Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Si Nasikia Kuna Wahariri Wengine Wako Kwenye Paycheck Ya Mafisadi!? Sasa Ni Kweli Wahariri Wa Bongo Wanaweza Kuungana? Kwa Sababu Pesa Ya Mafisadi Inaweza Kuwanunua Baadhi Yao. Cha Muhimu Ni Kumtatutia Hata Kumsaidia Kulipa Lawyer Mzuri, Ingawa Kwa System Zetu Za Afrika Mtu Aliye Kwenye Power Anaweza Kuwa-influence Majaji. Labda Kama Kungekuwa Na Jury System Na Hao Ma-jury Wenyewe Wasinunuliwe. Ila Namtakia Kila La Heri Jamaa Na Ni Kweli Wahariri Inabidi Ku-stand Up Kwa Mwenzao. Goodluck Wahariri All I Can Do Is Pray 4 U
 
Licha ya wahariri kuwa kwenye paycheque za wanaodhaniwa kuwa mafisadi (Mh. Aziz)lakini magazeti yenyewe yanamilikiwa na hao, kwa hiyo iether wahariri are in or out.
As we all know talk is cheap,
we can talk all we want,
We can click all we want, but truth is truth, and it is thre to be uncovered for those who are IN OF need it.
Kama tunataka kuosha vinywa kwa kuongea tu, its okay as ni anasa mojawapo.
Lakini nina matumaini kuwa kuna mtu anasoma, hizi hoja za humu, anachambua na anazifanyia KAZI.
 
Naomba kuuliza hivi kuna ubaya gani mtu kushtaki kama anaona ameandikwa vibaya? Na kama hakuna ubaya kwa nini wahariri wamvae huyu jamaa? Au waandishi na wenyewe wanataka kuwachagulia walaji wa habari nani aongee na aongee nini. Kama hawamtaki basi hawampi nafasi ya kuongea na akiongea anashambuliwa. Naomba wachangiaji mnisaidie kujibu hayo maswali mawili.
 
Katika toleo lake la wiki hii lililotoka leo, ukurasa wa mbele wa gazeti la RAIA MWEMA wamemuomba radhi Rostam Aziz kwa makala ambayo ilichapishwa katika ukurasa wa 15 wa gazeti hilo la Aprili 9, 2008. Naomba tujadili, je, alikua na haki ya kuombwa radhi? Je, kwanini hiyo radhi itoke ukurasa wa mbele wakati makala ilikua ukurasa wa 15? Kwanini itoke siku ambayo Mwanahalisi wametishiwa kushitakiwa?

Naanza kuchangia kwa kusema wazi kwamba BINAFSI sijafurahishwa kabisa na uamuzi huo wa Raia Mwema, kwani sisi wasomaji hatujashirikishwa kikamilifu katika uamuzi huo ambao unaashiria mambo mengi mabaya ikiwa ni pamoja na woga ama kuingia makubaliano, mambo ambayo WASOMAJI WA RAIA MWEME tunaamini kwamba si MSIMAMO wa Timu nzuri ya RAIA MWEMA ikiongozwa na mkongwe katika fani, Jenerali Ulimwengu.

MAKALA YA MIHANGWA AMBAYO RA AMEDAI KWAMBA AMEKASHIFIWA HII HAPA.

http://www.raiamwema.co.tz/08/04/09/mihangwa.php


NASAHA ZA MIHANGWA


EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (2)

Joseph Mihangwa
Aprili 9, 2008



MTANDAO wa ufisadi wa EPA unawajumuisha pamoja wafanyabiashara kadhaa akiwemo mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam.

Wengine katika mtandao huo ni pamoja na Salleth Vithlani, yule wakala wa uuzaji wa rada, vifaa vya kijeshi na ndege ya Rais aliyekuja kutoroka baadaye.

Huyo Bwana anayeishi karibu na Slipway Hotel ndiye anayesimamia mtandao mdogo unaohushisha makampuni kadhaa yaliyochota fedha za EPA. Inadaiwa pia kuwa ana hisa katika Benki M.

Wengine wenye hisa katika benki hiyo inaaminika kuwa ni pamoja na Jeetu Patel (alijitoa baadaye), Daudi Balali, Vima Meha, Sanjeer Kumar, Bhasker Narayan, Anna Muganda na wengineo.

Pia mtandao wa Jeetu Patel unamhusisha mfanyabiashara mmoja aishie nchini Kenya aliyewahi kumiliki Benki tata nchini humo “Delphis Bank”
iliyowahi kuwapora wateja zaidi ya dola milioni 90.

Aliwahi pia kumiliki nchini humo kampuni ya kuuza magari iitwayo “Marshalls Kenya Limited” na kuliuzia Jeshi la Kenya magari kwa mkataba wenye utata kama ilivyotokea hapa nchini kwetu kwa Sailesh Vithlani na Serikali yetu (mauzo ya rada).

Ni mfanyabiashara huyo pia ambaye amewahi kuwapora wateja wa Benki ya “Trust Bank” iliyosimamiwa na BOT chini ya dhamana ya Delphis Bank mwaka 1999, na hadi sasa angali anasakwa na polisi.

Wengine katika mtandao huo ni Bharat Patel, raia wa Uingereza ambaye ni mdogo wake Jeetu Patel anayeishi mjini London mwenye kumiliki kampuni iitwayo Motorsense. Yupo pia mtoto wa Bharat Patel, raia wa Uingereza anayeishi hapa nchini aitwaye Mitul Patel ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa baadhi ya makampuni yanayodaiwa kushiriki kuchota fedha za EPA.

Pengine sakata la pesa za EPA lisingejulikana na kulipuka kama mmojawao aitwaye Jitesh Ladwa asingewashambulia na kuwararua wenzake kwa kusahau kufuta pua na midomo yao!

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa “mteja mzuri” na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na “Mbwa mwitu” wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa pia kuwa, pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA.

Kuokolewa kwa Jitesh na Rostam Aziz kulijenga kambi mbili za “Mbwa mwitu” katika ufisadi wa EPA, kati ya kundi la wafanyabiashara “wapendwa” walioendelea kunufaika na BOT na kundi la “walioteuliwa” likiongozwa na Jitesh ambalo liliapa kuwalipua wale wa kundi la “wapendwa” isipokuwa Rostam Aziz kwa sababu ya umaarufu wake.

Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na “Serikali nyingine” chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni “Serikali” hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.

Kwa hili, kwa nini umma usiamini unapoona kwamba mafisadi hawakamatiki ambapo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act), Sheria ya Udhahidi (Evidence Act) na Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) zimesitishwa dhidi ya mafisadi ili waonekane kama wadaiwa wa kawaida chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Act), tena bila kutozwa riba?

Kwa nini umma usiamini hivyo unapoona kwamba fedha za ufisadi zinarejeshwa na mizuka (ghosts) isiyoonekana, lakini Serikali inakiri kuzipokea kutoka kwa “watu” (“serikali ya pili”) wasiojulikana?
Je, zinatupwa na kuokotwa barabarani?

Ajabu, yote haya yanatendeka mbele ya Tume iliyoundwa na Rais, ikijumuisha Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, na Mkuu wa TAKUKURU ambao wote ni wanasheria kwa taaluma.

Sakata la EPA ndani ya BoT liliibuka kutokana na Mbwa mwitu kuraruana wao kwa wao kiasi kwamba minyukano yao iliwaamsha wananchi wenye mali kutoka usingizini na kujionea jinsi wanavyoporwa mali zao.

Rais Kikwete aliunda Tume kuchunguza uporaji huo baada ya umma kupiga yowe muda mrefu kuwa unaibiwa. Ukichunguza kwa makini huwezi kushindwa kubaini kuwa wale wanaounda Tume, baadhi yao ni wale wale wanaonufaika na mizoga iliyoachwa na Mbwa mwitu wawindaji. Je, fisi anaweza kumhukumu mbweha anayempa chakula? Ili iweje na akale wapi?

Na kwa kuwa umma wa Kitanzania umeamshwa na minyukano ya mbweha mafisadi na kukuta umeporwa mali zake kwa muda mrefu kabla ya hapo, je kuna sababu gani kunyamazia uporaji wa kale iwapo ushahidi upo? Kwa nini Rais asiunde Tume kama ile ya EPA kufuatilia uporaji wa kale?

Tuna Serikali ya wananchi moja tu ambayo tumeambiwa haina ubia na mtu au kikundi chochote cha watu katika kuongoza nchi. Kama hivyo ndivyo, hatutarajii kuona “Serikali” ya kikundi cha mafisadi walio juu ya dhana ya utawala wa sheria wanaoweza kupora na kuyeyuka “kimiujiza” wasiweze kuguswa na mkondo wa sheria.

Inapokuwa hivyo, umma hauwezi kujizuia kuamini kwamba baadhi ya viongozi wetu wananufaika na mizoga inayotemwa na kundi la mmbwa mwitu wawindaji ndani ya nchi yao.

0713-526972

jmihangwa@yahoo.com
 
kaombwa radhi katika aya ipi? hebu tuwekee nimesoma sijaona au nami nimechoka?

Habari iliyomuomba radhi haijawekwa katika mtandao, tumeisoma tulioko Tanzania, kama uko Tanzania nunua Raia Mwema utaona... Ila makala ambayo ilimkera RA mpaka akawatisha Raia Mwema ni hiyo hapo juu, tujadili
 
Mimi sioni ubaya wacha tu wamuombe radhi!
Tumeshasoma na tumejua kilichojiri kwenye sakata la EPA kwenye hiyo makala ya Mihangwa madhambi ya RA.....Anatapatapa tu...
 
Halisi tunaomba uiscan then uirushe...

Pia mbona kuna makala zimemtetea Rostam-http://raiamwema.co.tz/08/04/23/23.php hapa napo vipi?
 
makucha ya vijisenti vimeanza kunyamazisha sasa... tusikate tamaa mwendo uwe huu huu
 
Mtu wa Pwani: Nafikiri aya zilizoleta shida kwa RA kwenye makala ya Raia Mwema ni hizi nilizozi-quote hapa chini. Baada ya kuisome hii makala ndio sasa naelewa kwa nini JK aliyamka kwamba urais wake hauna ubia kumbe tayari alikuwa amebanwa mbavu. Hii ni kubwa kwa sababu, pamoja na kwamba inasomeka vizuri sana na watu wengi wanaweza kukubaliana nayo, unawezaje kuthibitisha kwamba kulikuwa/kuna serikali mbili Tanzania ya JK na ya wafanyabiashara. Kwa hapa nawatetea Rai Mwema kuomba radhi. Hata hivyo kuomba kwao radhi sioni kama ni issue kwa sababu message yenyewe imeshakuwa sent. Sasa ni juu ya JK kuamua kuendelea kuilea hiyo serikali ya pili au aizime.

Labda ni muhimu watu wanaofikiria kugombea urais huko mbele wajifunze kwa yanayompata JK kwamba ukikubali pesa chafu zikuingize madarakani itakuwa ngumu sana kujinyofoa kutoka kwenye huo uchafu baada ya kuingia madarakani. By the way, Halisi, ile ahadi ya JK ya kuleta sheria ya kudhibiti upatikanaji wa hela za kampeni iliishia wapi au anaogopa kwamba itamrudi?

[I said:
Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na “Serikali nyingine” chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni “Serikali” hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.
[/I]
 
Halisi,

Poleni sana. Ndio mapambano hayo na muda wote kutakuwa na kupanda milima na kutelemka.

Muhimu ni kutokukata tamaa na kwa hili kama gazeti walikosea basi ni bora walivyofanya. Muhimu ni kuwa makini na kuhakikisha waandishi hawaandiki majina halisi ya wahusika mpaka pale wanapokuwa na uhakika mkubwa na habari husika.
 
You know, I do put people into two groups as far as decision concernd. A helcopter grp and a plan grp a helcopter does not take time to takeoff but a plan takes time to takeoff, so there people who used to rush to the decision without thinking or reasoning like wise RA (Huu ni ukurupukaji)if he would be in the grp of a plan wala asingefikia uamuzi wa kwenda mahakamani. People who are in a grp of a plan allways they take time to decide and find themselfs in the right way
 
Kwa sasa sina comments zozote naangalia na nitasema muda muafaka. Nataka kuwa kama Mkapa kidogo na baadaye niibuke .Kwa kuweka kijineno kuomba msamaa hakuleti nafuu yeyote kwa ukweli wa mambo ya Rostam na wana CCM wengine .Yeye ataendelea kunyamwa tu .
 
Cha msingi ninanachokiona hapa ni kwamba wote wanaweza kuwa sawa kwa mtizamo wa kisheria kwa vile bado ni tuhuma. Na kwa vile sheria inatafuta ukweli basi mahakama inaweza kuwa ndio kiwanja kizuri cha kwenda kuonyeshana mbivu na mbichi. Labda linalosumbua hapa ni suala la je ni kwa nini wahariri walishupalie. Mimi nalitazama katika jicho la utawala bora na uhuru wa vyombo vya habari... Na kwa vile wenye taaluma hivyo wanafikiri wanaweza kutetea haki ya mwanahalisi na mhariri wake mkuu kwa umoja, basi hatuna budi kukubaliana na hoja yao. Nadhani kwa mtazamo wa umoja wa wenye taaluma fulani ndio huo utasaidia kuleta mapinduzi stahiki na kutafuta kwa anayestahili haki hiyo, kwa vile haki kama hakustahili si haki yako.
Kumbe hapa tunaweza kujifunza jambo moja kwamba masuala yote yanyohusu taaluma fulani mathalan ualimu, uandishi wa habari, uhandis, na kada nyingine za kitaalam, ni vyema yakawa yatatuliwa kwa ushirikiano wa wadau wenyewe. Mie naunga mkono kwa wanahabari kutafuta namna ya kuupata ukweli kwa kutumia ushirika wa taaluma zao. Kwa vile wanazo kanuni za kiuandishi na kiuhariri zinazo waongoza katika shughuli zao, wanaweza kuona waanzie wapi katika kumsaidia mwanahabari mwenzao.
 
You know, I do put people into two groups as far as decision concernd. A helcopter grp and a plan grp a helcopter does not take time to takeoff but a plan takes time to takeoff, so there people who used to rush to the decision without thinking or reasoning like wise RA (Huu ni ukurupukaji)if he would be in the grp of a plan wala asingefikia uamuzi wa kwenda mahakamani. People who are in a grp of a plan allways they take time to decide and find themselfs in the right way

I said earlier kwamba jamaa yaani Rostam kakurupuka .Ama walio mpa ushahuri wamemkchoka wanataka akanyage mawaya arushwe ama kuna mtego wame mweka .Kaeni macho mtaona wenyewe soon. Hii kesi italeta weingi .

Juu ya wahariri wana haki kama tunavyi suggest hapa kila mara kwenda mahakamani kudai katiba .Mike alipo kamatwa JF tulikuja juu nakufanya jitihada .Leo hawa wahariri kusema ni sawa mana Kubenea wako naye .Sasa whether wako kweye payroll ama hapana tuanzie pale ambapo watamaliza kukutana tuanze kuona mwelekeo wao .
 
I absolutely agree with you Mwanangurumo for what you just said, but on the other side of the coin it's better to let that big guy RA to exercise his constitutional right... Once the truth will be revealed then we will be able to measure his ability to analyse things before making what we call final decisions in his career and personal life as well. I'll be thankful to see what will happen in the court of law. Money worth nothing but sauti za wanyonge....
 
Raia Mwema, kwa "kumwomba radhi" Rostam Aziz, wamedhihirisha ukweli kwamba wao ni wale wale wa Rai ya Rostam Aziz. Hakuna kipya. Usanii ndani ya usanii! Ndio maana sikulipenda hili gazeti!

Kaeni mkao wa kula, kitu kipya kikali zaidi ya MwanaHALISI kiko jikoni, karibu kitatoka. Utakuwa wimbo mtamu sana... yaani albam itauza kopi zote na chenji hairudi!

./Mwana wa Haki!
 
Back
Top Bottom