Rostam Aziz yumo kwenye ziara ya Rais Marekani, nawapa taarifa tu wale mliomwona kwa mara ya mwisho ziara ya Mwendazake Morogoro.

Rostam Aziz yumo kwenye ziara ya Rais Marekani, nawapa taarifa tu wale mliomwona kwa mara ya mwisho ziara ya Mwendazake Morogoro.

Hamna kitu, hao jamaa mnawakuza lakini naamini hawahusiki na chochote kwenye kumuweka mtawala, TISS, tume ya uchaguzi na polisi ndio wahusika wakuu.

Huwezi kuniambia mtu kama Magufulj aliwekwa na huyo Rostam, hao ni wajanja tu wanaotumia nafasi zao kujenga mahusiano na watawala ili wajitengenezee ulaji kwenye biashara zao, ndio maana hata wakati wa Magufuli bado Rostam alikuwa karibu naye.
Janja janja tu.

Hamna lolote.
 
Tanzania matajiri ni wahindi

Sasa wewe hata kiwanda huna Tanzania nani anakujua

Hao wahindi wana apartment Canada na Marekani na wana passport za kihuni mbili mbili kwa siri

Wanaitwa watanzania lakini kikinuka wana passport za Canada na Marekani wanakimbia

Huyu ni moja ya matajiri wanaomiliki billions of dollars na sio shilingi
Huyo Rostam siyo muhindi acha kukariri, ni mu Iran na kampuni yake kaipa jina la kwao Caspian.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hamna kitu, hao jamaa mnawakuza lakini naamini hawahusiki na chochote kwenye kumuweka mtawala, TISS, tume ya uchaguzi na polisi ndio wahusika wakuu.

Huwezi kuniambia mtu kama Magufulj aliwekwa na huyo Rostam, hao ni wajanja tu wanaotumia nafasi zao kujenga mahusiano na watawala ili wajitengenezee ulaji kwenye biashara zao, ndio maana hata wakati wa Magufuli bado Rostam alikuwa karibu naye.
Umesema ukweli. Rostam kidogooooo wakati wa Kikwete mwanzoni alikuwa na ushawishi kwa sababu ya fedha alizotoa kuwezesha Kikwete kuingia madarakani. Baada ya lile sakata la ''magamba matatu'' nguvu zake ziliisha na sasa amebaki mtu anayejipenyeza kwa watawala ili apige madili. Ila kipindi hiki cha Samia atapiga sana kwa sababu Samia ni mtu wa kuachia mambo yajiendee yenyewe. Kuna player mwingine tena ameingia kwa kasi sana sasa hivi, huyu jamaa wa Home shopping Center. Mohamed Dewji naye yupo kwa usiri sana japo Magufuli alimuonyesha cha moto kwa kutaka kufadhili ile operation ya kumuondoa kuwa mgombea wa CCM.
 
RA anaendelea kupunguza wazururaji mtaani!
Angalia investments zake siku za karibuni:
1) Williamson Diamond mine(Mwadui) - $15M
2)Tigo na Zantel (Partnership na Axian) - $100M
3) Mkataba na Northern Feed Company - $500M
4) Tancoal Energy ?
 
Nimekutana na heading kwenye gazeti la The Citizen akiitaka AfDB kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji. Mwamba huyu yupo.Ni hayo tu.
Acha wivu
Jamaa analamba asali
 
Tanzania matajiri ni wahindi

Sasa wewe hata kiwanda huna Tanzania nani anakujua

Hao wahindi wana apartment Canada na Marekani na wana passport za kihuni mbili mbili kwa siri

Wanaitwa watanzania lakini kikinuka wana passport za Canada na Marekani wanakimbia

Huyu ni moja ya matajiri wanaomiliki billions of dollars na sio shilingi
Upo uwezekano hata Ka Nzi unamjua
?
Riatam ni tajiri kweli
 
Huyo ndiye mtu gani? Ni nani..sijawahi kumsikia. Nisije kuwa nimepitwa.
Teh teh teh teh 😂😂😂 ...haaa..😂😂😂...nakumbuka enzi za awamu ya 4 na mada kuhusu 'king maker' nilikuwa napenda Sana kusoma michango yako (ulikuwa mkosoaji mkubwa sana wa ile awamu ).

Japo nilikuwa msomaji tu ila nilivutiwa kujiunga JF miaka kadhaa baadae, baada ya kuwa msomaji Sana wa mada na michango ya wadau wa humu (ikiwemo wewe).
 
Mfumo wa ujamaa umejenga sana chuki dhidi ya wafanyabiashara wenye mafanikio. Mpaka wanasiasa wanaogopa kuonekana karibu nao. Ni kitu kibaya sana tumejifunza.
 
2015 Magufuli ni zali tu lilimwangukia, aliandaliwa Edo lakini kwa sababu zisizoweza kuzuilika ilibidi mkasi upite na mbadala ilikuwa Membe. Kwa kumkomoa mkata mkasi kura alipigiwa Magufuli.
Uwongo mtupu, story ya vijiweni hii. Magufuli ndiye aliye andaliwa kushika kijiti 2015
 
Back
Top Bottom