Royal Tour yajibu! Ndani ya miezi 11 tu watalii waliotembelea Tanzania wafikia milioni 1.2

Royal Tour yajibu! Ndani ya miezi 11 tu watalii waliotembelea Tanzania wafikia milioni 1.2

Bahati mbaya wageni from Europe/America hawafahamu hiyo Royal Tour ni kitu gani.

Nikufahamishe tu wageni wanaokuja safari Tz wanakuja kwasababu ya marketing efforts zinazofanywa na tour operators wenyewe kwakushirikiana na agents, lakini pia sasa hivi kuna contents nyingi zinazopatikana YouTube, Trip Advisor an platform nyingine zinazoonyesha utalii wa Tanzania. Tena si kwanamna unayoifikiria wewe.

I have been in this industry for many many years so I should know about this.

Salaam kutoka North Serengeti. Sasa hivi majani ni kijani na wanyama wapo vizuri.

Tunaendelea kupiga kazi.
 
Hongera na kazi wadau..

Nitumie fursa hii kueleza habari Njema za Royal tour..

Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000)..

Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil..

Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.

Hongera zenu Ila bado Sana kuwafikia Egypt,Morocco,South Africa nk.[emoji116]

The Sunk Cost Fallacy 2 Msiwe mnakurupukia mambo mengine ambayo ni ya kitaaluma zaidi.

Vema mkajiridhisha na uhalisia kabla ya kuja kuandika humu.

Tatizo nchi hii u-chawa umegeuka mtaji.
Kila mtu anatumia u-chawa kwa nafasi yake.

Journalists
Politicians
Editors
Professor's
Police
Nk.

Utalii ni process ndefu ambayo ni tofauti na ununuzi wa bidhaa zingine tulizozowea katika maisha yetu ya kila siku.

Pia ikumbukwe,wazungu huwa hawana utaratibu wa kukurupukia mambo.

Wana utamaduni wa kupanga jambo kwa muda wa kutosha.
Na pia lazima liendane na misimu yao ya likizo na majira ya baridi.

Kwa hiyo sio sahihi,kuanza kuuaminisha Umma wa nchi hii kwamba Royal Tour tayari imeleta Impact kwenye utalii wetu.
Huu ni upotoshaji mkubwa.

Pia muelewe kwamba kuna platforms na efforts nyingine ambazo zinaitangaza Tanzania, tena kwa ubora wa kiwango cha hali ya juu,tofauti na hii Royal Tour yetu.

Mfano kwa uchache tu!
Kuna..
National Geographic!
Kuna Youtube! (ambako wadau mbalimbali wanajitangaza.).
TripAdvisor
Safari bookings
Nk.

Kabla ya kukurupuka na kuleta u-chwa kwenye jambo kama hili.

Tuambieni Cancelation zilikuwa ngapi,baada ya janga la covid19?

Muelewe kwamba covid19 iliibuka katikati ya kipindi cha watalii,wengi walisitisha safari zao baada ya janga hilo.

Halafu hawakuwa wamechukuwa fedha zao,bali walifanya amendment.

Sasa janga lilipopungua,wengi waliamua kukamilisha ratiba zao,sababu pesa ilikuwa imekwisha lipwa hapo awali.

Sasa basi,ikumbukwe pia kuna kundi lingine ambalo lilikuwa limechoka na lockdown iliyosababishwa na covid19.

Hilo nalo lilikuwa linatafuta hewa mpya Africa,hususan Tanzania ambako kwao walikuwa wakipata taarifa zetu vizuri sana,kuhusuana na ukubwa wa madhara ya covid19.

Ukiunganusha hayo makundi mawili makubwa,ndio unapata hii idadi iliyokuja kwa mkupuo mmoja na kufanya muanze kuupotosha umma.

Ukitaka uhalisia wa ujio wa watalii nchini,usitumie tu Data za NBS na TTB.

Tembelea Tour Operators ambao ndio rasmi wanaopambana na ma agents wao kutoka huko Ughaibuni.

Au nenda kwenye link ya "TATO"

Wao wanajua source za bookings na muda sahihi booking ilipofanyika.

Hawa NBS wao wanatumia records za Entry points kama viwanja vya ndege na malango ya mipaka yetu ya kimataifa.

Kama ni Royal Tour, basi ikifanikiwa tutaanza kuyaona matunda yake season hii na kuendelea.

Haya mengine ni blah blah tupu.

Nawashauri ma- chawa mumshauri mama yenu awaambie TANAPA na NCAA,waende wakatengeneze miundombinu kuanzia pale Loduare-Olduvai-Naabi Gate-Ikoma Gate-Ndabaka Gate na Ikoma Gate.

Magari yanaanguka na kuwaumiza wageni na saa ingine wanapoteza maisha.
Shauri ya ubovu wa miundombinu ya barabara.

Sehemu zingine hata maji kwenye vyoo yanakosekana.

Saa ingine wageni wanapoteza masaa kibao malangoni shauri ya uchache wa makarani na matatizo ya kimtandao.

Huku mmekaa mitandaoni mkisifia wakati hamjui uhalisia wa huko site.
20221221_112019.jpg
 
Morocco wanapata watalii 12M kwa mwaka. Mama ameonesha yuko serious na utalii ktk Royal Tour movie yake na Pira. Naamini kabisa atapambana zaidi kwa kushirikiana na North Africa ili kwa miaka 5 tuweze angalau ku-double idadi ya watalii nchini
 
Hongera na kazi wadau..

Nitumie fursa hii kueleza habari Njema za Royal tour..

Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000)..

Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil..

Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.

Hongera zenu Ila bado Sana kuwafikia Egypt,Morocco,South Africa nk.👇

Wengi wa hao watalii ni wale waliositisha safari zao(ambazo walishazilipia) kipindi kile cha corona. Walioko kwenye hii industry watanielewa.

Majibu ya RT tutayatathimini mwaka huu.
 
Hongera na kazi wadau..

Nitumie fursa hii kueleza habari Njema za Royal tour..

Idadi ya Watalii Waliotembelea Tanzania kwa miezi 11 ya mwaka 2022 wamefikia Milioni Moja na Laki mbili(1,200,000)..

Hizi Ni habari njema zikizoletwa na Royal tour na bila shaka Hadi Mwisho wa mwezi wa 12 Idadi ya Watalii itavuka 1.3Mil..

Bila Shaka huko tuendako Mambo yanaweza kuwa mazuri ikizingatia Tanzania umeweka lengo la kufikia Idadi ya Watalii mil.5 mwaka 2025.

Hongera zenu Ila bado Sana kuwafikia Egypt,Morocco,South Africa nk.👇

Chawa acha Kuremba sifa za kijinga kwa data za kupika.
 
Halafu anataka kutufumba midomo kwa kujificha kwenye ushahidi, ni sawa na mtu aulize sehemu kuku anapotolea kinyesi wakati upepo unapuliza.....
Yeye alete ushahidi, DEGE linalotumika kubebea wanyama lilitua Ili kubeba nn!!!

Kwani tunazalisha magari kwamba lilikuja kuyapeleka Ulaya magari tulozalisha Kutoka viwanda vyetu vya ndani???
 
Usikasirike ndugu. Mnyamazishe kwa kuijibu hoja yake kwa takwimu tu.
Atujibu pia Kwa Takwimu,

Baada ya Kasi ya kisafirishwa wanyama hai kwenda Nchi Hasa za kiarabu,

Anapredict utalii utakuwa Kwa % ngapi?

Na ikiwa utalii utaporomoka pia aseme ni Kwa % ngapi?😠😠😠😠
 
Na wewe pika za kwako mbuzi wewe,hizi taarifa zimetoka kwenye uchambuzi wa ripoti ya Uchumi wa banki kuu kwa mwezi Novemba.
Acha kupanick dogo, hakuna taasisi ya serikali kwa sasa inaaminika kwenye suala la uhakika wa data.
 
Leo Naona mmepewa memo ya Royal tour hapo Lumumba..

F*ckin Lol😂😀😀
 
Back
Top Bottom