Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Tukio la ajabu limetokea katika anga za juu na kuwaacha watu midomo wazi. Tukio gani hilo? Endelea kusoma...
Wakati dunia nzima ikifuatilia safari ya Artemis II, rubani wa misheni hiyo, Victor Glover, akiwa katika anga za juu, badala ya kutoa ujumbe wa kisayansi, ametoa ujumbe wa kiroho!
Victor Glover, akiwa mbali kabisa na dunia, katika ukimya wa anga za juu, amesema kwamba jambo muhimu kuliko yote ambalo mwanadamu anaweza kulibeba popote alipo ni upendo. Kisha akanukuu mafundisho ya Yesu Kristo katika Biblia, ambapo Yesu alisema: amri kuu ni kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote, na amri kuu ya pili ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako.
Tazama sehemu ya ujumbe wa rubani Victor Glover katika video hii...