Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Bi mdogo wameniambia tarehe 31, na wamenihakikishia hivyo.. lakini kwenye maelezo yao kuna * wakiangaliza kuhusu Butiama.. so sijui kuna uhusiano gani kati ya maswali hayo na kitakachotokea Butiama. [/SIZE
Btw, kuanzia kesho jumatano, nzi yule mwenye kupanda kuta za Ikulu, na Wizara atakuwa Butiama akipeperuka kunusa nusa... kwa hiyo inawezekana J'tano tukawa na "live" reporting toka Butiama.. kwenye both Bongoradio na KLH News..



Mwanakijiji,
Mbona unatuangusha??? tafadhali tuhabarishe, tarehe uliyosema imepita hatuoni lolote, aziz yupo anakata mitaa as usual! acha kukwepa.
 
Mwanakijiji,
Mbona unatuangusha??? tafadhali tuhabarishe, tarehe uliyosema imepita hatuoni lolote, aziz yupo anakata mitaa as usual! acha kukwepa.

Sources zote za Mwanakijiji zinashikiliwa na security detail ya Kikwete mwenyewe.... kwi kwi kwi kwi!

Unategemea Kikwete ataruhusu rafiki yake mkuu ROstam Azizi apate aibu ambayo anaelekea kupata kwenye hii thread. In the next few days, watanzania wataanza kujua huyu ROstam:

1. Alikozaliwa (maana hakuna uthibitisho kuwa alizaliwa TZ)
2. ALikosoma shule ya msingi
3. Alikopata pesa za kuanzia na kuendeleza biashara
4. Mwaka aliosoma chuoni na chuo alichosoma
5. Mwaka aliopata passport ya Tanzania (au kupata uraia wa TZ)
6. Vigezo vilivyotumika kumpatia passport ya Tanzania!

Get your lazy boy ready for the movie of the month!
 
Mwanakijiji,
Mbona unatuangusha??? tafadhali tuhabarishe, tarehe uliyosema imepita hatuoni lolote, aziz yupo anakata mitaa as usual! acha kukwepa.


Huyo aliyenipa habari kanitumia ujumbe jana na unasema kuwa alishindwa kufanya hivyo kwa wakati huu. Binafsi sina habari yoyote ndio maana nauliza.. kama kuna mwingine anayejua habari kuhusu Rostam anaweza kutupatia tu.. hasa kuhusu wazazi wake, wako wapi na walikuwa wazaliwa wa wapi..
 
Huyo aliyenipa habari kanitumia ujumbe jana na unasema kuwa alishindwa kufanya hivyo kwa wakati huu. Binafsi sina habari yoyote ndio maana nauliza.. kama kuna mwingine anayejua habari kuhusu Rostam anaweza kutupatia tu.. hasa kuhusu wazazi wake, wako wapi na walikuwa wazaliwa wa wapi..
Mkuu Mwanakiji,inawezekana kabisa Rostama akawa hana uraia wa Tanzania kutokana na sheria ipi inatumika,ila kwa sheria ya mwaka 1995 ya uraia Rostgam ni Raia wa Tanzania..ila kabla ya sheriua hiyo asingeweza kuwa Raia.
 
Mkuu Mwanakiji,inawezekana kabisa Rostama akawa hana uraia wa Tanzania kutokana na sheria ipi inatumika,ila kwa sheria ya mwaka 1995 ya uraia Rostgam ni Raia wa Tanzania..ila kabla ya sheriua hiyo asingeweza kuwa Raia.

Hauna uthibitisho na hili si ndio?
 
Rostam na wazaz wake walipata kuishi bukene ktk kijiji kimoja kinaitwa mwamala, b'dae waliondoka tanzania. Upo uhakika rostam hakuwah kusomea tanzania. Ukiweza nipe contact yako nikuunganishe kwa mtu mmoja anaweza kukupa reliable details za mtu huyu.
 
Rostam na wazaz wake walipata kuishi bukene ktk kijiji kimoja kinaitwa mwamala, b'dae waliondoka tanzania. Upo uhakika rostam hakuwah kusomea tanzania. Ukiweza nipe contact yako nikuunganishe kwa mtu mmoja anaweza kukupa reliable details za mtu huyu.

tatizo siyo wazazi waliwahi kuishi wapi, wazazi wake walizaliwa wapi?
 
Rostam na wazaz wake walipata kuishi bukene ktk kijiji kimoja kinaitwa mwamala, b'dae waliondoka tanzania. Upo uhakika rostam hakuwah kusomea tanzania. Ukiweza nipe contact yako nikuunganishe kwa mtu mmoja anaweza kukupa reliable details za mtu huyu.

KIla kitu kinachomzunguka huyu Rostam kuanzia alikozaliwa hadi alikopatia elimu yake, pesa zake, passport (uraia wa Tanzania), na kadhalika vimejaa utata mtupu.

Yeye mwenyewe ameshindwa hata kuweka kwenye report yake ya bunge amesoma wapi na lini. Nashawishika kusema kuwa Rostam Azizi sio raia halali wa Tanzania!
 
Ama kweli tz kuna mamambo kama si mambo!!!!!!!!
Hivi hakuna hata fisadi moja lenye asili ya kiafrika la kuziba nafasi ya huyu jamaa huko igunga?na huko igunga ni wazushi sana,ilikuwaje huyu mtu akapata hiyo nafsi,hivi hapa tz hamna mtu wa kudeal na hawa watu?aaaaaaaaaaaaaaaa,ishakuwa nomiiiiiiiiiii.

Watz nasema mwisho tena mwisho na mwishoooooooooo mtu asiye na asili ya kiafrika kushika uongozi tz wa chama au serikali na hapa zanzibar pia mnieleweeeeeee

Tena tuanzishe kampeni mara moja au siyo na hiki kipengele kiingie ktk katiba kwamba KIONGOZI YEYOTE WA CHAMA AU SERIKALI LAZIMA AWE MTU MWEUSI NA MWENYE ASILI YA KIAFRIKA NA MZALIWA WA TZ TU.

Tutahubiri makanisani,misikitini na vilabuni,hadi kielewkeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Anyway dawa yao iko kwa kitchen.
 
Sitta amzuia Rostam

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, jana alimzuia Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni, kwa maelezo kwamba mbunge huyo alikuwa hajatimiza masharti ya kanuni za Bunge.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jioni kwa njia ya simu, Sitta alisema hadi kufikia jana saa 11:01, hakuwa amepokea kwa maandishi maelezo binafsi ya mbunge huyo.

Alisema jana baada ya kikao cha mchana kumalizika, mbunge huyo alifika ofisini kwake akiwa hajaandika maelezo yake.

"Rostam alikuja mchana ofisini kwangu bila kuleta kwa maandishi maelezo yake binafsi anayotaka kuwasilisha bungeni.

"Nilimwambia haiwezekani akawasilisha maelezo yake kabla hajayawasilisha kwa Spika kwa maandishi, na nimemwelekeza arudi akayaandike maelezo yake, kisha ayawasilishe kwangu, angalau siku moja kabla, ndipo nitamruhusu asimame bungeni na kutoa maelezo yake.

"Baada ya kumwelekeza hivyo, Rostam alinielewa na akaniahidi kwamba atafanya kama nilivyomwelekeza, hivyo akileta kesho (leo Alhamisi) maelezo yake, basi kesho kutwa (Ijumaa) nitamruhusu atoe maelezo yake binafsi mbele ya Bunge," alisema Spika Sitta.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 50 (1), mbunge yeyote anaweza kwa idhini ya Spika kutoa maelezo binafsi bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii.

Hata hivyo kanuni hiyo hiyo ya 50 (2) inaonyesha dhahiri kutoa unafuu kwa mbunge mwenye maelezo binafsi ambayo akishayatoa katika muda usiozidi dakika 15, basi hakutakuwa na mjadala kuhusu jambo hilo.

"Mbunge anayekusudia kutoa maelezo binafsi atapaswa kuwasilisha maelezo hayo mapema kwa Spika na muda wa kusema utakuwa ni dakika zisizozidi 15, na maelezo hayo hayatakuwa na mjadala kuhusu jambo hilo," inasema kanuni hiyo.

Uamuzi wa Rostam Aziz kutoa maelezo yake binafsi unatokana na Azimio la Bunge lililofikiwa baada ya ombi lililotolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wenye utata wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, ilioingia na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), Dk. Harrison Mwakyembe.

Mwakyembe alilazimika kutoa hoja ya kulitaka Bunge lidai maelezo binafsi kutoka kwa Rostam, baada ya Mbunge huyo wa Igunga, ambaye jina lake lilitajwa katika ripoti ya kamati teule ya Bunge likimhusisha na mkataba huo wenye utata wa Richmond.

Rostam katika mchango wake wa kujadili ripoti hiyo ya kamati teule iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu, alikanusha kuhusika katika kampuni hiyo na akaeleza wasiwasi wake kwamba, kamati teule ya Bunge ilifanya kazi nje ya muda wake uliomalizika Desemba 31 mwaka jana.

Akizungumza kwa simu kutoka Dodoma jana, Rostam alikiri kuwasiliana na Spika kuhusu suala hilo na akasema tayari alikuwa ameshaanza kuandaa maelezo yake ya maandishi.

"Ni kweli nimewasiliana na Spika na hapa nilipo sasa ninaandaa maandishi ya maelezo yangu binafsi," alisema Rostam alipozungumza na Tanzania Daima.

Habari zaidi kutoka Ofisi ya Bunge zinaeleza kuwa, siku Bunge lilipoanza Dodoma Jumanne wiki hii, Rostam aliwasilisha kwa Spika notisi ya maandishi akieleza kuwa tayari kutoa maelezo yake binafsi kutokana na azimio hilo la Bunge.

Kwa siku kadhaa sasa, wadadisi wa masuala ya Bunge wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kutaka kujua siku ambayo mbunge huyo wa Igunga atatoa maelezo yake kuhusu suala hilo na mambo yanayoweza kutokana na hoja yake hiyo binafsi.

Mwanasiasa mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima juzi na jana anaeleza kuwa, hali imekuwa ni ya wasiwasi mkubwa kwa pande zote zinazohusika katika suala hilo la Richmond, zikisubiri maelezo ya Rostam ambayo yanaweza kufungua ukurasa mpya katika siasa za Tanzania.

"Hali ni tete. Watu wana wasiwasi mkubwa, hawajui huyu jamaa kaandaa kitu gani, ndiyo maana kumekuwa na mizengwe katika kuwasilisha maelezo yake binafsi," alisema mbunge mmoja ambaye hakuwa tayari kujitaja jina.

Aidha, wabunge ambao wanaiunga mkono ripoti ya Kamati ya Mwakyembe ambao wamekuwa wakizungumza na Tanzania Daima kwa muda sasa, wamekuwa wakisisitiza kuwapo kwa mkakati wa kuona Rostam anaadhibiwa kutokana na maelezo atakayoyatoa.

"Ninyi subirini muone nini kitatokea baada ya Rostam kutoa maelezo yake. Tunamsubiri kwa hamu kubwa na msishangae mkisikia mbunge wa CCM akisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge safari hii," alisema mbunge mmoja.
 
jaribio lake la kwanza la kuishtukiza Bunge limefeli (angalia habari niliyoandika hapa wiki iliyopita)...

Wanajipanga upya... alitaka kufanya kitu cha ajabu sana..
 
kazi kweli kweli wanataka kurudisha mara dufu pesa zao walizopoteza kuwavalisha wapiga kura khanga na tshirts na kofia tele...za kumwaga
 
Trivial but I can't help it,

Hivi Tanzania kitu kinachoestablish nani anaitwa kwa jina la kwanza kama "Rostam" na nani anaitwa kwa jina la familia kama "Sitta" ni nini?

Naona kuna wengine wanaitwa kwa majina ya kwanza na wengine wanaitwa kwa majina ya familia, where is the formula? That is if there is one.
 
Trivial but I can't help it,

Hivi Tanzania kitu kinachoestablish nani anaitwa kwa jina la kwanza kama "Rostam" na nani anaitwa kwa jina la familia kama "Sitta" ni nini?

Naona kuna wengine wanaitwa kwa majina ya kwanza na wengine wanaitwa kwa majina ya familia, where is the formula? That is if there is one.

hasa kwa wenzetu wazungu ndio hasa wao utumia majina ya kwanza,labda kwa security reason,ila kwetu tanganyika watu wanatumia majina ya pili kwa kumuheshimu mtu.
 
jaribio lake la kwanza la kuishtukiza Bunge limefeli (angalia habari niliyoandika hapa wiki iliyopita)...

Wanajipanga upya... alitaka kufanya kitu cha ajabu sana..

Inawezekana ndiyo sababu mwanasheria wa Richmond (Cuthbert Tenga) aliibuka juzi kwenye media na kukanusha kuwa Richmond si kampuni ya kitapeli. Alisema n kampuni halali, yenye ofisi zake US. Na kwamba kwa Tz, haina kazi yoyote na wala haihusiani na Dowans.

Ni wazi huu ulikuwa mpango wa makusudi wa kuimarisha utetezi wa R.A bungeni keshoye.
 
"There are always three sides of any story".
One The accuser, second The accused and third THE TRUTH.
Tumepata side ya kwanza ya Dr Mwakyembe, sasa tunasubiri ya pili ya RA and Finally tutapata side ya mwisho.
Richmond ndugu zangu wana JF ndiyo imeanza tutege macho na masikio yetu Dodoma.
Kilicho tokea Dodoma last session kimeandika upya historia ya nchi yetu.
Let us hear what RA has to say.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
DUNISHA UHURU NA UMOJA......
HIZI NI NGAO ZETU TANZANIA NA WATU WAKE.
 


Andrew Chenge (A) Kalipotezea taifa zaidi ya sh 17,857,616,400/- zilizoporwa na Tangold ltd kutoka BOT . Chenge hili hawezi kukwepa kwani alikuwa mkurugenzi wa Tangold ltd at the same time akiwa mkurugenzi wa BOT
na kimla, Tanzania, - 10.04.08 @ 10:34 | #5878


Huyu bwana chenge alishawahi kuwa mkurugenzi wa BOT?
 
Rostam azua kizaazaa
Maelezo yake yaficha siri nzito

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti Ya Watu

MAELEZO binafsi ya maandishi ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz yanayolenga kutoa utetezi kuhusu kuhusishwa kwake katika sakata la mkataba wa kufua umeme wa dharura kati ya Kampuni ya Richmond na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), yanaonekana kuwashtua Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka Dodoma zinaeleza kuwa, Rostam aliwasilisha maelezo yake binafsi kwa Spika juzi jioni majira ya saa 12:30, saa chache baada ya kupewa maelekezo yaliyokuwa yakimtaka afanye hivyo, siku moja kabla hajapewa fursa ya kujibu Azimio la Bunge.

Hata hivyo pamoja na kukidhi maelekezo hayo ya kikanuni, Rostam alishindwa kutoa maelezo yake hayo binafsi bungeni jana kutokana na sababu ambazo hadi hivi sasa gazeti hili halijaweza kuzithibitisha.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya Bunge zinaeleza kuwa, maelezo hayo ya Rostam yanaonekana dhahiri kubeba ujumbe unaoweza kusababisha kutokea kwa mtikisiko mwingine ndani ya Bunge, baada ya ule wa Richmond ambao ulisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari hizo, uzito wa maelezo hayo ya Rostam ambayo kwa kiwango kikubwa yanaonekana kukilemea chama tawala, ulisababisha mapema jana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alazimike kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya CCM muda mfupi baada ya Bunge kuahirishwa jana mchana.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Rostam kuhusu maelezo yake binafsi jana, mbunge huyo hakuwa tayari kueleza lolote kwa undani zaidi ya kumtaka mwandishi kuwasiliana na ofisi za Bunge kwani yeye alikuwa ameshatekeleza maelekezo ya Spika.

"Nadhani mimi sina lolote la kusema la zaidi. Ninachoweza kukwambia ndugu yangu ni kwamba, niliwasilisha maelezo yangu ya maandishi kwa Spika jana jioni (Jumatano). Nasubiri kupangiwa muda wa kuyasema ndani ya Bunge kama nilivyoelekezwa katika mkutano uliopita wa Bunge. Watafuteni wahusika," alisema Rostam huku akikataa kutoa maelezo mengine yoyote ya ziada.

Tanzania Daima ilipowasiliana kwa simu na Spika Sitta jana mchana, alikiri kupokea maelezo ya mbunge huyo kwa maandishi juzi majira ya saa 12:00 jioni na akasema tayari alikuwa ameshaanza kuyafanyia kazi.

Alisema baada ya kukabidhiwa maelezo hayo, jana asubuhi aliyapeleka kwa washauri wake ambao ni maofisa wa Bunge ili waweze kuyachambua kitaalam na kisha kumpatia ushauri unaofaa, kabla ya kumruhusu Rostam kuwasilisha utetezi wake huo.

"Mimi ni Spika, nina washauri wangu, hivyo nimewakabidhi maelezo (ya Rostam) ili wayachambue kitaalam na wakimaliza watakuja kunishauri, na ushauri huo ndiyo utakaoniruhusu nimpangie tarehe ya kuwasilisha maelezo yake bungeni au la," alisema Spika Sitta.

Alipotakiwa kueleza iwapo kikao cha Kamati ya Uongozi cha CCM kilichoitishwa jana kinahusu maelezo hayo ya Rostam, Sitta alisema aliyekiitisha ni Waziri Mkuu na si yeye.

Pamoja na kukiri kuwa katika kikao hicho cha Kamati ya Uongozi ya CCM kilichoketi jana hiyo, suala hilo la Rostam lilikuwa moja ya mambo yaliyojadiliwa, Spika alisema kililenga kuzungumzia ajenda mbalimbali ambazo zimeibuka ndani ya Bunge hilo katika siku za karibuni.

Alipotakiwa kueleza nini kilikuwa kimejiri ndani ya kikao hicho kuhusu hatima ya maelezo binafsi ya Rostam, alisema yeye binafsi alishindwa kuhudhuria kwa kuwa, wakati kikifanyika alikuwa na ugeni wa Balozi wa Uingereza hapa nchini, aliyekwenda ofisini kwake kumuaga.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba, hoja ya Rostam ilijadiliwa kwa zaidi ya saa moja, na kwamba baadhi ya wajumbe walifikia hatua ya kumtaka aiondoe, pendekezo ambalo hadi jana jioni mbunge huyo alikuwa amelikataa.

Mbunge mmoja wa CCM aliyezungumza na gazeti hili jana jioni ambaye alikiri kuyaona maelezo hayo binafsi ya Rostam, anasema kikubwa kinacholeta wasiwasi ni nini kinachoweza kutokea iwapo mbunge huyo wa Igunga ataruhusiwa kutoa utetezi wake bungeni.

"Mambo yamekuwa mazito, wakubwa wamejadili hoja hii kwa zaidi ya saa nzima. Tumeambiwa kuwa wamemtaka ayaondoe maelezo yake yanayoeleza mambo mengi mapya kuhusu Kamati Teule ya Richmond iliyoongozwa na Dk. (Harrison) Mwakyembe. Mimi nimeyasoma maelezo hayo ya Rostam, tunasubiri tuone nini kitatokea ingawa naamini ni mambo mazito," alisema mbunge huyo.

Alisema, katika maelezo yake hayo, Rostam anatarajia kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu namna Kamati ya Mwakyembe ilivyofanya kazi, kujiuzulu kwa Lowassa na mawaziri wengine wawili, na namna yeye mwenyewe alivyohusishwa katika sakata hilo.

Hali hii imefikia hapo baada ya juzi, Sitta kumzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni akimtaka kwanza atimize masharti ya kanuni za Bunge yanayomtaka kuwasilisha kwake (Spika) hoja yake kabla hajaitoa bungeni.

"Nilimwambia haiwezekani akawasilishe maelezo yake kabla hajawasilisha kwa Spika kwa maandishi na nimemwelekeza arudi akayaandike maelezo yake, kisha ayawasilishe kwangu, angalau siku moja kabla, ndipo nitamruhusu asimame bungeni na kutoa maelezo yake.

"Baada ya kumwelekeza hivyo, Rostam alinielewa na akaniaidi kwamba atafanya kama nilivyomwelekeza, hivyo akileta kesho (jana Alhamisi) maelezo yake, basi kesho kutwa (leo) nitamruhusu ayatoe," alisema Sitta alipozungumza na gazeti hili juzi.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Na.50 (1), mbunge yeyote anaweza kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii.

Hata hivyo kanuni hiyo ya 50 (2) inaonyesha dhahiri kutoa unafuu kwa mbunge mwenye maelezo binafsi, ambayo akishayatoa katika muda usiozidi dakika 15, basi hakutakuwa na mjadala kuhusu jambo hilo.

Uamuzi wa Rostam kutoa maelezo yake binafsi unatokana na Azimio la Bunge lililofikiwa baada ya ombi lililotolewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wenye utata wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond, iliyoingia na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO), Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alilazimika kutoa hoja ya kulitaka Bunge lidai maelezo binafsi kutoka kwa Rostam, baada ya mbunge huyo wa Igunga, ambaye jina lake lilitajwa katika ripoti ya kamati teule ya Bunge likimhusisha na mkataba huo wenye utata wa Richmond, kuipinga ripoti ya kamati teule.

Rostam katika mchango wake wa kujadili ripoti hiyo ya kamati teule, alikanusha kuhusika katika na kampuni hiyo, na akaeleza wasiwasi wake kwamba, kamati hiyo iliendelea kufanya kazi nje ya muda wake ambao ulimalizika Desemba 31, mwaka jana.



Maoni ya Wasomaji

hapo rostam apewe haki yake a kueleza anachotaka kusema,ili tumjue mchawi nani!!hapa kunasiki kubwa lazima,kuna mambo ya kuchafuana.rostam kama unajiamini ukinyimwa nafasi ya kujieleza ndani ya bunge waite waandishi wa habari ueleze kwa kina.watanzania wameamka watachambua na kujua ukweli uko wapi.

na john - 11.04.08 @ 12:51 | #6016

inashangaza kuona baada ya taarifa ya harrison kutoka ndo viongozi na wabunge waliohitajika kutoa maelezo yao kabla na wakakataa kutoa ushirikiano ndio walewale sasa hivi wanaanza domodomo! tumeshachoka na wasanii hawa, ukweli umewekwa wazi, taarifa ya harrisson itawekwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kama mwanamapinduzi aliyekuwa tayari kufa kuipigania nchi yake kwa kueleza ukweli mbele ya matawala *******,thank
God!

na Elsaid barak, south afr., - 11.04.08 @ 13:08 | #6022

Hakuna lolote hawa watu wameamua kuifilisi nchi hii na hawana jipya. Watanzania tumeona pumba na mchele na tunamuomba mola wetu amlaze mahali pema peponi Mwalimu Nyerere. Alikuwa ni mtanzania wa kweli na kiongozi wa Watanzania. Hawa wengine ni akina kajamba nani. Hawana utu wala ubinadamu na watanzania wenzao. Watanzania tumechoka sana na hawa watu wanaoitwa viongozi kwani hawana cha uongozi wowote ni wahalifu wote kazi yao kupanga madili ya kuifilisi nchi na kuongeza umasikini Tanzania. Utasikia rais yuko China, mara London, Mara Japani n.k. Miaka yote wamekuwa wanasafiri nchi hizo hizo na hakuna jipya na wanatumia fedha nyingi za umma wacha hizo wanazojichotea kwa kupitia mikataba hewa, unafikiri kuna uongozi hapo. Yana mwisho.

na Aziz Said, Dar, - 11.04.08 @ 13:09 | #6024

Kaka Rostam kwa hili tunakuunga mkono. Tulijua wakati Lowassa anajiuzulu kulikuwa na ajenda zilizofichwa nyingi tu zikiwemo hata za makundi yaliyoshindwa urais kwenye kura za maoni za ccm 2005. Spika alikuwa mwepesi sana kuunda kamati teule na kushabikia ripoti yake.Iweje sasa Rostam azungushwe kupewa nafasi yake ya kidemokrasia tena akiwa tayari kufuata maelekezo ya azimio la kamati hiyo ya bunge? Kulikoni Spika uanze kumbana Rostam na kumchelewesha kama vile matokeo ya uchaguzi wa Urais wa Zimbabwe? We umekuwa Mugabe? Mnaogopa nini? Mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu? Moto si mliuwasha nyie wenyewe? Mpeni nafasi Rostam wananchi tujue ukweli.
 
Back
Top Bottom