Rostam Maelezo yake yamenyooka na yanaeleweka. Huenda Mtangazaji ndiye ameshindwa kumhoji

Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Akuna mzawa mwenye asili ya kihindi au tofauti na bara la africa nenda south africa utaona wazungu wanagombana na wa south ,
Iko hivi mtoto usiye mzaa sio wako siku akionyeshwa wazazi wake ataondoka na kuwajali kwa kuwapa kila kitu wewe utaishia kusema ni mwanao ndicho rostam anacho kifanya watanzania hatuwezi jivunia yeye ni bora wale wawekezaji wanao kuja tunajua direct siku wakizingia tuna wafukuza ila huyu anataondoka kwenda uko kwao na atawafaidisha watu wawo
 
Maelezo ya rostam yamenyooka, shida Iko kwa watawala...
 
Umekosa kazi sio...
Ndo maana mlitukanwa..
Fanya kazi achana na mafisadi

Huu ni mjadala huru. Hongera kwa mchango wako.

Kwa nini mtanzania mwenzako akifanikiwa unamuita Fisadi, muuza madawa, mganga wa kienyeji, Freemason n.k.?

Kwa nini huamini kwamba kuna njia halali?

Tukirudi kwa Rostam, je hoja yake ipi amepotosha?
 
Akuna mzawa mwenye asili ya kihindi au tofauti na bara la africa nenda south africa utaona wazungu wanagombana na wa south ,
Iko hivi mtoto usiye mzaa sio wako siku akionyeshwa wazazi wake ataondoka na kuwajali kwa kuwapa kila kitu wewe utaishia kusema ni mwanao ndicho rostam anacho kifanya watanzania hatuwezi jivunia yeye ni bora wale wawekezaji wanao kuja tunajua direct siku wakizingia tuna wafukuza ila huyu anataondoka kwenda uko kwao na atawafaidisha watu wawo

Huu ni mtazamo wa Watanzania wengi.

Kwa nini unaamini hivyo?
Kwenye ukoo wenu hamjachangamana na jamii zingine?
Mfano Dadaako au kakaako akioa mhindi au muarabu. Hao watoto sio Watanzania?

Huoni kama huo ni ubaguzi?
 
Nlitamani mwandishi angemuuliza namna mchakato wa kununua hizo share za makaa huko australia kama ulikuwa wa wazi kwamba yeyote mwenye mtaji angeweza kununua?

VIlevile kwenye ununuzi wa hizo hisa za mgodi wa mwadui,palikuwa na uwazi huko Londoni??
Unaijua vizuri London Stock Exchange? Au unabwata?
 
CCM wamejimilikisha mgodi wa MAKAA ya MAWE tunataka document
 
Sasa kwa Mwandishi Mkongwe na ambaye tuna Dhani ni mweredi, kwa nini hakumhoji Rostam au kum Challenge katika maelezo yake kama wanavyofanya waandishi wengine tena wachanga kama akina Chief Odemba na Aloyce Nyanda??

Kwa Nini Todo alikuwa kama vile kilainishi katika maelezo ya Rostam?

Sasa kosa pale ni la Tido mhando Sio Rostam.

Mimi nimechukua maelezo ya Rostam kama nilivyochukua ya Polepole na tuhuma anazopewa Rostam.
Majibu ya Rostam yamenyooka na yanaeleweka.
 
Matajiri wa ndani wapo wengi si yeye tu kwanini yeye ndio mara nyingi anaonekana mpigaji hasa kwa kujiweka karibu na serikali

Mzee mengi alikuwa mtanzania na aliwahi kumkosoa huyu rostam mbna kina bakhresa wapo kina mo wapo japo wanasemwa kwa ukiritimba lakni si kwa kiwango chake

Ukiwa mwadilifu si rahisi kuwa suspicious kila mara na mambo yako
 
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Je vipi ameelezea zile shehena ya silaha walizokamatwa nazo na kwanini zile habari na picha siku hizi hata ukizi google uwezi kuziona wala kuzipata mitandaoni ...ninani kazifuta
 
Tatizo MIKATABA ya wawekezaji Nchi hii huwa ya kificho ndiyo maana watu wanabaki na maswaki mengi.ukiangakia makaa ya mawe tanavyosombwa Tani na matani kupelekwa ulaya na faida kidogo tunayopata lazima uhoni huu uwekezaji
 
polepole apuuzwe anakitu cha roho mbaya kiko rohoni kwake kunakitu anaona hatendewi haki pengine kanyima madaraka makubwa aliyokuwa anataka hivyo roho yake imejikunja sana
Ushajiuliza kwa nini kule UTV alikula kona kuhojiwa LIVE?
 
Ukweli ni kwamba wabantu tumelala sana. Pia hata uwezo wa kuchungulia fursa ni mdogo sana. Sana sana tumezidiwa na Majungu na Roho mbaya iliyopitiliza kwa wale waliofanikiwa.

Badala ya kutafuta namna wamefanikiwa tunaanza kuwa wachawi kwao. Ninaapa sitakuja kuwa na chuki na aliefanikiwa bali nitatafuta mbinu alizotumia.

Unakuta mtu anamsema na kumbagaza mtu eti amefanikiwa kwa wizi. Yeye mwenyewe unamwambia kama ni rahisi kuiba ili uwe tajiri nawe iba. Anabaki kushangaa.

Si dhambi kutafuta connection ili kufanikiwa. Kama Rostam alivyosema kuwa kwenye mtandao ili ufanikishe jambo flani si dhambi. Tuache chuki tufanye kazi.

Tunakesha kwenye mitandao kutukana afu ikifika jioni tunaanza kulia njaa. Tubadilike kwakweli tusisaidie watu kusukuma ajenda zao binafsi.

Kabla ya kumtukana Rostam jiulize yeye kaajiri watu 7000. Wewe umeajiri wangapi?

Jamaa kichwani yupo smart kwelikweli. Changamoto anazopitia ni kwasababu yupo kwenye jamii isiyopenda kutafuta ukweli bali inaongozwa na chuki.
 
Huenda kuna jambo analijua ambalo wengine hatulijui.
Tuhuma kwa Rostam kuhusu Mtandao, na kumiliki migodi naona Rostam kaijibu kiufasaha sana.

Tunamsubiri Polepole apangue hoja za Rostam.
Hakuna alichojibu hapo. Kama mnabishi mpelekeni kwa chief Odemba

Muda mwingine punguzeni mahaba kwa mafisadi. Ebu niambie ni swali gani gumu aliloulizwa?

Hayo maswali yote aliyoulizwa wameyadisscus kwanza na kuyaweka kwenye mlolongo sahihi.

Tindo alikuwa amepewa ukomo wa kuuliza maswali magumu. Na hii ilionekana wazi walikuwa kama ana hofu kubwa
Zaidi ya yote mwambieni Rostam ni muhoji mimi hapa kama atatoboa.
 
Tido na uzoefu wake nilitegemea naye awe na utulivu na aendeshe mahojiano kwa namna ya kumbana Rostam ambaye mahojiano hayo yapo kwaajili ya yeye kujibu tuhuma. So kumuacha mtu ajitetee muda mrefu bila kumpa maswali magumu na tata ni kumpa nafasi jamaa awe shujaa
Kumbana kivipi?!..hoja dhidi ya rostam ni migodi na mtandao,kaulizwa na kajibu
Todo alimhoji idd Amin 2003/4/5 sijumbuki vizuri,napo utadai hakumbana..kisa mahojiano hayakwenda utakavyo
 
Huu ni mtazamo wa Watanzania wengi.

Kwa nini unaamini hivyo?
Kwenye ukoo wenu hamjachangamana na jamii zingine?
Mfano Dadaako au kakaako akioa mhindi au muarabu. Hao watoto sio Watanzania?

Huoni kama huo ni ubaguzi?
Jibu hoja yangu, ukoo wa huyu RA uko wapi ? Wanapitia changa moto sisi tunazo pitia?
kuna kipande anasema "tangu anunue mgodi wa makaa bado awaja maliza kukabiziana document kwahiyo bado ajaanza kuzalisha "icho kitu una akiamini?
 
Back
Top Bottom