Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtikila anamwaga point nyingi sana hapa nafikiri Rostamu kama alifikiri kusema milioni tatu alikuwa amemaliza sasa inawezekana akawa amewasha moto ambao hataweza kuuzima.
Hawa watu inawezekana si raia wa tanzania nafikiri tufuatilie RA amesoma wapi? na hao ndugu zake wamesoma wapi anaweza kupatikana kirahisi sana.
hivi kwanini Rostam alisema suala la watu wasioheshimu ndoa zao akijua mengi ya JK na ushemeji wao?
Ujumbe mzuri. Naona umeingia kwa kasi sana humu kumtetea Mtikila. Kama unajua waliomtuma waambia nawaambie wamemfanya mwenzao ang'ate mkono uliokuwa ukimlisha lakini pia amejianika vile alivyo! mtupu kabisa. Mpe shukrani kwa kujifunga mabomu na kujilipua. Amesaidia kumshughulikia FISADI Rostam Aziz ila na yeye amekufa. Mwenzie bado anatapa tapa ila na yeye lazima amaliziwe. Mtikila is not a pastor, he is an impositor. Hoja zake kwenye huo waraka zina maana lakini yeye mwenyewe haya maana kabisa. Na hoja zake za ufisadi zina maana, lakini hoja zake za ubaguzi hazina maana kabisa! Tell him, shame on him!
Asha
Wezi hawa wanaipora nchi hii bila huruma, na ndio wanaowaambia watawala wa CCM cha kufanya ili wakombe mapesa yetu B.O.T na Hazina, na kutumia matrilioni yetu kuwatia viongozi wetu ndani ya mifuko ya makoti yao, ambamo wanalishwa masazo yao na kuchomoza vichwa kuchungulia nje kama vindege kuwasanifu wananchi, na kurudi mifukoni mwao wakidhani wanakula kumbe wanaliwa wao na Nchi yao! Hatutaki Rais wetu wala Wabunge wetu wawe vindege ndani ya mifuko ya makoti ya Rostam Aziz na Yusuf Manji!
[/B]
Kwa vile Rais Kikwete anahusika katika uporaji huu ambao ulimnufaisha hata katika hila za mtandao wake za kumwingiza Ikulu, na kutokana na udhaifu wake mkubwa wa kujali zaidi maslahi ya kibinafsi na maswahiba kuliko hatima ya nchi na walalahoi, tulifahamu kabla ya tamko lake kwamba atamtumia Mkurugenzi wa Mashitaka (Director of Public Prosecution) kuwalinda wote waliohusika katika uporaji wa Nchi pamoja na mtuhumiwa mkuu Benjamin William Mkapa.
Ndiyo maana Kamati hii ilianza kazi yake mwaka 2006 kwa kufungua kesi ya Katiba Nambari 86/2006 ili kumwondolea Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mamlaka makubwa mno kupita matakwa ya Katiba ya Nchi, yaliyompa uwezo wa kuwalinda maharamia wote ambao Rais hatataka washitakiwe na kufungwa na kufilisiwa. Ndipo unaposimama ujasiri wa Kikwete wa kutamba kwamba atayalinda majizi ya mapesa yetu ya EPA, Richmond/Dowans yasifikishwe mahakamani! Tunataka haki ya wananchi ya kujiendeshea mashitaka wao wenyewe wasipokuwa na imani na DPP.
Swali zito ni Kwanini Mahakama Kuu haitoi hukumu ya kesi hii nyeti ya hatima ya Nchi yetu na uhuru wetu?
KAMATI YA KUPAMBANA NA UPORAJI WA NCHI
PUBLIC INTEREST LITIGATION COMMITTEE
(PILCOM)
Kamati hii ilianza kujiunda tangu mwaka 2006 na wahanga wa ukombozi wa nchi yetu, kutoka katika Vyama vya siasa, taasisi za kidini, makampuni ya wanasheria mahiri, Taasisi huru za wananchi, na mshikamano mtakatifu wa wazalendo ndani ya Bunge letu, ambalo katika Ibara ya Nane ya Katiba ya Nchi yetu ndilo linaloitwa Wananchi. Ni mbinu yetu ya vita kutowaweka wazi wahanga wetu kwa sasa.
Bank nazo si zimejaa ufisadi uleule? ukienda mweusi upati ukienda mweupe hata bila bond unapewa unazopenda sio unazohitaji. Upo hapo?Unajua hapa Mtikila hakujipanga lakini ndo hivyo kaharibu kauli alizotoa zinasababisha RA ajipange zaidi kummaliza kabisa Mtikila.Cha kusikitisha alishindwa hata kwenda kukopa BANK?
Mwanahalisi usiogope. Wengi tunakuunga mkono. Kama walitaka kukutoa roho pale walipokumwagia tindikali na bado hukuogopa kuendelea kuwaumbua, nini shs bilioni 3?. Kweli Mwanahalisi halina hizo bilioni 3 lakini sisi maskini wengi tunaotetewa na Mwanahalisi tutazichanga.
UJUMBE KWA ROSTAM: Fanya haraka uende mahakamani maana hata hilo ulilozuiwa kulisema bungeni, utaweza kulisema mahakamani!