Not necessarily kumiliki mpira mkuu, pick some moments kamshambulie mpinzani ili nayeye ajue kwamba yuko hatarini kufungwa hivyo aje kwako kwa heshima.
Kipindi cha pili bado Berkane alikua na possession kubwa kuliko sisi lakini hatukukaa nyuma muda wote, tukisubiri yeye aje kutushambulia sisi kazi yetu iwe ni kulinda tu.
Hiki ndicho wadau tunaamini kwamba ndio ilipaswa kubwa best approach.
Jambo jingine, in a long run, Simba inapaswa kupunguza wachezaji wanaopunguza ufanisi wa timu.
Mchezaji ambaye hawezi kutuliza mpira, ambaye hawezi kupiga pasi kwa usahihi, wachezaji ambao hawawezi "kukaa na mali", n.k
Madhara ya hawa watu unaweza usiyaone kila siku, lakini kimsingi wanashusha sana overall performance ya timu.
Yaani hawa ni sawa na wanafunzi wanaopata division two pale St. Francis secondary school, wanakua hawajafeli lakini wanaifanya shule isiwe ya kwanza kitaifa.
Nadhani umenielewa.