Habari za Sabato!
Nimemsikia Rostam kwa umakini, amejieleza vizuri sana na yapo mambo kupitia Press yake yameniongezea kitu hasa katika utafutaji na biashara.
Kuhusu tuhuma zake, zote alizoulizwa amejibu kiufasaha kabisa na maelezo yake yamenyook na yenye kueleweka.
Tatizo nililoliona lipo kwa anayemhoji,
Tido Mhando ndiye ameonyesha upungufu mkubwa katika interview hiyo.
Ni kama anamhoji mtu kwa tahadhari kubwa, akiwa na hofu fulani na mara nyingi amekuwa upande wa Rostam kumkubalia kila hoja yake bila kumpa challenge kubwa.
Hoja ya Makaa ya Mawe na mgodi wa Almasi amejibu vizuri sana na kutupa uelewa mpta Wasikilizaji na watazamaji, ambao kimsingi tunasikia mambo haya kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii huku tukiwa katikati hatujui ukweli ni upi
Rostam amefanya vizuri kujitokeza na kujitetea na kujibu madai yanayoelekezwa kwake. Ili kuweka Mambo sawa.
Kitu kingine ambacho nimekigundua katika mahojiano haya ni kuwa, ukisoma Saikolojia ya Rostam kwa ndani kabisa anajaribu kujieleza na kutaka watanzania wamuone Kama mtanzania mwenzao.
Jambo hili kupitia matamshi yake hasa akijaribu kueleza uasili wake, kwamba yeye ni Mtanzania.
Saikolojia ya Watanzania wengi hasa wenye asili ya kibantu, huamini wao ndio Watanzania halisi na wanahaki kuliko Watanzania wa jamii zenye asili zingine kama Watanzania wenye asili ya uhindi, uarabu, usomali, na jamii zingine.
Ni katika mtazamo huohuo, ndio maana Rostam na watu wenye muonekano kama wake katika masimulizi yao lazima jambo hilo walitilie mkazo wa nguvu huu ni tofauti na wabantu wengine.
Watanzania wengi hawaamini Mtu kama Rostam au Mo Dewji na watu aina hiyo ni Watanzania wenzao ile yenyewe yenyewe. Ingawaje hili halisemwi waziwazi.
Na hii inatoa kazi kwa serikali kutafuta namna ya kuwaunganisha watanzania wote kuwa kitu kimoja na kuondoa hizo fikra za kikabila au races.
Fikra hizo hujitokeza zaidi katika masuala ya siasa na uchumi.
Tunaona hata kwenye uchaguzi katika ubunge kuna kauli kama huyu sio mzawa wa hapa, au huyu sio kabila la hapa, huo wote ni ukabila na ubaguzi ambao serikali inapaswa iuchukue kama homework.
Kwa hoja za Rostam, nasubiri Hoja za Polepole zijibu kwa nguvu na uthibitisho.
Hofu yangu ni kwamba, tusije unda mitazamo na falsafa za kuchukia wenye utajiri na wenye Mali kwa kutumia propaganda ambazo sio kweli.
Zaidi, serikali isijeikaungana na matajiri na wenye mali kukandamiza Maskini na wanyonge. Au tuseme Matajiri wasijeiteka serikali kukandamiza Maskini.
Kila mtu abaki kwenye nafasi yake, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Na sio mtu mmoja kula kwa kamba za wengine au kupunguza kamba za wengine kujinufaisha.
Ni hayo tuu.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar wa salaam