Ndugu yangu, ni muhimu sana kumuomba Mungu atulinde safarini. Hivi hujui kwamba kuna marubani na wanaanga wengi waliofariki wakati walipoanza kupaa kwenda anga za juu au wakati wa kurudi?
Unaikumbuka ajali ya Space Shuttle Challenger (1986)? Chombo hiki cha NASA kililipuka sekunde chache tu baada ya kurushwa. Wanaanga wote 7 waliokuwemo walifariki.
Mwaka 2003 ilitokea ajali nyingine ya Space Shuttle Columbia. Chombo hicho kiliharibika kilipokuwa kinarudi duniani, kikasambaratika angani. Wanaanga wote 7 walipoteza maisha.
Unaikumbuka Soyuz 11? Hiki kilikuwa chombo cha Soviet space program. Wanaanga watatu walifariki baada ya hewa kutoka ndani ya chombo hicho walipokuwa wanarudi duniani.
Matukio hayo yote yanaonyesha kuwa safari za anga ni hatari sana, hivyo ni muhimu kuomba ulinzi wa Mungu hata katika safari hizo. Mungu ni Mkuu, anao uwezo wa kutuepusha na ajali tukimtumaini.
Mimi hilo nimelishuhudia katika safari nyingi angani, baharini na barabarani. Mungu ameniepusha na ajali nyingi zilizokuwa dhahiri kabisa.
Nafikiri umeona sasa kwanini rubani Victor Glover alimtanguliza Mungu katika safari yao.
Halafu nakutahadharisha ujiepushe kutamka matusi. Matusi ni mojawapo ya dhambi ambazo watu wanaziona ndogo, lakini zitawapeleka katika moto wa milele. Soma 1 Wakorintho 6:9-10
Cc:
Davidmmarista