereza wanakoishi ndugu zao.

Premji alizaliwa hapa, lakini kwavile wazazi wake walikiri kutoukana uraia wa kwao na uraia wa mtoto unasimama katika uraia wa wazazi, na kwa vile yeye mwenyewe Premji hakuwa ameomba rasmi uraia na kutangazwa magazetini, Mahakama Kuu ilimvua Ubunge kwa vile si raia. Lakini Premji ni afadhali kuliko Sakarir Aziz ambaye wazazi wake hawajawahi kuishi hapa, wala yeye mwenyewe hajawahi kuomba uraia wa Tanzania wala kuukana uraia wa kwao, badala yake kwa ufisadi wake alijaribu kutungisha sheria ya kumruhusu kuwa na uraia wa Tanzania na kwao Iran, kwa sababu akithubutu kuchezea utaifa wa Iran anaweza kukatwa kichwa chake, hivyo anachezea utaifa wetu sisi anaotudharau kuwa “mataahira”. Amepataje passport ya nchi yetu, na amejipatiaje Ubunge wa Igunga, atajieleza Mahakamani!

Rostam ameropoka kwamba apelekwe Mahakamani kwa kuikomba nchi yetu kwa hila ya Richmond/Dowans, mapesa ya EPA kwa kampuni feki ya Kagoda Agriculture Limited, kuifilisi Bandari kwa kampuni ya TICTS na uharamia mwingine wote alioifanyia nchi yetu, hakika huko ndiko atakakoishia tu!

Kifo cha Daudi Balali si dawa, na wananchi wana haki ya kujua Rostam alikwenda kufanya nini Marekani katika kifo hicho? Wala Kikwete hana uwezo wa kumlinda, na hata yeye amekwishaona ndiyo maana sasa anaanza kupagawa. Hajakanusha tahadhari za vyombo vya habari kwamba amejizatiti kutoroka. Lakini hata akikikimbilia huko alikolimbikiza matrilioni ya fedha aliyoikomba nchi yetu atakamatwa, hata akikimbilia kuzimu atarudishwa hapa.

Aidha kwavile hata watoto wadogo mitaani wanalia naye nchi nzima kwamba ndiye fisadi anayeimaliza nchi yao, basi hata yeye atangulie mahakamani kama alivyoshitaki MwanaHALISI, kiyama kitamfuata tu. Saa ya ukombozi ni sasa!

Matusi kwamba Mtikila hana heshima ya kustahili kujibiwa na yeye (ingawa ndicho alichokuwa anafanya) ni ile dharau yake iliyokithiri kwa watu wa nchi hii kwamba ni taka tu kwake, hawana akili kabisa, eti hata Rais wetu ni yeye aliyemwingiza Ikulu, Lowasa ndiye aliyempa uwaziri mkuu, Spika wa Bunge alimweka yeye, viongozi wa nchi na hata majaji anawapa ulaji yeye n.k ndiyo majigambo ya huyu mwizi na fisadi, hasa akilewa!

Sakarir Aziz amepiga vijembe Wakristo aliodai kuwa wanachangia misikiti na shughuli zingine za Waislamu. Lakini kama wapo basi wasingekubalika kama wangethubutu kutoa masharti ya kuitumia misikiti hiyo kama toilet paper zao za kuwasafisha ufisadi kama alivyofanya yeye.

Isitoshe, amezungumzia biashara za madawa ya kulevya, wakati yeye ni mshirika wa Yusuf Manji na Mohamed Dewji, ambao wote ni waovu wa hatari. Wala Rostam si mtu wa kunyooshea kidole mafuska wanaozini na vitoto, kwa sababu yeye mwenyewe mkewe ni mgonjwa mahututi kwa siku nyingi sasa, na badala ya kumuuguza yeye alijiletea kisichana kama hivyo kutoka kwao! Rostam ameharibikiwa.

Mchungaji C. Mtikila
KAIMU MWENYEKITI
14/7/2008

Bwana Mtikila, pamoja na uwendawazimu wako wallah nakupongeza kwa maneno yako yakiwendawazimu lakini yenye kumkoma nyani! Hii jino kwa jino nimeipenda. Na ukianza kurusha mawe kwa bwana huyu akipita barabarani nitakuunga mkono.

Wakati wa ukombozi ni wakati wa machizi kama wewe kuwa mstari wa mbele. Endelea kumfisadi huyu jamaa mpaka apande mwenyewe mahakamani kwa hasira

Asha
 
Back
Top Bottom