Ukisema si nzuri sana unakuwa unaifananisha ni timu gani?
Kumbuka yupo nyumbani, kuna nguvu inayo m-favor kwa yeye kupata ushindi
Pili magoli tuliyofungwa binafsi naona kupeleka lawama kwa wachezaji ni kama tunawaonea tu
Hivi goli la kwanza lile utampa nani lawama?
Mbini ya mwalimu tangu dakika ya kwanza iliomesha wazi kua amekuja kuzuia, matokeo ya sare ndio matokeo aliyoyataka
Timu icheze kwa kujilimda na ikipata nafasi basi ifanye shambulizi la kushtukiza
Berkane wameshindwa kutufunga kwa njia ya pasi na kufika golini, kilichowapa faida ni ile mipira ya kutengwa so kwa situation hiyo ukiangalia na utulivu waliokuwa nao tujaribu kuwapa credit nao, hii ni timu bora huo ndio ukweli.