Rafiki, jinsi unavyoendelea ku-copy na ku-paste majibu ya AI ndivyo unavyojionesha wazi kwamba Biblia imekupita kando. AI haiwezi kukupa majibu yaliyo sahihi 100%. Kwa mfano: andiko hili la
1 Wakorintho 14:33, alilokupa AI wako, halina uhusiano kabisa na kile tunachoongea hapa.
AI wako amekuambia pia Yesu alinena wazi, sawa, lakini alinena wazi kuhusu nini? Na je, kila aliponena wazi watu wote walimuelewa? Jibu ni HAPANA. Angalia hapa, Wayahudi walitaka kumpiga Yesu kwa mawe kwa sababu hawakuelewa aliyowaambia...
Yohana 8:57-59
"Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Abrahamu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Kabla ya Abrahamu kuwako, mimi niko. Basi wakaokota mawe ili wamtupie...."
Andiko hilo linaonesha Yesu alinena wazi kuwa kabla Ibrahimu hajazaliwa, Yeye Yesu alikuwepo. Lakini Wayahudi hawakumwelewa. Kwa ufahamu wao walijua ana miaka chini ya 50, wasitambue ya kuwa Yeye ndiye Mungu, na hana mwanzo. Hivyo ni kweli alikuwepo kabla ya Ibrahimu.
Kwahiyo AI yako imekudanganya! There is a saying that goes, "To speak is not necessarily to be understood." It suggests that communication is a complex, two-way process rather than a simple transmission of information. Ndio maana nazidi kusisitiza kwamba ili uyaelewe Maandiko, tubu dhambi zako, uokoke na ujazwe Roho Mtakatifu. Ukifanya hivyo, Roho Mtakatifu atakuongoza kuyaelewa Maandiko. Otherwise utanifanya nitumie muda wangu mwingi bure kujaribu kukuelewesha, halafu mwisho wa siku utake kunipiga mawe. Mimi pia kabla sijaokoka, kuna mambo nilikuwa siyaelewi hata watu walivyojaribu kunielewesha. Lakini baada ya kuokoka na kujazwa Roho Mtakatifu, Maandiko nayaelewa kwa urahisi. Katika post zilizotangulia nilikuambia kwamba kama unashindwa kujua mambo ya msingi kama vile dhambi ya kutukana, utawezaje kujua mambo complex kama hili la Uungu wa Yesu. Unahitaji msaada wa Roho Mtakatifu.
Halafu, my friend, unapotumia Qur'an kujaribu kunipa majibu ya hoja zangu, hapo sasa ndio unaharibu kabisa. Mada hii sio mada ya kushindanisha Biblia na Qu'ran. Kama lengo lako ni kutaka kuonesha kwamba Qu'ran ndio kitabu bora, basi hapa sio mahali pake. Ni heri uanzishe mada nyingine yenye lengo hilo. Vinginevyo, nitakaa kimya nisikujibu tena kama Yesu alivyofanya katika Mathayo 27:12–14.