Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 614
Sistery mbona hapo umeniacha kwenye mataa umeshuhudia kwa macho yako hayo yakifanyika wapi? kwenye soko la hisa, au wapi?
Mwaka huu kazi ipo...
Jamani sina hakika kama Tina ni mwandishi wa habari ama mtaalamu wa kuandika. Inaonekana hana taaluma hiyo. Kama hivyo ndivyo, wataalamu kama Masatu, Kapinga, Mwanakijiji na wengineo tumsaidie kutafuta 'nyama nyama' na kuiboresha hii topic aliyoileta. Kama munasema Noni aliuza hisa zake kabla ya JK kuingia madarakani, basi Tina alikosea nahani hapo 'aliposhuhudia' kwa macho hakuangalia tarehe maana si mwandishi kama wengine walivyo humu ndani. Sina haja ya kumtetea sana maana atakuja na yeye kama amefika huko majuu akiwa salama (maana wanaweza kum-Ballali). Jambo la msingi naona hakuna aliyepinga kwamba Rostam hajaweka hisa zake nje, hakuna anayebisha kwamba alinunua hisa za Planetel. Sasa munaojua ukweli kwa hakika ni bora muweke humu tujadili badala ya kusema tu kwamba watu wanadandia ama watu hawajui. Mtu anaposema kwamba fulani hajui, yeye anajua na hivyo atuelimishe hicho anachokijua kwa manufaa ya JF na WATANZANIA wote.
TAHADHARI: Bado naona kuna jambo na kuna kila dalili hii TOPIC ikapotea katika anga za habari nchini.