Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

KakindoMaster,

Nakubaliana na wewe moja kwa moja!

Lakini si tunafahamu kuna kamati kwenye kila uchunguzi?

Hivi kweli umenikumbusha EPA imeishia wapi? Wameongeza muda maana inawezekana nimepitwa.

RA anahusishwa na Richmond mpaka sasa (kwa mujibu wa ripoti ya Mwakyembe) na tunasikia PM anasubiri kibali cha Spika ili kutangaza utekelezaji wake.

Sasa katika hili Rais afanye nini?

Hivi hiki Kibali kimeagizwa kutoka nchi gani?

Si nasikia hata Dowans haikuwa na Makataba? au ilikuwaje?
 
KakindoMaster,

Nakubaliana na wewe moja kwa moja!

Lakini si tunafahamu kuna kamati kwenye kila uchunguzi?
RA anahusishwa na Richmond mpaka sasa (kwa mujibu wa ripoti ya Mwakyembe) na tunasikia PM anasubiri kibali cha Spika ili kutangaza utekelezaji wake.

Sasa katika hili Rais afanye nini?

Nina maswali mawili kwako...NCHI INAONGOZWA NA NANI?
Majibu ya RIPOTI YA KINA MWEMA YANAPEWA NANI?
Yani umesahau hayo yote?
 
Hapa ndipo ninapochanganyikiwa , watanzania wengi wanataka eti mtu aseme, sidhani kama Rostam amezungumza habari za udaku, action and reaction are equal bust opposite.The whole issues za ufisadi tumeziweka kidaku zaidi kuliko vitendo.Mafisadi wanatamba, wanaongea wako mitaani na ndio hao wanawaita na kuwaeleza hayo.mimi nigekuwa mwandishi wa habari nisingeenda maana naona ni kupoteza muda.Kama ameshakuwa tuhumiwa kuhusika na Ufisadi KWA NINI YUKO MITAANI? WAANDISHI WA HABARI WAMEFUATA NINI KAMA SIO UDAKU NAO?

TUAANDIKA MPAKA VIDOLE VITUUME, LAKINI KAMA HATUTACHUKUA HATUA HATA ZA ''NGUVU'' NCHI HII HAIENDI.ANASEMA KAMA YUPO MWENYE VITHIBITISHO AENDE MAHAKAMANI!! KWANGU MIMI NAONA MATUSI.KATIKA NAKALA YANGU YA ROSTAM VS KKKT-DMP, NIMEELEZA SWALA LA VYAMA VYA UPINZANI KUWA NI WANAFIKI WOTEEEEEEEEE. MAMLAKA ZA KISERIKALI NDIO HIZOOOOOOOOO.RAIS NDIYO HUYUUUUUUUUUUU.

TWAFAAAAAAA!!!!!!1
 
wananchi tukubali tuliingia mkenge kuchagua mkulu jk.Tujirekebishe 2010

JK ndiye aliingia MKENGE KWA KUPATA MADARAKA KUTOKA KWENYE UCHAGUZI AMBAO PESA ZA EPA ZILITUMIWA.

HIVYO KAMA HATAKI KULISHUGHULIKIA HILI SWALA KWA NAMNA TUNAYOMPA USHAURI...THEN NA YEYE ATAKUWA NI RAIS BATILI NA PIA WOTE YEYE NA MKAPA WANAWEZA KUJIBU MASHTAKA MAHAKAMANI.
 
Ameshakuwa batili tangu siku nyingi mkuu Mushi

Kalenge
Man is by nature a political animal’’Aristotle (384 BC - 322 BC)
 
Afanye mapinduzi...Awe kama kiongozi wa kweli...Chama chake kizaliwe upya na Taifa lizaliwe UPYA...Taifa lirudi PAMOJA NA SHERIA ZA PAMOJA ZITUNGWE KWANI TUMESHANGUNDUA KUWA HAKUNA MAWAZO YA MTANZANIA YATAPUUZIWA!

Wote iwe upinzani ama whatever...TUNASIKILIZA NA PIA KUFUATILIA UTENDAJI WAO...Hatutaki maslahi ya chama tunataka umoja wetu kama TAIFA!

TUNATAKA THE TANGANYIKA REVOLUTION!

TUNATAKA MAPINDUZI...TUNASUBIRI WA KUTUONGOZA....NA TUTAMSIKILIZA...KWANI SAUTI ZAO ZINAJULIKANA NA KUWEZA KUTAMBULIWA MASIKIONI MWA WAZALENDO...NA SI KAULI TU..BALI HATA VITENDO!
 
Ameshakuwa batili tangu siku nyingi mkuu Mushi

Kalenge
Man is by nature a political animal’’Aristotle (384 BC - 322 BC)

Nilkuwa najaribu kumwelewesha THINK BIG kwani naona anafagilia kisichofagilikika.
 
Nilkuwa najaribu kumwelewesha THINK BIG kwani naona anafagilia kisichofagilikika.

waTanzania tu wazuri katika kuongea lakini hakuna vitendo ... Ndio maana sishangai tunapomnyooshea vidole Rais .. kwasababu sisi (wananchi) tunapenda kuongea na vitendo tumwachie mwingine atekeleze!

Na leo hii tunaonyesha tumemchoka kweli (JK), lakini cha ajabu ni sisi tena tutamrudisha 2010! Kwasababu tunapenda kuongea na kunyoosheana vidole bila kuonyesha vitendo!
 
wananchi tukubali tuliingia mkenge kuchagua mkulu jk.Tujirekebishe 2010

Ambianeni.

Wengine tulikuwa ile 20%.

Labda wenyewe kwa wenyewe mtasikilizana, mtaaminiana. Sisi hamkutuelewa.

Na msiposaidia kuambiana kitakachofanyika ni atashuka kidogo tu, toka kura 80.3% kwenda 55%. Good enough, isn't it?

Halafu Kikwete-Shein itarudi kumalizia kazi, kuanua jamvi, na kutandika zulia kuandaa Karume-Malecela 2015.
 
waTanzania tu wazuri katika kuongea lakini hakuna vitendo ... Ndio maana sishangai tunapomnyooshea vidole Rais .. kwasababu sisi (wananchi) tunapenda kuongea na vitendo tumwachie mwingine atekeleze!

Na leo hii tunaonyesha tumemchoka kweli (JK), lakini cha ajabu ni sisi tena tutamrudisha 2010! Kwasababu tunapenda kuongea na kunyoosheana vidole bila kuonyesha vitendo!

Hivi unaweza kuniorodheshea madaraka yote ya kikatiba aliyo nayo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?

Hilo litasaidia ili niweze kukueleza kwa ukamilifu kabisa kwamba yeye kama AMIRI MJESHI MKUU ANAWEZA KUFANYA NINI.
 
anasema "natoa changamoto kwa mtu yeyote mwenye ushahidi wa vitendo vya uvisadi awakilishe hayo kwenye vyombo vya sheria"

Lahaula! fisadi anajitahidi kujisafisha lakini hata hajui aanzie wapi!!!...Na sisi tunakupa changamoto. Kwanza twambie mali zako zote ulizonazo na pia una shares katika makampuni gani ndani na nje ya Tanzania. Pili twambie ni biashara gani unazozifanya zilizokupatia utajiri na umeanza kuzifanya lini. Je, unalipa kodi katika biashara zako hizo mbali mbali? Una uthibitisho wowote kwamba hizo biashara zimelipiwa kodi? Je, kama unadai huna uhusiano na Richmond ilikuwaje kampuni hiyo itumie sanduku la barua lilitolewa kwa jina lako.
 
Wakuu,

Pamoja na kwamba Rais wetu ni "mnyonge" lakini katika hili mnataka aingilie nini? Mbona haya mambo ni ya kawaida tu na wala hayaingiliani na utawala au serikali yake?

Mambo ya RA kusema bila ya kutaja wahusika, eti
.. wanatembea na watoto wadogo,
.. nimeshawahi kumpa Mtikila milioni 3,
.. mbona wakristo hutangazwa wakisaidia taasisi za kiislamu,
.. na kadhalika

haya hayaingiliani na utawala wa nchi, mpaka tumuhusishe Rais, kwa sisi haya ni malumbano ya wafanyabiashara, na kwa upande mwingine ni mpambano wa wanasiasa!

Katika hili Rais hatakiwi kufungua mdomo, anatakiwa kufungua mdomo iwapo serikali yake imeguswa, ama mmoja wa wasaidizi wake anaguswa moja kwa moja na maneno hayo ya RA! Na uzuri wa RA anazungumza bila kuweka wahusika, hata hao wahusika ni sisi (JF) ndio tunaowataja! Sasa katika hili Rais aanzie wapi?

Angekuwa ameamua tangu mwanzo kuzishughulikia tuhuma zote za ufisadi bila kumuogopa yeyote yule awe tajiri wa kupindukia au kingunge wa kupindukia haya ya fisadi Rostam kuitisha kikao cha waandishi wa habari pale Kilimanjaro Hotel.

Wameshaona kuna vacuum kubwa katika vita dhidi ya mafisadi na wanamjua mkuu wa nyumba mwenyewe siyo msafi na walimsaidia kwa mali zao za kifisadi ili aingie Ikulu. Sasa wamegundua jamaa ni muoga na hana ubavu wa kuwashughulikia ndiyo maana wanapata jeuri ya kuchonga. Waungwana, haya ndiyo matokeo mabaya ya kuingia Ikulu kutumia njia za kifisadi.

Angekuwa Rais jasiri na anayetaka kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania huyu Rostam Azizi na wengineo wengi wangekuwa rumande wakati uchunguzi unaendelea.
 
Bubu ataka Kusema,
Lahaula! fisadi anajitahidi kujisafisha lakini hata hajui aanzie wapi!!!...Na sisi tunakupa changamoto. Kwanza twambie mali zako zote ulizonazo na pia una shares katika makampuni gani ndani na nje ya Tanzania. Pili twambie ni biashara gani unazozifanya zilizokupatia utajiri na umeanza kuzifanya lini. Je, unalipa kodi katika biashara zako hizo mbali mbali? Una uthibitisho wowote kwamba hizo biashara zimelipiwa kodi? Je, kama unadai huna uhusiano na Richmond ilikuwa kampuni hiyi itumie sanduku la barua lilitolewa kwa jina lako.

Mkuu lazima tukubali tumeisha pigwa bao na Rostam..
Anajua fika hakuna mwananchi anayeweza kuja na Ushahidi hasa baada ya kuona yaliyowakuta kina Balali --(warning)...
Kifupi ukilisoma swali la Rostam, hatuna jibu isipokuwa kuuliza swali...
Ushahidi upo ktk banda la Simba mla nyama ya watu..nani atakayeweza kujitoa mhanga?...
 
Mkandara ningeomba uwe specific kidogo...Umesema ushaidi Dhidi ya mafisadi umerudi kwa simba mla nyama?
Kivipi?
Maana si kina Slaa wana ushahidi wote?
Ama na wao wamempa Simba mla nyama za watu?
 
Angekuwa Rais jasiri na anayetaka kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania huyu Rostam Azizi na wengineo wengi wangekuwa rumande wakati uchunguzi unaendelea.

Kwa hiyo Jongwe angekuwa ni mtanganyika angetufaa?
NB: Jongwe ni Mugabe...kwi kwi kwi kwiiiiiii
 
Last edited by a moderator:
Angetufaa vizuri tu...Maana maslahi ya watanzania yangezingatiwa na si kugawana mali za taifa na kina Sinclair.
 
Bubu ataka Kusema,

Mkuu lazima tukubali tumeisha pigwa bao na Rostam..
Anajua fika hakuna mwananchi anayeweza kuja na Ushahidi hasa baada ya kuona yaliyowakuta kina Balali --(warning)...
Kifupi ukilisoma swali la Rostam, hatuna jibu isipokuwa kuuliza swali...
Ushahidi upo ktk banda la Simba mla nyama ya watu..nani atakayeweza kujitoa mhanga?...

Mkuu mimi bado naamini kwamba Fisadi Rostam hajatufunga goli. Naamini kabisa kwamba tukiendelea kumshinikiza JK na serikali yake basi ni lazima wafanya uchunguzi wa kina kuhusu watuhumiwa mbali mbali wa ufisadi.

Unasikia sasa hivi baadhi ya wabunge wanaanza kuongea pembeni kumkimbia JK hapo 2010. Hili halijawahi kutokea ndani ya nchi yetu wabunge wa chama twawala kutaka kutishia kumkimbia kiongozi wa chama chao katika uchaguzi unaokuja. Hawa pia wanayatathmini mambo wanayoyasikia ndani ya majimbo yao. Kama JK hakufanya lolote kati ya sasa na mwishoni mwa mwaka 2009 basi wajiandae kwa wizi mkubwa wa kuiba kura 2010, vinginevyo wanaweza kuwa ni chama cha upinzani bungeni na yeye mwenyewe CCM kuumtema na kutafuta mgombea mwingine.

Kamwe katika vita hii dhidi ya mafisadi tusikubali kunyoosha mikono juu mapema, kufanya hivyo ni kuwapa ushindi mafisadi.
 
Kuna swali moja ambalo ameulizwa mwisho na waandishi kuhusu Richmond na ambalo jibu lake ukilisikia kwa wengine linaridhisha lakini kwa mtu anayesikiliiza makini atagundua Rostam amefanya kitu gani katika jibu hilo.

Ndani ya nusu saa zijazo mtamsikia wenyewe akielezea mambo haya.
 
Nina mashaka kwamba wale wanaomsema Rostam Aziz, kuna siku wanaweza kutafuta sehemu ya kujificha... maana mpaka leo hakuna tangible evidence za uchafu wa Rostam Aziz zaidi ya kwamba jamaa wa watu utajiri wake labda ndio unamponza ikiwa ni pamoja na Rangi yake... Lakini wananchi anaowawaklisha angalau bado wako naye.
 
Back
Top Bottom