Rostam Maelezo yake yamenyooka na yanaeleweka. Huenda Mtangazaji ndiye ameshindwa kumhoji

Rostam Maelezo yake yamenyooka na yanaeleweka. Huenda Mtangazaji ndiye ameshindwa kumhoji

Kuna watu ninaamini mnampenda na mnamheshimu sana Rostam Aziz kiukweli na nyie sio wale wa buku 7 na ni haki yenu kabisa na mimi siwezi kuingilia maamuzi yenu. Mwisho wa siku hili jukwaa ni sehemu ya kupromote na kulinda free speech na free speech includes mawazo ambayo hayaendani na ya kwako.

Experience yangu na wanamtandao ni mbaya sana. They are the epitome of evil in my humble opinion. Mimi ni mtu mmoja tu na hayo ndio mawazo yangu. Vitu nilivyopitia kwasababu ya figusi zao vilikuwa vigumu sana lakini kama watu wengi wanavyopenda kusema including hapa JF, labda mambo hayo ndio yamenipa ujasiri nilionao.

Mimi nimeishi na ukweli wangu kwa miaka karibia 30, na nitabiki nao mpaka mwisho wa miasha yangu. Nimedeal na shida zangu na wanamtandao in private maisha yangu yote. Nilijitokeza kuongea only once mwaka jana na sasa hivi wanamtandao wamekuwa topic nchini ndio maana wanaongelewa kila mahali lakini nimeishi na fitna zao maisha yangu yote.

Una uhuru wakumpenda na kumheshimu mtu yoyote unayechagua kumpa upendo na heshima yako lakini experience yangu na hawa watu is never going to change. Mawazo yangu kuhusu hawa watu hayatabadilika and that is okay, hauwezi kupendwa na kila mtu.
Uvivu wa kufanya kazi na kuendekeza starehe tu ndiyo unakutesa
 
Kasema kauziwa na kampuni binafsi. Hajauziwa na serikali. Kwamba alinunua share za kampuni binafsi.

Sasa Polepole tunategemea akija aje na hoja za moto kupangua maelezo ya Rostam
Ameonyesha documents zozote au maneno mtupu?
Kama hajaonyesha hizo documents unapata wapa uhalali wa kusema jamaa kaeleweka?
 
Ndio maana hawakwenda live, kwa sababu kuna cut ✂️ nyingi sana, mengi yamekatwa kwa faida ya upande mmoja.

Lakini kushindwa kwa tido kuhoji maswali magumu inaonekana hii intavyuu ilikua ya kujitetea na kujisafisha zaidi kuliko kukutana na maswali fikirishi.

Suala la migodi, Rost kasema yeye alinunua kwa mtu wa nje, kwamba kuna mtu aliuziwa na serekali, kisha yeye akaenda kuununua kwa huyo mtu(hapo napo hujiongezi) wao kina rost huwa ndio madalali wa michongo hii kisha huzunguka na kwenda kununua ref kipindi cha mgogoro kuhusu vitalu vya gesi mpaka mzee mengi akawa anagombana na profesa muhongo.

KUMBU KUMBU SOMA HAPA
- Prof. Muhongo: Alieleza kuwa hakuna kampuni ya Kitanzania yenye uwezo wa kuwekeza katika sekta ya gesi, akiwatuhumu baadhi ya wafanyabiashara wa ndani kwa ubinafsi na kutokuwa na uzalendo. Alidai kuwa baadhi yao walikuwa wakitaka kuwa madalali katika uuzaji wa vitalu vya gesi.

Mkuu haya mambo mimi na wewe hatuyajui vyema zaidi ya kuyasikia tuu mtandaoni na kwenye media.

Swali ambalo niliona Tido kauliza lenye nguvu ni lile alilomuuliza, Rostam anawezaje kuwa na kujenga ukaribu na viongozi wakuu ingawaje Rostam alikuwa akilikwepa
 
Ameonyesha documents zozote au maneno mtupu?
Kama hajaonyesha hizo documents unapata wapa uhalali wa kusema jamaa kaeleweka?

Mkuu tunasubiri aliyemtuhumu yeye ndiye atakuwa na kazi ya kuthibitisha maelezo yake kuliko mtuhumiwa (Rostam) ila mpaka sasa maelezo ya Rostam yamenyooka kwa asilimia kubwa kama ni mapungufu yapo sehemu chache sana.
 
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Wizi huwa ajiseminkuwa ndio nimeiba mwizi uwa anajiteteasiku zote hajaiba wenye kuweza kuthibitisha hilo ni mamlaka husika ambao pia kwa sasa ninkama hawana meno yeyote.
 
Tido kashindwa kumuuliza maswali yaliyotakiwa.

Siasa za ccm ni kama vile China na Vietnam hazina mitandao ndani ya chama. Chama hushika hataki.

Siasa za Kimagharibi na demokrasia zao vyama havishiki hatamu. Anayekuja anakuwa na sera zake na chama hufuata. Kwahiyo makundi ni kuchonganisha sera.
 
Tido na uzoefu wake nilitegemea naye awe na utulivu na aendeshe mahojiano kwa namna ya kumbana Rostam ambaye mahojiano hayo yapo kwaajili ya yeye kujibu tuhuma. So kumuacha mtu ajitetee muda mrefu bila kumpa maswali magumu na tata ni kumpa nafasi jamaa awe shujaa
Mhando, ama hakujianaa kwa mahojiano au anafuata script aliyoelekezwa kufuata.
 
Habari za Sabato!

Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.

Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.

Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi

Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.

Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.

Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.

Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.

Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.

Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.

Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.

Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.

Ni hayo tuu.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam
Wewe binafsi unaamini nini? Maana akija Polepole utahamia tena kwa Polepole, akirudi tena Rostam utahamia tena kwa Rostam…yan unahamahama kama sheikh anayefakamia ubwabwa; Kama Sheikh wa Chauma
 
Usitathmini jambo kwa base nyepesi km hizo ulizotumia na kusema rostam kajieleza kwa ufasaha bila kujali anayoeleza yana ukweli..? Kwa ufupi nikosoe utambulisho wake..kuonyesha si kweli anachosema..
1. Hospitali ya ndala anayoitaja amezaliwa, iko umbali wa takriban km 40 kutoka mwisi anapodai wazazi wake walikuwa wakiishi, lkn jirani kabisa na mwisi kuna hospital ya nkinga, umbali wake ni takriban km 10..zama hizo za kuzaliwa rostam hospital ya nkinga ilikuwa bora zaidi ya hospital ya ndala, zote ni hospital za misheni..ni ajabu wazaz wa rostam kuamua akazaliwe ndala badala ya nkinga, na kumbuka zama hizo barabara ilikuwa ni changamoto kubwa..ni rahis zaid kufika nkinga kuliko ndala..inawezekana anataja ndala sabb hakuna records tofauti na nkinga ambako pana records toka hospital ilipoanza miaka ya 30, hivyo ukweli wa kuzaliwa kwake una mashaka.
2. Pili, anasema waasisi wa mageuzi mzee mapalala na kaselabantu wanatoka kijiji cha ussongo/Izimba jirani na asili yake mwisi umbali wa km 5, si kweli umbali sahihi kati ya ussongo na mwisi ni takriban km 28, sidhani ni rahisi kwa mtu aliyekuwa mwakilishi wa maeneo haya kwa miaka 18 kusahau umbali wa maeneo maarufu aliyoishi..
Kwa utangulizi huu wa rostam kutoa taarifa tata zenye mashaka, unamuamini vipi hayo anayosema ya biashara zake na kuhusishwa na ununuzi wa hisa za petra huko mwadui na za makaa ya mawe kuwa ni za kweli?
3. Unamsema tido kushindwa kuuliza kulingana na vile inatarajiwa, kwa nini hufikiri kwamba rostam ndie alimwandalia maswali ya kumuuliza..? hasa ukijua kwamba rostam alikuwa ofisin kwake na tido alikuwa mgeni wake..
4. Rostam mambo yake ya biashara yana utata mwingi, kwa hadhi hiyo anayopewa kwq biashara zake unatarajia awe na wasaidiz wengi tena hodari kbs..kumsaidia kutoa maelezo pale biashara zake zinapotajwa, lkn sivyo hivyo, kila biashara zake zikitajwa lazima yeye ndie aje kutoa maelezo..mbona huoni hilo kwa bakhresa au wengine? Inakuwa km biashara zake ni za mfukoni..anazijua yeye tu! Kwa hali km hii lazima pawepo shida kubwa kati yake na biashara anazomiliki!
Hospitali ya Nkinga Imeanza Kazi Mwaka Gani Mkuu? Na Hospitali ya Ndala Imeanza Mwaka Gani? Mimi Naweza Kukuthibitishia Physically Kuwa Rostam ni Mkazi wa Maeneo Yale, Mimi ni Mkazi wa Nkinga, Wewe ni Mkazi wa Maeneo Gani Mkuu?
 
unajijua kiundani na kujitambua Kwa kina na kiuhalisia ya kwamba mwenyewe ulivyo huna tofauti na Tido anayetetea kitumbua chake.

Kaniki haisafishiki,chukua chako sepa...
 
Matajiri wanajua kuigiza kutumia media!
Kuwa makini!
 
nimesikiliza hotuba yote ya papa, nikiri kusema kuwa maelezo yote aliyotoa ni laini sana na hoja zake ni nyepesi sana zikiwa very general, hakuna la maana alilojibu zaidi ya kufuata script aliyomwandalia ndugu Mwandishi,
itoshe kusema kua mtu huyu ni mpigaji, nashangaa sana ndugu mwandishi wa makala hii kumsifia, sijui ndugu taikon amelishwa nini leo, ni aibu na fedheha kusifia maelezo yasiyo na facts, nachelea kusema kua kila hoja aliyosema kijana slow slow ni kweli isipokua mjibu hoja ameshindwa kujitetea, tunayoyajua ni mengi kumhusu yeye basi tu tunamwangalia na kusema hiiiiii bagosha,
 
Back
Top Bottom