Otorong'ong'o
JF-Expert Member
- Aug 17, 2011
- 37,957
- 26,414
Jamaniii....KAZI ya polisi ni kuilinda CCM TU.
Na wanajisikia Raha sana mpaka Huwa wanatamani kufi...rwa na viongozi wa CCM waone mikunduuu Yao.
Police hovyo sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaniii....KAZI ya polisi ni kuilinda CCM TU.
Na wanajisikia Raha sana mpaka Huwa wanatamani kufi...rwa na viongozi wa CCM waone mikunduuu Yao.
Police hovyo sana
Kwani uongo mzeeHayo yote yanatokana na mtazamo wako wa kufikiri polisi wanawashughulikia wapinzani tu nchii hii.
Wadau wametoa maoni yao juu ya kauli ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera (RPC), Wankyo Nyigesa kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumteuwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania haliyakuwa (IGP) Simon Sirro bado anaihudumia nafasi hiyo.
Baadhi wamesema siyo jambo baya kwa mtu kutamani cheo fulani huku wengine wakisema siyo sawa kutamani nafasi ya juu wakati aliyonayo hajaifanyia kazi ipasavyo.
Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumo, alisema mtu kutamani cheo cha juu siyo dhambi bali inaweza kutafsiriwa tofauti endapo atatumia njia za hujuma kupata nafasi anayoitamani.
“Siyo vibaya kuomba kuteuliwa, huwenda kuna kitu kakiona kuwa hakiko sawa na kufikiri kuwa endapo atapatiwa nafasi hiyo anaweza kukirekebisha hivyo huo ni ujumbe kwa IGP aliyopo,” alisema Olengurumwa.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga alisema misingi ya kiutendaji kazi au cheo cha kuteuliwa hakiombi ila Rais humteua mtu pale atakapoona kuwa anafaa.
“Watu wote hawawezi kuwa nafasi za juu usitamani cheo kikubwa wakati katika nafasi uliyopo bado hujatatua yaliyopo, katika mkoa alipopelekwa kuna mambo mengi ya kipolisi hayapo sawa hivyo tulitegemea angewaambia wanaKagera kuwa huko anakokwenda atafanya nini kutatua changamoto zilizopo,” alisema Anna.
Akizungumza jana Kibaha Mkoani Pwani wakati wa sherehe za kumuaga baada ya kuhamishwa katika mkoa huo na kupelekwa Kagera RPC Nyigesa, alisema moja ya malengo yake na ndoto zake kubwa ni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Polisi nchini (IGP) na anatamani Rais amteue huku akiahidi kuwa atafanya kazi kubwa.
Alibainisha kuwa awali alikuwa anajiandaa kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Kamishna wa Zanzibar, lakini baada ya nafasi hizo kuchukuliwa sasa anajiandaa kuwa IGP, na aninaamini kwamba Rais Samia anayasikia maombi yake.
“Siku moja tafadhali niteue kuwa IGP, mimi naamini nitafanya makubwa, huwa ninaomba sana Mama (Rais) siku moja aniote tu halafu anitamke tu niwe IGP, Mimi nitamuomba nifanye miaka mitatu halafu nimwambie Mama mimi nakukabidhi naondoka unaonaje hapo,” alisema Nyigesa.
“Binadamu lazima uangalie mbele, natamani kuwa IGP, najua IGP aliyopo Sirro hajafanya makosa anafanya mazuri, lakini mimi nitafanya mazuri zaidi, matarajio yangu ni hayo, unajua binadamu lazima uwe na malengo ya mbele, uwe na ndoto kubwa, huwezi tu kuwa una malengo ya kwamba nitaendeela tu kuwa RPC…mimi nataka kuwa nafasi za luu, ili nifanye makubwa kwa faida ya Watanzania wengi kuliko wa mkoa mmoja,” alisema Nyigesa.
Aliongeza kuwa anaamini siku moja Rais atakapomuona vizuri anaweza kumpa U-IGP na matamanio yake ni kuhudumu katika nafasi hiyo, na alimuhakikishia mkuu huyo wa nchi kuwa endapo atamuona anafaa na kumteua atakuwa amepata mtu sahihi kwa wakati sahihi.
Source: Nipashe
Wenye weredi hawajisemi,sifa zao hujitangaza,nakumbuka wakati wa IGP Said Mwema anateuliwa,iliwekwa CV yake,huyo alikuwa anafanya kazi Interpol Kituo Cha Kenya,CV kama hizo ndio zinahitajika,sasa huyu anajipigia debe kwenye mkutano wa Siasa, he is just sychophants,ass kisser,chawa!
Hakuna kitu,hujawahi hata kutoa shule kuhusu mambo ya usalama kwenye mtandao,leo unataka kuwa IGP,hapo pwani umefsnya nini Cha upekee,umeacha program gani za usalama,
Kwamba ni wapinzani tu Tanzania ndio wanashughulikiwa na polisi na wengine wasio wapinzani hawapati misukosuko ya polisi?Kwani uongo mzee
Keshaliwa kichwaWankyo Nyigesa ni room mate wangu mabibo hostel ni comedian flan hiv anapenda utani, mchangamfu sana lkn yote Tisa jamaa anaupendo sana. Mara ya kwanza kukutana nae room nilikua simuelewi kabisa lkn baadae nikagundua jamaa ana amani sana moyoni mwake.
Kukilinda dhidi ya nani mkuu? Kwani hao wapinzani wanataka kuwafanyia uhalifu ccm hadi ccm polisi iwalinde?Kazi ya police ni kulinda chama tawala
Tayari amerudishwa makao kusoma magazeti na kuchunguzwa juu. Amezingua kwa kweli.Muda si mrefu hana RPC,atakwenda kufundisha CCP au kusoma magazeti makao makuu.Fitina zao nizaidi ya Lumumba.
Dhidi ya wapinzani Ili wasichukue madarakani wanawasaidia ccm kuiba kuraKukilinda dhidi ya nani mkuu? Kwani hao wapinzani wanataka kuwafanyia uhalifu ccm hadi ccm polisi iwalinde?
YAMETIMIAWatamrudisha makao makuu kujiweni soon
Naona huyu jamaa u rpc ameuchoka,
Asubiri kupangiwa kazi maalum hivi karibini ya kuchemsha chai makao makuu ya polisi.
Ndiyo huyo kapigwa kipapaiHivi huyu jamaa sindio 2020 alikesha road kuzuia msafara wa TAL usifike Kibaha?
Amesharudishwa HQFinally yametimia
Naona huyu jamaa u rpc ameuchoka,
Asubiri kupangiwa kazi maalum hivi karibini ya kuchemsha chai makao makuu ya polisi.
Kama ni hivyo mbona 2015 vyama vya upinzani vilishirikiana kuweka mgombea mmoja wa kugombea urais ina maana walifanya hivyo ili kukabiliana na polisi au hawakuwa wakijua kwamba polisi wanawasaidia ccm?Dhidi ya wapinzani Ili wasichukue madarakani wanawasaidia ccm kuiba kura
Kama ni hivyo mbona 2015 vyama vya upinzani vilishirikiana kuweka mgombea mmoja wa kugombea urais ina maana walifanya hivyo ili kukabiliana na polisi au hawakuwa wakijua kwamba polisi wanawasaidia ccm?