Siku zoote nimekuwa nikiamini RA is one of the smartest crooks we have in TZ lakini inaonekana si kiiivyo!!!!!!! With this one, jamaa ameplay so low!
Well mitambo ya dowans inauzwa na hii inaonekana imewekwa jana kwenye alibaba.com maana watu tumekuwa tukiitafuta details za DTL siku nyingi kwa kugugo na only this morning tunaiona hii ikiambatana na press release (Soma mwananchi hapo chini) iliyotolewa jana hiyo hiyo na Dowans. Soma mwenyewe uangalie hizo details za muuzaji halafu tell me kwamba je ni kweli hapa kuna uuzaji au changa la macho.
Mauzo (Bofya hapa mbele):
On sale - Dowans Tanzania Ltd - Energy,
How do u sell stuff that is worth $100m (as quoted from Dowans)
1. Huna Address?
2. Mtu wa kumpigia anasema call me?
3. Simu yenyewe imekaa kimazabe mazabe au kimagumashi?
4. Company details hamna?
5. Hamna picha
KWA KIFUPI HUYU JAMAA SASA ANATAPATAPA. ETI HUU NI USHAHIDI KWAMBA WALIKUWA WANAUZA SI KWA TANESCO TU. But why ianze kuonekana kuanzia leo asubuhi????????
Dowans yaibuka na kitendawili
Mwananchi Tanzania News Paper
KAMPUNI ya Dowans Tanzania Limited (DTL) jana ilivunja ukimya wake katika sakata la ununuzi wa mitambo ya kuzalishia umeme wa dharura na kutoa taarifa ya ufafanuzi wa sakata hilo, huku ikiendeleza kuficha wahusika wake hapa nchini.
Serikali imekuwa ikihaha kutaka kununua mitambo hiyo ya Dowans, ambayo ilirithishwa mkataba wa uzalishaji wa umeme wa dharura kutoka kampuni Richmond Development Company iliyoshinda zabuni hiyo mwaka 2006, lakini wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wadau wengine wamepinga vikali azma hiyo wakitaka Sheria ya Manunuzi ya Umma, inayopinga ununuzi wa mitambo ambayo ni mitumba, iheshimiwe.
Tangu kuanza kwa sakata hilo mwishoni mwa mwaka jana wakati Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iliposhauri mitambo hiyo isinunuliwe, Dowans imekuwa kimya licha ya watu kadhaa kuhoji umiliki wake, huku watendaji wake wa hapa nchini wakikaa mbali na vyombo vya habari.
Lakini jana, Dowans ilitoa tangazo ambalo halikuwa na jina la aliyelitoa wala wadhifa wake, ikijielezea kuwa ni kampuni safi ambayo imefanya kazi sehemu mbalimbali duniani na kwamba mitambo yake ni bora, ambayo kama si Tanesco ingeshapata mnunuzi zamani.
Pia Dowans imetetea azma ya Tanesco ya kununua mitambo hiyo, lakini kuponda kitendo chake cha kusitisha mkataba uliokuwa uishe Septemba mwaka huu, ikisema kuwa kilifanywa bila ya kuwepo kwa malalamiko yoyote ya uzalishaji mbaya na kwamba kitendo hicho kimejibiwa kwa hatua muafaka, ambayo ni kuishtaki kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara.
"Kwa kutilia maanani ukubwa wa uwekezaji wa DTL, madai na shutuma kwamba DTL siyo chochote na kuwa siyo mwekezaji makini na mwenye msimamo siyo za kweli, ni za kupotosha na kwa kweli ni za kupakana tope tu," inasema taarifa hiyo ya Dowans iliyotolewa na mtu ambaye hakutajwa jina wala wadhifa wake.
"Isitoshe, tofauti na ripoti kadhaa zisizokuwa za kweli, mitambo ya kuzalisha umeme ya Dowans haikurithiwa kutoka kwa mtu mwingine".
DTL ni kampuni makini ambayo ilijiingiza kwa nia nzuri katika shughuli hiyo kwa misingi ya kibiashara.
"Mkataba wa DTL na Tanesco ulifikiwa kwa majadiliano ya wazi kabisa na DTL inaridhishwa na utendaji wake kwa muda wote wa mkataba kwa sababu tuliutekeleza mkataba huo kama ilivyostahili.
Na ili kuondosha shaka lolote, DTL haina uhusiano na haijapata kuwa na uhusiano na kampuni ya Richmond Development Company LLC, kampuni ya Texas, ambayo awali ilishinda mkataba wa kuzalisha umeme kwenye eneo la Ubungo.
"Yamekuwapo madai vile vile kuwa mitambo ya kisasa kabisa inayotumia gesi ya DTL ni mizee na michakavu". Wakati wote wa muda wa mkataba kati ya Dowans na Tanesco, suala la utendaji na uwezo wa mitambo halikupata kutokea wala kutajwa na Tanesco, kwa sababu kila moja ya mitambo hiyo ni aina ya mitambo ya kuzalisha umeme inayoheshimika na kukubalika duniani, na kuwa mitambo hiyo ilinunuliwa moja kwa moja kiwandani kwa mtengenezaji/mwuzaji ikiwa mipya chini ya dhamana ya mwuzaji.
"Mitambo yote mitano inao uwezo wa miaka mingi wa kufanya kazi, na kama itatunzwa vizuri, inaweza kuendelea kuzalisha umeme kwa zaidi ya miaka 25."
Taarifa hiyo pia imezungumzia hatua ya mkurugenzi wa Tanesco, Dk Idris Rashid cha kusitisha mkataba huo kabla ya kipindi chake kumalizika, ikisema kuwa kilifanywa bila ya kuwepo na sababu yoyote iliyo dhahiri wala kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa Dowans.
Dk Rashid, ambaye amekuwa mstari wa mbele kushinikiza kununuliwa kwa mitambo hiyo, aliandika barua ya kuvunja mkataba na Dowans mwishoni mwa Julai, akisema urithishaji mkataba kutoka Richmond ulikuwa na matatizo ya kisheria na pia utata katika usajili wa Richmond, ambayo ilishindwa kuleta mitambo hiyo ya kuzalisha umeme wa dharura.
Hata hivyo taarifa hiyo ilifafanua kwamba, agizo la Tanesco la kuiamuru DTL kuacha kuzalisha umeme lilikuja ghafla, wakati DTL haikuwa na mipango bora zaidi ya kupata matumizi mengine ya mtambo wake katika eneo la Afrika Mashariki.
"Hatimaye, kwa kukiuka agizo lake la kutaka DTL iache kuzalisha umeme, Tanesco, kwa mara nyingine bila kuiarifu Dowans, ilifanikiwa kupata amri ya mahakama iliyotolewa bila DTL kuwasilisha maelezo yake, ya kuizuia DTL kuendelea na mchakato wa kujaribu kuuza mtambo wake. Hii, bila shaka, itaongeza gharama ambazo DTL tayari imeingia. Amri hiyo ya Mahakama... inapingwa kwa njia mwafaka," inaeleza taarifa hiyo ya Dowans.
Kuhusu hatua ya Tanesco kung'ang'ania kununua mitambo ya Dowans, taarifa hiyo inaeleza kuwa shirika hilo la umeme si mteja pekee kwa sababu tayari ilishaanza mchakato wa kuiuza katika soko la dunia, ambalo kampuni hiyo imedai lilivutia wateja wengi. Lakini imeeleza kuwa kitendo cha Tanesco kwenda mahakamani na kufanikiwa kupata amri ya kuzuia kuuzwa kwa mitambo hiyo ndio kumeifanya isitekeleze azma hiyo.
"Taarifa hiyo ilizidi kueleza kuwa, ingawa Tanesco ilijitahidi kutafuta kila njia ili kuikwamisha Dowans katika mipango yake, DTL ilikaribisha wanunuzi kwa njia ya uwazi na iliyo ya hadhara kutoka makampuni ya kimataifa yenye sifa ya kununua mitambo yake, inaeleza taarifa hiyo.
"Kwa hiyo hisia zozote kuwa TANESCO ilitaka kununua mtambo huo kinyemela na bila ushindani ni jambo lisilo la kweli. Kwa kutilia maanani mahitaji makubwa ya kimataifa kwa ajili ya mitambo ya kisasa kama hiyo na maombi yenye ushindani mkubwa ambayo yamepokelewa, ni dhahiri kuwa Mitambo hiyo ingekuwa imeanza kutumika kibiashara sehemu nyingine siku nyingi, kama isingekuwa kutokana na amri ya bahati mbaya kabisa ya mahakama iliyotolewa kwa Tanesco."
Dowans Tanzania Limited, ambayo inamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Dowans ya Costa Rica na Portek ya Singapore, imekuwa haipatikani kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu kutokana na watendaji wake kuelezwa kuwa wako nje kikazi kila wanapofuatwa kwenye ofisi zao zilizopo Ubungo.
Jana, Mwananchi ilifanikiwa kumpata mmoja wa maofisa wake ambaye nambari yake ya simu imewekwa kwenye tovuti yao, lakini hakutaka kutoa maelezo yoyote zaidi ya kuahidi kuwa wangetoa taarifa.
Mtu huyo, aliyekuwa akizungumza lugha ya Kiingereza, alikataa hata kutaja jina lake, akisema kuwa vyote vingekuwepo kwenye taarifa yao.
Lakini, taarifa hiyo (iko ukurasa wa 14 wa gazeti hili) haikutaja jina la mtendaji huyo wala muhusika mkuu hapa nchini. Hata mwandishi alipokwenda kwenye ofisi za kampuni hiyo jana, alijibiwa kuwa taarifa hizo zote zingetolewa kwenye tangazo hilo.
Ikizungumzia mitambo hiyo aina ya TM 2500 na LM 6000PD iliyotengenezwa Marekani na yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 120, Dowans imeielezea kuwa ni ya bei nafuu, iliyonunuliwa ikiwa mipya, iliyotumika kwa muda mfupi na yenye uwezo wa kuendelea kufanya kazi kwa miaka 25 ijayo kama ikitunzwa vizuri.
"DTL ilifunga na kuzindua mtambo huo wa kisasa kabisa kwa gharama ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 100. Gharama hizo zinalingana, ama kuzidi, kabisa na gharama zinazokubalika kimataifa za kufunga mitambo ya umeme za kiasi cha Dola za Marekani milioni moja kwa megawati moja ya uwezo wa kuzalisha umeme (installed capacity)," inaeleza taarifa hiyo.
"Ni jambo lisilowezekana kufunga Mtambo unaofanana na huo kwa gharama ya dola za Marekani milioni 30."
Taarifa hiyo inalinganisha thamani ya mtambo wake na miradi mipya ya Kenya, ambako umefungwa mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 90 kwa gharama ya Dola 160 milioni za Kimarekani, Rwanda (mw 100 kwa Dola 325 milioni) na Ghana (mw 660 kwa Dola 900 milioni za Kimarekani) kuwa sehemu ya mifano ambayo inaonyesha gharama za mitambo hiyo kuwa kubwa.