RS Berkane 2- 0 Simba Sc | CAF Confederation Cup | Stade Municipal de Berkane

RS Berkane 2- 0 Simba Sc | CAF Confederation Cup | Stade Municipal de Berkane

Zengwe La Soka La Africa linafahamika Kwa hiyo Sisi Mashabiki na Wapenzi Wa 'Nguvu Moja' tumeshaelewa na Tunawapa Moyo Wachezaji Wetu Kuwa Hayo Matokeo ndio 'Imeisha Hiyo'.... Wahamishe Mawazo Yao Gemu Zinazo kuja, Na Kwa Kadiri tunavyowajua hizi timu Zote ni Nyepesi saaana..cha Muhimu Wang'ate Meno....Hata Akija Bayeni Muncheni analala....
 
Not necessarily kumiliki mpira mkuu, pick some moments kamshambulie mpinzani ili nayeye ajue kwamba yuko hatarini kufungwa hivyo aje kwako kwa heshima.

Kipindi cha pili bado Berkane alikua na possession kubwa kuliko sisi lakini hatukukaa nyuma muda wote, tukisubiri yeye aje kutushambulia sisi kazi yetu iwe ni kulinda tu.

Hiki ndicho wadau tunaamini kwamba ndio ilipaswa kubwa best approach.

Jambo jingine, in a long run, Simba inapaswa kupunguza wachezaji wanaopunguza ufanisi wa timu.
Mchezaji ambaye hawezi kutuliza mpira, ambaye hawezi kupiga pasi kwa usahihi, wachezaji ambao hawawezi "kukaa na mali", n.k

Madhara ya hawa watu unaweza usiyaone kila siku, lakini kimsingi wanashusha sana overall performance ya timu.

Yaani hawa ni sawa na wanafunzi wanaopata division two pale St. Francis secondary school, wanakua hawajafeli lakini wanaifanya shule isiwe ya kwanza kitaifa.

Nadhani umenielewa.
Nakubaliana na hoja yako kwamba simba ilipaswa kucheza kwa kumiliki ili kuweza kujiweka katika usalama.

Na ni kweli kuna utofauti wa ku dominate mpira kati ya kipindi cha kwanza na cha pili kwa upande wa simba

Lakini kipindi cha pili ndio kipindi ambacho simba imecheza sana foul na kusababisha kadi za njano kutolewa.

Hiyo ni kwasababu walizidiwa sana uwezo na hapo ndipo matumizi ya nguvu yalipoanza, na ukumbuke kua berkane wamekuwa wakitumia mipira iliyokufa kutengeneza nafasi ya kushambulia na kusababisha magoli 2

Lakini pia hawa jamaa walikuwa wanakaba na kufanya pressing za nguvu kiasi ambacho kilikuwa kinawapa ugumu wachezaji wetu kuweza kumiliki mpira bila kupoteza.

Halafu swala la wachezaji kubadilishwa hilo nalo nila muhimu, msimu ujao tuachane na wachezaji ambao wanakuja kukuzia viwango vyao simba, inabidi tununje wachezaji ambao wana title kwenye mashindano makubwa kama haya
 
Unataka kusema kulinda ni kuwa na idadi kubwa ya walinzi ?
(Mfano golikipa na mabeki 10).

Na kushambulia ni kuwa na idadi kubwa ya washambuliaji ?
(Mfano golikipa na washambuliaji 10) ?
Nimekuambia position za wachezaji hao sio wote wanaweza kubaki kwenye kulinda tu

Nafasi anayocheza kapombe huwezi kumfananisha na wawa, huyu ni mtu ambaye anafika mbele na anaweza kukaba na kufunga na ndio maana nimekuambia kua kuna wachezaji wanakuwa wanatumika kama target yenye plan A na B kwa mpigo
 
Nini lilikua lengo la kuwa na Kanoute, Nyoni na Kennedy wakati tayari nyuma una Onyango na Inonga ?
Nani anapandisha timu hapo ku link na Bocco, Sakho na Banda wakati hao wote walikua wanataka kukaa nyuma ?

Anyways, tugange yajayo, tuna points 4, tukishinda mechi mbili za nyumbani tutakua na points 10 ambazo kwa asilimia kubwa zitatuvusha.

Ila tukishavuka tu, tutaondolewa mashindanoni na mpinzani yeyote yule ambaye yuko serious.
 
Haya mashindano ni tough sana na napenda simba angekuwa anapata series ya kukutana na upinzani mkali zaidi ili umjenge akomae

Tukifika robo ni swala la kushukuru sana, maana saizi hakuna timu ya kuibeza na kuichukulia kibonde

We si umemuona mniger alichokifanya leo huko kamuua mtu goli 2?

Tukizitumia vizuri mechi za nyumbani tukashinda zote itakuwa ni hatua nzuri
 
Hata hao Berkane si wazuri sana. Japo wamemkojolea mtu mbili
Unatumia kigezo kipi kusema so wazuri broh 2018 wamefika quarter-final 2019 wamefika final na 2020 wamechukua ilo kombe how comes unai undermine team kama hiyo
 
Hivi wakati mnaongea hayo yote mnajua kuwa Leo Simba ilikuwa na kiungo mmoja tu katikati ya uwanja!?
Mnajua kuwa
MKUDE
LWANGA
MUZAMIRU
CHAMA (KANUNI)
BWALYA
DILUNGA
KANOUTE ( alilazimika tu Leo kucheza lakini hakuwa fit aliumia mazoezini jana)

Kwa hali hii Ungekuwa Pablo Ungekuwa na chaguo gani hasa ukiwa ugenini Kwa waarabu ikiwa umebaki na kiungo mmoja tu!? ambaye NYONI tena Kwa kuforce sababu yeye ni beki alafu umri umeenda.
Timu imebaki na mawinga tupu
SAKHO
BANDA
MHILU
JIMSON ambaye naye Hana uzoefu wa hizi mechi za kimaifa hata kidogo.

Yaani mfano Leo itokee Kwa wakati mmoja mfano
AUCHO
BANGALA
MAUYA
SURE BOY
Wote wawe majeruhi Kwa wakati mmoja Kisha NTIBAZONKIZA na FEI TOTO wana KADI alafu una mechi na mechi na Raja Casablanca pale Morocco utafanyaje!?

Mnapo mlaumu kocha Kwa Jinsi alivyo panga kikosi na approach aliyo itumia lazima Muangalie pia na timu ipo kwenye wakati gani na inacheza na nani na wapi??

Berkane yupo nyumbani kwake pale hujui wamejipangaje ubora wa viungo walio nao huujui vizuri huku wewe ukiwa na kiuongo mmoja tu tena ni beki anaforce kucheza kati alafu mzee na Hana mechi fitness sababu hakupata mechi nyingi za kucheza hapa kwenye ligi alafu unataka uende ukajiachie ufunguke mbele ya Berkane pale kwao Morocco ?? Mko serious kweli !!?

Sina cha kumlaumu PABLO Kwa mchezo wa Leo amefanya kile kilichotakiwa kulingana na hali ya timu ilivyo kwasasa turudi nyumbani tujipange Kwa mchezo ujao.
 
Haya mashindano ni tough sana na napenda simba angekuwa anapata series ya kukutana na upinzani mkali zaidi ili umjenge akomae

Tukifika robo ni swala la kushukuru sana, maana saizi hakuna timu ya kuibeza na kuichukulia kibonde

We si umemuona mniger alichokifanya leo huko kamuua mtu goli 2?

Tukizitumia vizuri mechi za nyumbani tukashinda zote itakuwa ni hatua nzuri
Watu wanaongea tu hawaangalii uhalisia jamani kila mtu anashinda nyumbani kwake we ukifanikiwa kuokota ata point Moja ugenini we kidume. Leo MIMOSSA Kilicho mkuta haamini kabisa na Berkane vile vile wawe makini na hao jamaa pale Niger sio sehemu salama pale wasipo kuwa makini watakufa pale na huku Kwa mkapa wajipange
 
Na hayo matokeo ni uwezo binafsi wa wapinzani

Hii ya leo sio ya kumlaumu kanoute kama ile ya niger

Utapoteza muda mwingi kutafuta makosa madogo madogo ya wachezaji ili kuhalalisha sababu ionekane ni wao wamefelisha

Hii ya leo tukiri tu kuwa hawa majamaa wametuzidi kiwango bila kupepesa macho
Berkane hawana mpira wa kutisha ...naamini kuwa watakuja tu kupoteza hapa kwa mkapa inshaAllah. Ukiacha na uwezo wao wa kutumia mawinga wenye kasi kushoto na kulia ,sijaona lingine.Uwezo wao wa kuweka mpira wa pasi chini ni mdogo sana. Simba waliwaheshimu wapinzani kupita kiasi na hicho ndicho kilichotokea
 
Hivi wakati mnaongea hayo yote mnajua kuwa Leo Simba ilikuwa na kiungo mmoja tu katikati ya uwanja!?
Mnajua kuwa
MKUDE
LWANGA
MUZAMIRU
CHAMA (KANUNI)
BWALYA
DILUNGA
KANOUTE ( alilazimika tu Leo kucheza lakini hakuwa fit aliumia mazoezini jana)

Kwa hali hii Ungekuwa Pablo Ungekuwa na chaguo gani hasa ukiwa ugenini Kwa waarabu ikiwa umebaki na kiungo mmoja tu!? ambaye NYONI tena Kwa kuforce sababu yeye ni beki alafu umri umeenda.
Timu imebaki na mawinga tupu
SAKHO
BANDA
MHILU
JIMSON ambaye naye Hana uzoefu wa hizi mechi za kimaifa hata kidogo.

Yaani mfano Leo itokee Kwa wakati mmoja mfano
AUCHO
BANGALA
MAUYA
SURE BOY
Wote wawe majeruhi Kwa wakati mmoja Kisha NTIBAZONKIZA na FEI TOTO wana KADI alafu una mechi na mechi na Raja Casablanca pale Morocco utafanyaje!?

Mnapo mlaumu kocha Kwa Jinsi alivyo panga kikosi na approach aliyo itumia lazima Muangalie pia na timu ipo kwenye wakati gani na inacheza na nani na wapi??

Berkane yupo nyumbani kwake pale hujui wamejipangaje ubora wa viungo walio nao huujui vizuri huku wewe ukiwa na kiuongo mmoja tu tena ni beki anaforce kucheza kati alafu mzee na Hana mechi fitness sababu hakupata mechi nyingi za kucheza hapa kwenye ligi alafu unataka uende ukajiachie ufunguke mbele ya Berkane pale kwao Morocco ?? Mko serious kweli !!?

Sina cha kumlaumu PABLO Kwa mchezo wa Leo amefanya kile kilichotakiwa kulingana na hali ya timu ilivyo kwasasa turudi nyumbani tujipange Kwa mchezo ujao.
Kama alikuwa anajua anakwenda kupoteza game hakukuwa na maana ya kupaki basi...Mhilu,kagere,morrison, jimmyson hawa wote walikuwepo sub...kwann unawaweka nje..na why amtoe banda kipindi cha pili wakati kulikuwa na nafasi ya kuondoa beki na kiungo mkabaji mmoja na akaongeza midfielders kati ? Berkane nguvu yao ipo kwenye kutumia winga wa pembeni tu ..ila ukiamua kuwawekea mpira chini unawafunga..cheki game yao dhidi ya Asec na USGN
 
Nini lilikua lengo la kuwa na Kanoute, Nyoni na Kennedy wakati tayari nyuma una Onyango na Inonga ?
Nani anapandisha timu hapo ku link na Bocco, Sakho na Banda wakati hao wote walikua wanataka kukaa nyuma ?

Anyways, tugange yajayo, tuna points 4, tukishinda mechi mbili za nyumbani tutakua na points 10 ambazo kwa asilimia kubwa zitatuvusha.

Ila tukishavuka tu, tutaondolewa mashindanoni na mpinzani yeyote yule ambaye yuko serious.
We ndugu unanifurahisha sana aisee wee Ungekuwa kocha wewe Leo tungepingwa 7 kama Ruvu shooting nakwambia!!
 
Nini lilikua lengo la kuwa na Kanoute, Nyoni na Kennedy wakati tayari nyuma una Onyango na Inonga ?
Nani anapandisha timu hapo ku link na Bocco, Sakho na Banda wakati hao wote walikua wanataka kukaa nyuma ?

Anyways, tugange yajayo, tuna points 4, tukishinda mechi mbili za nyumbani tutakua na points 10 ambazo kwa asilimia kubwa zitatuvusha.

Ila tukishavuka tu, tutaondolewa mashindanoni na mpinzani yeyote yule ambaye yuko serious.
Nakubaliana na wewe ..ktk knockout stage tukiingia na mentality hii ya kwa mkapa hatoki mtu basi ni lazima tung'oke tu hakutakuwa na namna kama ambavyo tulitolewa na jwaneng galaxy au kaizer chiefs. Piga boli nyumbani na ugenini ikitokea unefungwa hakuna cha kujilaumu cuz mpira umepiga wa kutosha zinabaki tu kudra za Mungu.
 
Kama alikuwa anajua anakwenda kupoteza game hakukuwa na maana ya kupaki basi...Mhilu,kagere,morrison, jimmyson hawa wote walikuwepo sub...kwann unawaweka nje..na why amtoe banda kipindi cha pili wakati kulikuwa na nafasi ya kuondoa beki na kiungo mkabaji mmoja na akaongeza midfielders kati ? Berkane nguvu yao ipo kwenye kutumia winga wa pembeni tu ..ila ukiamua kuwawekea mpira chini unawafunga..cheki game yao dhidi ya Asec na USGN
Hiyo midfield kati unaenda kumuongeza nani pale kati ya hao ulio wataja hapo?? Morrison, MHILU na JIMSON wote mawinga hao sa hapo nani utampeleka katikati ya kiwanja pale awe mbadala wa chama au Bwalya??

Ile mijamaa inavyopiga longballs namna Ile unadhani kama kusingekuwa na hiyo back three ya Kennedy, Inonga na Onyango unadhani tungepingwa ngapi Leo??

Hao jamaa usiwaone wajinga wameamua kupitia pembeni sababu katikati palikuwa pangumu kupitika Kwa uwepo wa Kanoute, Nyoni na Inonga kwenye mstari wa ulinzi japo hawakuwa na kiwango kizuri Leo.

Tungekuwa na Mkude pale alafu Kanoute Yuko fit au Muzamiru yassin acheze sambamba na Mkude alafu juu tuwe na playmaker kama Chama au Bwalya kulia Banda/Morrison kushoto Sakho mbele Kuna Bocco ( Bacco kwasababu anauwezo wa kuchezesha timu tofauti na Kagere mzee wa kuvizia kwenye box tu) Hawa jamaa wasinge Toka Hawa.

Kwenye ulinzi kungebaki na Onyango na Inonga. Kushoto Zimbwe kulia Kapombe hapo timu ingetembea vizuri.

Lakini Leo tumewakosa watu muhimu sana kwenye timu ikabidi tucheze kulingana na hali ya timu ilivyo.

Tungesema tukafunguke huku katikati una Nyoni na Kanoute ambao wapo hawako fit ki mchezo alafu huku una Morrison na Banda ndani Kwa wakati mmoja ambao hawakabi timu ikipoteza mpira na jinsi Kapombe na Zimbwe wanavyopanda vile na Ile kasi ya Kisinda TK Master historia ya hamsa hamsa ingejirudia Leo pale.
 
Mkuu, kwahiyo second half tumepigwa tatu (nusu ya hizo saba) ?
Sasa naona umeanza kuelewa umuhimu wa Ile backthree pale nyuma eeh ?? Mechi za ugenini hazichezwi kama hivyo unavyofikiri mkuu. Kwa uwezo mkubwa wa washambuliaji wa Berkane alafu tungecheza kama tulivyo cheza nawale wa Niger tungeaibika zaidi Leo
 
Nakubaliana na wewe ..ktk knockout stage tukiingia na mentality hii ya kwa mkapa hatoki mtu basi ni lazima tung'oke tu hakutakuwa na namna kama ambavyo tulitolewa na jwaneng galaxy au kaizer chiefs. Piga boli nyumbani na ugenini ikitokea unefungwa hakuna cha kujilaumu cuz mpira umepiga wa kutosha zinabaki tu kudra za Mungu.
😂😂😂😂 Daah aisee sawa mkuu.
 
Leo majira ya saa 4:00 Usiku, RS Berkane watakuwa wanawakaribisha Simba Sc katika mchezo wa tatu wa CAF Confederation Cup katika dimba la Stade Municipal de Berkane, nchini Morocco.

Katika mchezo huu, Simba itawakosa Jonas Mkude, Mugalu na Israel Mwenda kutokana na sababu mbalimbali.

Ikumbukwe, Simba wataingia katika mchezo huo wakiwa na alama 4 huku Berkane wakiwa na alama 3 katika Kundi D.

Mchezo utakuwa mubashara kupitia AzamTv pamoja na Dstv.

Updates zote utazipata hapa, Simba...Nguvu Moja
Hujaweka update hata moja
 
Ka
Mkuu, leo Pablo ameanza na WALINZI NANE.
Ninaposema walinzi namaanisha defending or defending minded players wa idadi hiyo.

1. Manula
2. Kapombe
3. Zimbwe
4. Inonga
5. Kennedy
6. Onyango
7. Erasto Nyoni
8. Kanoute

This is too much. Kucheza kwa kujilinda haimaanishi uwe na walinzi wengi. Ni namna timu nzima inavyocheza. Kuna siku atakuja kucheza na mabeki kumi huyu jamaa.

Wachezaji wasio walinzi walikua watatu tu,

9 Bocco
10 Sakho
11 Banda

Nilivyoona tu hicho kikosi nikapata wasiwasi, kwamba ina maana tunaamini katika idadi ?
Ulitaka acheze nani ilhal ,viungo wote ni majeruhi!?
Acheni udwanzi....wanaume wamepigwa wanasimama maisha yanadonga...Robo fainali ni lazima!
 
FMpEPFMWUAsMQls.jpeg
 
Back
Top Bottom