Rostam Azizi ahoji wawekezaji uchwara

Watu wanazungumzia kama vile umasikini ndiyo chanzo. Na wakati kumbe umasikini nao una chanzo.

Tunarudi kule kule kwa serikali. Inachukua kodi nk lakini haitaki kukubali kuwa yenyewe ndo sababu ama pengine chanzo cha umasikini.
 
Michezo yote ya kubahatisha ilitakiwa kufanywa na Bahati Nasibu ya Taifa. Nina mfano wa nchi ambazo hii michezo inafaidisha sana wananchi kwa sababu hufanywa na mashirika ya umma na fedha zinazopatikana huelekezwa kwenye mambo muhimu ya Taifa. Kwa mfano hapa kwetu, tungeweza kutumia fedha zinazopatikana kwenye kujenga madarasa au hospital, kuchangia gharama za elimu ya juu nk. Tatizo hapa kwetu imekuwa holela, unregulated na faida inayopatikana inachukuliwa na watu binafsi huku jamii ikiangamia. Ingefanywa na serikali basi ingekuwa rahisi hata kudhibiti vijana wasiwe addicted.
Kuhusu ''someone, somewhere has to say something'' hili nakubaliana na wewe kabisa. Na wala simpingi Rostam ila nasema ametoa maoni siyo kuwa anatuonea huruma au anaipenda nchi sana. Ana motive yake binafsi.
 
Kwanza ni MsamaRia sio MsamaLia.

Halafu Rostam ni mfanyabiashara na amezungumza kama mfanyabiashara sio msamaria mwema. Ni jambo la hovyo sana Wachina kuuza simu na kucheza kamari katika vijiji vya nchi hii.
Hahaaa, mara hii rostam kajigeuza kuwa msamalia mwema ma kusahau alikotoka? Labda kama tumgekuwa hatumjui!
 
Sasa mkuu Rostam anaona kitisho gani kwenye biashara yake. Rostam ni mfanyabiashara wa kimataifa, sidhani ni aina ya Mtu anayeogopa wawekezaji. Amekuwa na hisa nyingi Vodacom, tena wakati huo haikuwa inategemewa soko la mawasiliano litakuwa kubwa kama sasa na akafanikiwa sana na Vodacom ni kampuni inayolipa mishahara mizuri na huku ikiwa kampuni inayolipa kodi kubwa tena top three. Na baadaye wakaja akina Airtel na hawakumtisha

Ni mzawa ambaye amewekeza kandarasi kwenye migodi mikubwa kuliko mfanyabiashara yeyote Afrika Mashariki na kati na wafanyakazi wanaolipwa vizuri.

Kawekeza kwenye kiwanda kikubwa cha ngozi kinachotoa ajira na kusaidia sekta ya mifugo. Kiwanda kikubwa sana hapa Afrika Mashariki.

Amekuja na kuzikuta kampuni nyingine kwenye soko la gesi lakini amepambana na yupo hapo. Ana biashara kubwa Afrika kusini. Sasa kuna mwekezaji gani uchwara atakayemtisha!

Mimi naamini Rostam ni Mzalendo kuliko hata hao wengine wenye ngozi kama yangu ingawa naye ana mapungufu yake lakini pia kama tunataka mfanyabiashara malaika awe anaongea hayo mleteni kama yupo.
 
Haya ni maoni yako. Nayaheshimu lakini siafiki.
 
Serikali Ina wajibu wa kulinda walaji (raia) kupitia taasisi kama TBS.
Tatizo kubwa ni umasikini wa fikra ambapo matokeo yake ni vijana wanaohitimu kutumika katika taasisi za kuhalalisha bidhaa kutoka nje na kudhibiti ubunifu wa ndani badala ya kuboresha na kuendeleza.
 
Hayo madubwasha ni balaa haladu watu yanawapa addiction pesa za maskini zinakuwa drained na watunga sera wamening'iniza vitambi maofisini in short we are doomed
 
Nakubaliana nawe, michezo hii IWE ya serekali except cassino ziwe regulated na serikali,maana hizi hukaa katika specific area.
 
Hayo madubwasha ni balaa haladu watu yanawapa addiction pesa za maskini zinakuwa drained na watunga sera wamening'iniza vitambi maofisini in short we are doomed
Ziwe drained ziingie serikalini na si zitoroshwe nje!
Wasituzidi maarifa hawa ndugu zetu.
 
Anataka kukaba kila mradi uwe chini yake
Ni Gupta wa Tanzania. Hashikiki, anaogopwa na kuna 'Mtu' ameshawekwa Mfukoni mwake halafu anaingia Magogoni na Chamwino muda wowote akijisikia.
 
rostam ni mwizi kuliko matajiri wengine angalia clip ya marehemu R mengi walipokuwa wanagombana na rostam
 
Huyu hapa. Akemea wawekezaji uchwara

View attachment 2396908
Wachina kuwekeza kumbi za starehe vijijini sio kufilisi wanavijiji. Watu wanaamia mijini kufuata huduma hizo, kwa nini wasipelekewe huko? Halafu, kuingia kwenye ukumbi wa starehe ni ridhaa ya mtu mwenyewe - alazimishwi.
Uchwara unatokea wapi wakati hao Wachina ni wabunifu na leseni wamepewa?
Hapo ukute anataka waondolewe akafanye yeye hiyo biashara!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…