MlimaSayuni
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 7,285
- 13,703
Waislamu walisema mwezini kuna adhana 🤣🤣
Huko kwenye moto bado hujafika umejuaje kuwa umeokoka?Nimeokoka hukumu ya kuchomwa moto milele.
Kama mimi sina akili, je huyo aliyekuhubiri Injili akiwa angaza za juu, wewe unamzidi akili?
Pole sana, unasubiri uone ndio uamini? Soma Yohana 20:29.Huko kwenye moto bado hujafika umejuaje kuwa umeokoka?
Tumia akili zako vizuri Ajuza
Huyo bado hajasoma Mathayo 12:36-37. Katika andiko hilo, Yesu alisema:Bangi eee
Nipeleke kanisani kwenu.Nakusikitikia sana kwa sababu, kwa video hii uliyoweka, tayari umejiweka kwenye kundi la watakaokuwa mkono wa kushoto, siku ya hukumu, maana umeisikia Injili ukawakashifu waliokuletea Injili kuwa ni watu wa bangi. Nasikitika hutakuwa na la kujitetea utakapoambiwa:
"Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, ulioandaliwa kwa ajili ya Ibilisi na malaika zaike." (Mt 25:41).
Tubu kabla neema haijafungwa.
YoungHoon Kim mtu mwenye highest IQ duniani ,with IQ score ya 276 mtu mwenye akili zaidi duniani anamwamini YESU Kristo na hii inaendana na maandiko ya biblia Methali 1:7Shetani ameaibika sana safari hii. Uongo wake kwamba wanaomwamini Yesu ni vichaa, umesagwa sagwa na rubani mahiri wa NASA!
Ameen, ubarikiwe sanaYoungHoon Kim mtu mwenye highest IQ duniani ,with IQ score ya 276 mtu mwenye akili zaidi duniani anamwamini YESU Kristo na hii inaendana na maandiko ya biblia Methali 1:7
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
ZABURI 14:2 “2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.”
ZABURI 14:1 “1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu
Hapo hapo unapoishi, tafuta kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha kuishi maisha matakatifu, ujiunge nalo. Ila kama hujatubu, fuatisha sala hii ya toba kwanza, utaokoka sasa hivi:Nipeleke kanisani kwenu.
Nataka nikuoe mpenziHapo hapo unapoishi, tafuta kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha kuishi maisha matakatifu, ujiunge nalo. Ila kama hujatubu, fuatisha sala hii ya toba kwanza, utaokoka sasa hivi:
Omba sasa sala hii ya toba kwa moyo wa dhati:
Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na nimeamua kuziacha kabisa. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha matakatifu. Halafu kama nilivyokuambia, tafuta Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, ili ujifunze jinsi ya kuishi maisha mapya ya wokovu. Ubarikiwe sana
Asante kutuhabarishaTukio la ajabu limetokea katika anga za juu na kuwaacha watu midomo wazi. Tukio gani hilo? Endelea kusoma...
Wakati dunia nzima ikifuatilia safari ya Artemis II, rubani wa misheni hiyo, Victor Glover, akiwa katika anga za juu, badala ya kutoa ujumbe wa kisayansi, ametoa ujumbe wa kiroho!
Victor Glover, akiwa mbali kabisa na dunia, katika ukimya wa anga za juu, amesema kwamba jambo muhimu kuliko yote ambalo mwanadamu anaweza kulibeba popote alipo ni upendo. Kisha akanukuu mafundisho ya Yesu Kristo katika Biblia, ambapo Yesu alisema: amri kuu ni kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote, na amri kuu ya pili ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako.
Tazama sehemu ya ujumbe wa rubani Victor Glover katika video hii...
Marko 12:28-34
Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza? Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye; na kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama nafsi yako, kwafaa kuliko sadaka nzima za kuteketezwa na dhahibu zote pia. Naye Yesu, alipoona kwamba amejibu kwa busara, alimwambia, Wewe hu mbali na ufalme wa Mungu. Wala hakuthubutu mtu kumsaili neno tena tokea hapo.
Ndugu yangu, ni muhimu sana kumuomba Mungu atulinde safarini. Hivi hujui kwamba kuna marubani na wanaanga wengi waliofariki wakati walipoanza kupaa kwenda anga za juu au wakati wa kurudi?Kutapatapa na uzwazwa mtupu. Kwani, amefika huko kwa sayansi au hizo ngano uchwara zako. Acneni udandizi kumbaff