Hongera na kazi wadau..
Nitumie fursa hii kueleza habari Njema za Royal tour..
Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000)..
Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil..
Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.
Hongera zenu Ila bado Sana kuwafikia Egypt,Morocco,South Africa nk.[emoji116]
The Sunk Cost Fallacy 2 Msiwe mnakurupukia mambo mengine ambayo ni ya kitaaluma zaidi.
Vema mkajiridhisha na uhalisia kabla ya kuja kuandika humu.
Tatizo nchi hii u-chawa umegeuka mtaji.
Kila mtu anatumia u-chawa kwa nafasi yake.
Journalists
Politicians
Editors
Professor's
Police
Nk.
Utalii ni process ndefu ambayo ni tofauti na ununuzi wa bidhaa zingine tulizozowea katika maisha yetu ya kila siku.
Pia ikumbukwe,wazungu huwa hawana utaratibu wa kukurupukia mambo.
Wana utamaduni wa kupanga jambo kwa muda wa kutosha.
Na pia lazima liendane na misimu yao ya likizo na majira ya baridi.
Kwa hiyo sio sahihi,kuanza kuuaminisha Umma wa nchi hii kwamba Royal Tour tayari imeleta Impact kwenye utalii wetu.
Huu ni upotoshaji mkubwa.
Pia muelewe kwamba kuna platforms na efforts nyingine ambazo zinaitangaza Tanzania, tena kwa ubora wa kiwango cha hali ya juu,tofauti na hii Royal Tour yetu.
Mfano kwa uchache tu!
Kuna..
National Geographic!
Kuna Youtube! (ambako wadau mbalimbali wanajitangaza.).
TripAdvisor
Safari bookings
Nk.
Kabla ya kukurupuka na kuleta u-chwa kwenye jambo kama hili.
Tuambieni Cancelation zilikuwa ngapi,baada ya janga la covid19?
Muelewe kwamba covid19 iliibuka katikati ya kipindi cha watalii,wengi walisitisha safari zao baada ya janga hilo.
Halafu hawakuwa wamechukuwa fedha zao,bali walifanya amendment.
Sasa janga lilipopungua,wengi waliamua kukamilisha ratiba zao,sababu pesa ilikuwa imekwisha lipwa hapo awali.
Sasa basi,ikumbukwe pia kuna kundi lingine ambalo lilikuwa limechoka na lockdown iliyosababishwa na covid19.
Hilo nalo lilikuwa linatafuta hewa mpya Africa,hususan Tanzania ambako kwao walikuwa wakipata taarifa zetu vizuri sana,kuhusuana na ukubwa wa madhara ya covid19.
Ukiunganusha hayo makundi mawili makubwa,ndio unapata hii idadi iliyokuja kwa mkupuo mmoja na kufanya muanze kuupotosha umma.
Ukitaka uhalisia wa ujio wa watalii nchini,usitumie tu Data za NBS na TTB.
Tembelea Tour Operators ambao ndio rasmi wanaopambana na ma agents wao kutoka huko Ughaibuni.
Au nenda kwenye link ya "TATO"
Wao wanajua source za bookings na muda sahihi booking ilipofanyika.
Hawa NBS wao wanatumia records za Entry points kama viwanja vya ndege na malango ya mipaka yetu ya kimataifa.
Kama ni Royal Tour, basi ikifanikiwa tutaanza kuyaona matunda yake season hii na kuendelea.
Haya mengine ni blah blah tupu.
Nawashauri ma- chawa mumshauri mama yenu awaambie TANAPA na NCAA,waende wakatengeneze miundombinu kuanzia pale Loduare-Olduvai-Naabi Gate-Ikoma Gate-Ndabaka Gate na Ikoma Gate.
Magari yanaanguka na kuwaumiza wageni na saa ingine wanapoteza maisha.
Shauri ya ubovu wa miundombinu ya barabara.
Sehemu zingine hata maji kwenye vyoo yanakosekana.
Saa ingine wageni wanapoteza masaa kibao malangoni shauri ya uchache wa makarani na matatizo ya kimtandao.
Huku mmekaa mitandaoni mkisifia wakati hamjui uhalisia wa huko site.