Rostam Azizi to build 200 million LPG Facility in Kenya with Our money may be!

Ni kama utani vile, lakini hakuna cha utani hapa.
Tanzania yetu ndivyo ilivyo hii!
 
Hicho kitu cha kuchukia matajiri kitawatafuna sana watanzania. Kwa taarifa yako Rostam Aziz amezaliwa amekuta Baba yake mzazi ndiye Biggest exporter wa hides and skin kutoka Tanzania kwenda nje.

Kwa sasa anazo kandarasi kuanzia South Sudan, Kenya, Ethiopia na South Africa ambazo alishinda kipindi cha 2016-18 wakati anaishi nje ya Tanzania kipindi Magufuli amepata Urais.
 
Ni kama utani vile, lakini hakuna cha utani hapa.
Tanzania yetu ndivyo ilivyo hii!
Sio utani ndugu....Riz 1 atakuwa rais wa nchi hii trust me. Ni swala la mda tu,mtandao unasukwa kabsa.....nimepata taarifa kutoka chanzo cha kuaminika mtu wa karibu kabisa na Beno Malisa mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye kawekwa pale kwa kimemo na Riz 1. Mtandao umeshaanza kusukwa
 
Kwa ninavyojua na nilivyomsikia Rostam mwenyewe anaongea ni kuwa;

Taifa gas wanataka kulifikia soko lote la gas ya kupikia (LPG) afrika. Sasa hv wapo baadhi ya nchi kama Rwanda Burundi tanzania nk. Yaani taifa gas itakuwa ndio kampuni ya kwanza yenye makao makuu DsM ikihudumu kwenye nchi zote za afrika kuanzia mijini hadi vijijini. Na sio kwamba Taifa gas hawana plant Tz Tyr wana plant Tanzania (Kigamboni) yenye uwezo wa kujaza tani elf 7, hiyo ya kenya itakuwa mara nne kwa kuwa na uwezo wa kujaza na kudistribute tani elf 30. Lkn bado Tanzania inabakia kuwa na refueling network facilities 25 za taifa gas wakati kenya wamepanga kuanza na 10 tu.

Swali la kwa nini hajajenga hiyo plant Tanzania nishakueleza hapo juu tyr kuna plant ya taifa gas Tanzania tofauti tu ni kwamba ya Kenya itakuwa kubwa zaidi mara nne na hii ni kulingana na ukubwa wa soko analotegemea kulihudumia kwa plant husika pamoja na sababu nyinginezo.

Kutaka kufananisha/Kuhusisha jambo hili na EPA ni kwa sababu hujui kwa undani mojawapo ya majambo haya au yote kwa pamoja. Unauliza Rostam kapata wapi pesa!? Mtu aliyekuwa bilionea wa dola tangu 2012 unauliza kapata wapi dola milioni mia 2!? Mwaka 2014 tu jamaa aliuza share zake 17% za voda kwa 240 usd. Juzi hapo 2019 tena tukasikia kauza 26% kwa zaidi ya 200 usd. Kaja akazinunua tigo na zantek kwa pamoja.

Hivi kumbe mtu anaweza kukopa pesa na mdhamini akawa ni serikali kisha akishindwa kulipa Serikali ndio italipa!? Mbn hatukuambiana huu utaratibu ili na mimi nikakope kwa udhamini wa serikali jamani nishindwe kulipa waje wanilipie!

Tutafute pesa jamani.
 
Unaweza kukuta kabisa amechukiwa mkopo na aliyedhamini huo mkopo ni sisi nikimaanisha Serikali ya Tanzania maana yake ni kwamba akishindwa kulipa deni mdaiwa ni sisi lkn bado kaenda kujengea Kenya???
Hii kitu inaweza kabisa kuwa kweli kwani watawala wetu wakati mwingine utafikiri sio wa Tz
 
Riz 1! Mh! ni sawa na kiwiliwili bila kichwa wallah!
 
Duuu! Kudadeki!!!!!!! Ndo maana mdogo wake hakufungwa jela licha ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
 
Hayo matoto mambumbu,yamejaa udaku vichwani
 
Wakati anamiliki voda hamkuhoji pesa kapata wapi ila kwa kuwa kawekeza kenya ndio mnahoji, huyu jamaa ame invest nchi nyingi sana serikali inatakiwa iwe karibu na watu kama hawa na kuwashauri wa invest nchini, wapewe mazingira mazuri utaona nchi itakavyo kua na maendeleo ya viwanda
 
Kwenye Ile ziara marekani Rostam alikuwa anasaini Nini?
 
Ile nchi ambayo haina akiba ya kutosha ya dola za kimarekani ni ipi mkuu

Kuna uhusiano na uwekezaji huu wa bilionea "Rostam"?
 
Ikiwa Kenya na nchi nyingine zimewekeza $billions hapa Tz inakuwaje unahojihoji $200million alizowekeza Mtanzania Rostam Aziz huko Kenya? Una habari Safaricom ya Kenya inawekeza $3 billion huko Ethiopia?
Unachotakiwa kufanya ni kumpongeza R.A.!!!
 
Reactions: Ame
Hii hali ya kuhisi watu ni wezi kwa watanzania sijui ni genetically embedded? Kila mara mtanzania akisikia mtanzania mwenzake kapata pesa anawaza wizi kwakua wengi wamezoea kuiba kwenye public coffers na hawajui kuzalisha au ku create wealth....Hii mentality ya kimasikini inahitaji uponyaji
 
Badala ya kupunguza loopholes za kuiba public funds watu wapo busy kupunguzia watu kasi yao ya maendeleo...For God sake mtu huyu hana hata cheo kimoja kwenye public office, kama ni mwizi je ni yeye au hao wenye stake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…