Royal Tour! kulikoni wagharimiaji hawatajwi hadharani? Tunaishia kuambiwa ni Watu Binafsi

Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
Alikuwepo Magufuli hukuuliza, Sasa anaulizwa aliyepo wewe unataka aulizwe marehemu!
Atakusumbua Sana Magufuli.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Imegharamiwa na pesa za watanzania, hii ni kutoka kwenye kinywa cha Rais.
 
Mbona hatukuona tangazo la kuomba mchango? Pesa zilichangwa kupitia akaunti gani ya serikali? Je CAG atakuwa na access ya kukagua matumizi ya akaunti hiyo!
Pia watuambie sheria ya utumishi wa umma insemaje kuhusu Rais kupokea msaada na kuwaficha watoaji?
 
Aisee,Watanzania,hypocrites kabisa.Hivi seriously huoni kwamba Watanzania wana haki ya kulijua hili.Je kama Rais kaingia kwenye uhusiano usiofaa na watu wasiofaa kwa maslahi mapana ya taifa letu.....!!No,tunahitaji kujua,Tanzanians need to know.
Na sheria za utumishi wa umma pia haziruhusu Rais kupokea zawadi bila kutaja mtoaji na malengo yake?
 
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
Naona bado mnapambana na chato. Atleast kule chato kuna uwanja unaonekana, utaweza kutumiwa hata na jeshi ukikosa kazi kabisa wenyeji wa chato watz wenzetu wataanika mpunga, watajifunzia driving etc. Sasa mtujibu iyo Royal tour nani ameifadhili na malipo gani atadai. Na kitu gani tangible tutapata hapo. Tunajua idadi ya watalii post covid after covid. Tutachunguza aftr royal tour.
Patamu hapo, mtapambana na mzimu hadi mkome.
 
watu wanataka uthibitisho na uwazi

inawezekana hao wafadhili wenye mapenzi mema kwa Nchi yao wamechangia jumla ya billion 9 na 7 zikapelekwa kwa 'Rambo' na zingine zikaingia kwny mifuko binafsi

lakini kubwa zaid kuna taratibu za kisheria za kukusanya, kuratibu, kutumia na ku report fedha zote za wenye mapenzi mema na nchi zilifuatwa?

hata JPM nae alikuwa akikosea kukopa kwa siri na kutudanganya ni makusanyo ya ndani

usichukulie kila anaemkosoa Samia ni mfuasi wa JPM

wa Tz wengi sana si wafuasi wa wanasiasa na wana haki ya kuhoji
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
 
Unao uthibitisho gani kwamba ni hela za watu binafsi?

Kwani fedha za ujenzi wa uwanja wa Chato ni siri?

Wewe ni kilaza usojitambua!
Team msoga uyo toka enzi za chuma, sasa wanapambana na mzimu wake.
 
Royal tour ni upigaji tu hamna lolote.Kama wana ujasiri watupe cost and benefit analysis,vinginevyo wasituchoshe Watanzania na usanii wao.
 
Na sheria za utumishi wa umma pia haziruhusu Rais kupokea zawadi bila kutaja mtoaji na malengo yake?
Na yeye ni mtumishi wa umma!Msimamizi mkuu wa sheria anakuwa wa kwanza kuvunja sheria,patamu hapo.Yale yale ya Boris Johnson kufanya drinking party No.10 Downing Street bila observation ya Covid rules,ambazo yeye mwenyewe alisimamia kuzitunga na hivyo alipaswa kuhakikisha kwamba zinakuwa observed.Vyombo vyetu vya sheria vinasemaje?
 
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?
Wewe fungua uzi uliza hilo swali lako usimpangie mleta mada aulize swali ambalo halipo kichwani mwake.

Huyu Bi Tozo Bin Maushungi ni corrupt kama walivyo predecessors wake na ccm wote kwa ujumla.

Hii nchi inahitaji mapinduzi ya kijeshi, njia za kiraia zimeshaprove failure
 
Kabisaaa!
 
Ni vizuri ukajikita kuuliza ni kampuni gani ilijenga uwanja wa ndege Chato maana kule ndo pesa za walipa kodi zilitumika!

Unauliza hela za watu binafsi walizotoa kwa mapenzi yao kwa Taifa Lao ili iweje?

Wewe KICHWA MAJI elewa swali la mleta mada kabla ya kukurupuka kujibu,

ni kina nani hao watu binafsi waliotoa hizo pesa kwa mapenzi yao kwa Taifa?

Je kuna ubaya wowote tukiambiwa majina ya WAZALENDO hao kwa Taifa waliojitolea pesa zao binafsi zaidi ya tsh billion saba?
 
Uko humu 24/7 kuvizia tu Rais Samia kafanya nini ili ukosoe. Baada ya kuhisi kakaa 2 weeks kwa fedha ya wahisani watanzania, na si kwa fedha ya Serikali kama MLIVYOKUWA MNABWABWAJA, sasa voicer unataka kujua majina ya wachangaji.

Ulivyo POPOMA ukipewa majina yao utataka kujua majina wa wake zao au waume zao.

Tafuteni shughuli za maana za kuwaingizia hela haya MAUJINGA yamepitwa na wakati baada ya kumfukia mungu wenu pale Chato
 
Filamu ya Royal Tour haionekani?
 
Awajue yeye Kama nani? Waliochanga wamelalamika fedha zao kutotumika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…