Rostam Maelezo yake yamenyooka na yanaeleweka. Huenda Mtangazaji ndiye ameshindwa kumhoji

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
 
Kingine nimegundua hauwezi ukawa tajiri pasipo kuwa smart kichwani. Jamaa yupo smart sana. Anapangilia hoja zake bila papara ila Tido kwa kiasi fulani ametuangusha.
 
polepole apuuzwe anakitu cha roho mbaya kiko rohoni kwake kunakitu anaona hatendewi haki pengine kanyima madaraka makubwa aliyokuwa anataka hivyo roho yake imejikunja sana

Huenda kuna jambo analijua ambalo wengine hatulijui.
Tuhuma kwa Rostam kuhusu Mtandao, na kumiliki migodi naona Rostam kaijibu kiufasaha sana.

Tunamsubiri Polepole apangue hoja za Rostam.
 
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Mtajitekenya sana mwaka huu 🤣🤣

Kuangalia ule upuuzi bora niangalie #Movie za mkojani nitapata kitu ndani yake .

Simply to say ,rudini studio ,mzigo umegoma ule, watanzania siyo mafala.
 
Kingine nimegundua hauwezi ukawa tajiri pasipo kuwa smart kichwani. Jamaa yupo smart sana. Anapangilia hoja zake bila papara ila Tido kwa kiasi fulani ametuangusha.

Tido na uzoefu wake nilitegemea naye awe na utulivu na aendeshe mahojiano kwa namna ya kumbana Rostam ambaye mahojiano hayo yapo kwaajili ya yeye kujibu tuhuma. So kumuacha mtu ajitetee muda mrefu bila kumpa maswali magumu na tata ni kumpa nafasi jamaa awe shujaa
 
Mtajitekenya sana mwaka huu 🤣🤣

Kuangalia ule upuuzi bora niangalie #Movie za mkojani nitapata kitu ndani yake .

Simply to say ,rudini studio ,mzigo umegoma ule, watanzania siyo mafala.

Mkuu hapa tunajadili mahojiano yalivyokuwa.
Unaweza kushiriki hapa kwa kuonyesha udhaifu hasa wa mtuhumiwa katika majibu yake ambayo anajitetea.

Sisi wengine ni Watu huru, hatuko limited katika kupokea taarifa.
 
Nguvu mnazotumia chawa wa CCm na buku saba zenu
IMG_2469.jpeg
 
RA yuko mbele ya muda. Ni wale wenye wivu tu ndiyo watambeza. Mimi siwezi kumdharau Mtanzania anaye toa ajira za moja kwa moja 7,000 kwa Watanzania. Anatengeneza bidhaa na huduma kwa Watnzania na analipa kodi kwa TRA.

Williamson Diamond ipo tangu miaka ya 1940, inawezekana walioianzisha hawapo duniani, RA amenunua Hisa za Wamiliki wengine, kuna kosa gani? Serikali ilipewa nafasi (first right) ya kununua, haikuweza. Tatizo la RA kununua ni lipi. Makaa ya mawe na chuma yamekuwepo Karne na karne, mimi na ndugu zangu tupo pale jirani, hakuna hata mmoja aliweza kuchimba na kuanzisha hata kiwanda kidogo cha kufua majembe kama wazee wa zamani. Tembo na nyati wamekuwepo; akina Tip Tipp walisomba pembe za tembo wakaenda nazo; sisi tunalalamika wanaharibu mazao. Tumeshindwa hata kuanzisha biashara za utalii. Wengine wakimudu kufanya sisi tunawaita mafisadi. Viongozi tunawachagua miongoni mwetu wenyewe, kesho tunalalamika kuwa ni Rostam. Hii si sawa, Polepole APUUZWE
 
Nguvu mnazotumia chawa wa CCm na buku saba zenu View attachment 3466675

Wewe unafikiri kila mtu ni mwanasiasa hilo ndilo tatizo lilipo.

Kwa hiyo wewe ukiambiwa Tundu Lisu ni Mhaini utaichukua hiyo taarifa kama ilivyo bila kusikiliza pande mbili?

Kama tunavyowatendea Haki Chadema ndivyo hivyo hivyo kwa upande wa ccm.
 
Nlitamani mwandishi angemuuliza namna mchakato wa kununua hizo share za makaa huko australia kama ulikuwa wa wazi kwamba yeyote mwenye mtaji angeweza kununua?

VIlevile kwenye ununuzi wa hizo hisa za mgodi wa mwadui,palikuwa na uwazi huko Londoni??
 
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Bado siku Moja tu kutimia kwa Septemba 7. Tunakusubiri kwa hamu!
 
Umekosa kazi sio...
Ndo maana mlitukanwa..
Fanya kazi achana na mafisadi
 
RA yuko mbele ya muda. Ni wale wenye wivu tu ndiyo watambeza. Mimi siwezi kumdharau Mtanzania anaye toa ajira za moja kwa moja 7,000 kwa Watanzania. Anatengeneza bidhaa na huduma kwa Watnzania na analipa kodi kwa TRA.
Kutoa Ajira isiwe kichaka cha kuficha uovu wa mtu.

Mimi hoja yangu ni kuwa Tuhuma alizopewa Rostam na alivyojieleza amejaribu kujibu kwa ufasaha kabisa kama utasikiliza bila kuwa na upande

Williamson Diamond ipo tangu miaka ya 1940, inawezekana walioianzisha hawapo duniani, RA amenunua Hisa za Wamiliki wengine, kuna kosa gani? Serikali ilipewa nafasi (first right) ya kununua, haikuweza. Tatizo la RA kununua ni lipi. Makaa ya mawe na chuma yamekuwepo Karne na karne, mimi na ndugu zangu tupo pale jirani, hakuna hata mmoja aliweza kuchimba na kuanzisha hata kiwanda kidogo cha kufua majembe kama wazee wa zamani. Tembo na nyati wamekuwepo; akina Tip Tipp walisomba pembe za tembo wakaenda nazo; sisi tunalalamika wanaharibu mazao. Tumeshindwa hata kuanzisha biashara za utalii. Wengine wakimudu kufanya sisi tunawaita mafisadi. Viongozi tunawachagua miongoni mwetu wenyewe, kesho tunalalamika kuwa ni Rostam. Hii si sawa, Polepole APUUZWE

Sio kosa kwa Mtanzania kufanya biashara ndani ya taifa lake.

Rostam amejaribu kuonyesha kuwa hata hapo Ruvuma kuna migodi zaidi ya 16 ambayo sio yake. Na wakwake bado hajaanza kuzalisha, kufikia hapo nimepata maswali mengi sana. Hasa kwa wanaomtuhumu.
 
Back
Top Bottom