Rubani wa Artemis II ahubiri Injili akiwa anga za juu!!

kwani wavalishwa pampers wanaona nini ?? kinyesi ??
Tayari umejitega kwa mtego wako mwenyewe! Kinywa chako kimekutambulisha wazi kwamba wewe ni Antichristos na unailazimisha AI ikusaidie kupinga Uungu wa Yesu. Hiyo kauli yako ya matusi imefunua jinsi ulivyo kwa ndani.

Mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni. Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao. (Mathayo 7:17-20).
 
YESU NI MUNGU. *** MUDI
 
Kobaz wanaona wivu 🤣🤣🤣🤣... Huu uzi wanajisonya tu..

Hivi kwa mtu mwenye akili, nini cha ajabu alicho tamka?....
Mbona wa Iran ambao wote ni Madactari (Dr by qualification) walivyo sema kwenye kikao chao na wamarekani kifunguliwe kwa sala..hamkusema?
By the way, safari ilikuwa ya kwenda kupiga picha na sio kwenda mwezini.....hawakufika mwezini....
 
Ndio ushahidi wa Yesu kuwa ni mungu huo ??
 

Leo ninawe mpaka utambuwe kuwa Yesu ni mtu kama wewe wala si Mungu

“Unasema Yesu alikuwa tumboni na bado anasimamia dunia? Hiyo si Biblia — ni mawazo yako tu.”

1. Biblia inasema Yesu alikua kama mwanadamu wa kawaida​

Yesu Kristo: “Akazidi kuendelea katika hekima na kimo…” (Luka 2:52). Mungu hakui, wala haongezeki hekima , Huyo ni mwanadamu, si Mungu.

2. Yesu alikuwa na mipaka ya maarifa​

“Wala Mwana hajui…” (Marko 13:32) . Mungu anajua kila kitu . Asiyejua hawezi kuwa Mungu.

3. Yesu hana uwezo wa kujitegemea​

“Siwezi kufanya neno lolote kwa nafsi yangu” (Yohana 5:30). Mungu hawezi kuwa na tegemezi . Hapa Yesu anaonyesha utegemezi.

4. Biblia inasema Mungu si mwanadamu​

“Mungu si mwanadamu…” (Hesabu 23:19) . Wewe unasema Mungu yuko tumboni kama mtoto . Unapingana moja kwa moja na Biblia yako.

5. Kuhusu Wakolosai 1:17​

Hapo haimaanishi Yesu ndiye anayeshikilia dunia kwa nafsi yake. Biblia inaeleza wazi: “Kwa yeye vitu vyote viliumbwa…” (Wakolosai 1:16) Hii ni lugha ya mamlaka aliyopewa, si kwamba yeye ndiye Mungu
Na Aya nyingine inasema wazi: “Kwa ajili yetu kuna Mungu mmoja, Baba…” (1 Wakorintho 8:6)
Muumba wa kweli ni Baba, si Yesu.



 
Ndio ushahidi wa Yesu kuwa ni mungu huo ??
Huo ni ushahidi kuwa Maandiko huyajui.
Mtu anayeshindwa kuelewa jambo la msingi kabisa kwamba kutukana ni dhambi, anaonyesha wazi kwamba kweli haimo ndani yake. Biblia inasema maneno mabaya hayapaswi kutoka katika vinywa vyetu (Waefeso 4:29), na watukanaji hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:10). Sasa kama msingi huo mdogo hujauelewa, unawezaje kudai unaelewa mambo ya juu zaidi kama Uungu wa Kristo?
 

Ingalikuwa vizuri ukatupa ushahidi wa uungu wa Yesu , usikimbie,
Kuhusu kuutukana sijui huyu unayempakazia uungu utampa daraja lipi la matusi?

Tunampima Bwana Yesu Kristo sawa na maandiko ya Biblia. Bila ya kupoteza muda ningependa kukuletea baadhi ya maneno na lugha ya Bwana Yesu aliyotumia katika uhai wake.

1. Wasioamini (wasio Waisraeli) wameitwa mbwa na nguruwe. (Mathayo 7:6).
2. Aliwaita watu wabaya: ”Enyi wazao wa nyoka” (Mathayo 12:34).
3. Mayahudi waliitwa: “Kizazi cha zinaa.” (Mathayo 12:40,, 16:4).
4. Mayahudi waliitwa “Wazinifu na wakosefu.” (Marko 8:38).
5. “Ole wenu waandishi na wafarisayo, wanafiki,” (Mathayo 23:16).
6. “Ole wenu viongozi vipofu.” (Mathayo 23:16).
7. “Enyi nyoka, wana wa majoka (Mathayo 23:33).
8. “Watu wengine waliitwa mbwa.” (Mathayo 15:27).
9. Aliwaita manabii wenzake: “wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi.” (Yohana 10:8).
10. Aliwaita wanafunzi wake: ”Enyi kizazi kisicho amini, kilichopotoka.” (Mathayo 17:17).
11. Akamwambia Petro “Nenda nyuma yangu Shetani.” ( Mathayo 16:23).
 
Hayo Maandiko ili ujue tafsiri yake, unahitaji uokoke kwanza, ujazwe Roho Mtakatifu ndio utaelewa Yesu alikuwa anamaanisha nini kutamka hivyo. Vinginevyo huyo AI wako atazidi kukupotosha.

1 Petro 2:22
“Yesu hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.”
 
Sasa tuletee hiyo biblia ya tafsiri ya Roho Mtakatifu wa kanisa lako . Kwani Kuna makanisa kwa maelfu na kila kanisa linadai linaongozwa na Roho Mtakatifu.
Huyo Petro si ndiye Shetani au vipi tena ? Kumbe Shetani unamwamini ?
 
Sasa tuletee hiyo biblia ya tafsiri ya Roho Mtakatifu wa kanisa lako . Kwani Kuna makanisa kwa maelfu na kila kanisa linadai linaongozwa na Roho Mtakatifu.
Huyo Petro si ndiye Shetani au vipi tena ? Kumbe Shetani unamwamini ?
Mathayo 22:29
Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
 
Mathayo 22:29
Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
Mbona hiyo Aya inakupinga mwenyewe. .Yaani Yesu anasema Nakwenda kwa Mungu wangu na Mungu wenu , wewe unafahamu Yesu anajiendea mwenyewe. Anaposema , Mimi siwezi kufanya jambo lolote mwenyewe , wewe unasema opposite, kuwa anaweza kufanya chochote.
 
Kwani asingemtaja asingefika? Wangapi weshaenda huko bila kufa ya hivo? Neill Armstrong hakutaja Mungu bali mafanikio. Husomi nini?
 
Mathayo 22:29
Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


Umenukuu Mathayo 22:29, lakini hujaelewa hata hiyo aya.

Hiyo ndiyo hali yako wewe.

Biblia unayodai huijui inasema wazi:​

“Mungu si mwanadamu” (Hesabu 23:19) , “Baba ni mkuu kuliko mimi” (Yohana 14:28) , “Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu uliyemtuma” (Yohana 17:3)

Sasa jiulize: Nani hajui maandiko?

Yule anayesoma aya hizi wazi na kukubali, AU Yule anayezipuuza na kuleta hadithi za “nafsi na mwili”?

Hiyo aya uliyotumia inakurudia wewe mwenyewe unapotea kwa sababu hujui maandiko wala uweza wa Mungu.
 


“Unasema lazima ‘uokoke kwanza ndio uelewe’ hiyo ni njia ya kukwepa hoja, si kujibu maandiko.

Biblia haisemi ukweli unaeleweka kwa kundi fulani tu, bali inasema: ‘Neno lako ni ukweli’ (Yohana 17:17)

Ukweli hauhitaji upendeleo , unasimama wazi.

Kuhusu 1 Petro 2:22​

‘Yesu hakutenda dhambi…’ Sawa lakini kutokufanya dhambi hakumfanyi awe Mungu . Biblia pia inasema:
Yohana Mbatizaji alikuwa mwadilifu (Marko 6:20), Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu (Ayubu 1:1) . Jee nao ni Miungu?

Yesu bado ana Mungu juu yake​

Yesu Kristo anasema: ‘Mungu wangu na Mungu wenu’ (Yohana 20:17) . Hata bila “Roho Mtakatifu” wako, aya hii iko wazi kabisa , Yesu ana Mungu juu yake.

Yesu anatofautisha yeye na Mungu​

‘Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu uliyemtuma’ (Yohana 17:3), Hapa hakuna fumbo ni wazi kabisa.

Hoja yako ya “Roho Mtakatifu”​


Biblia inasema: ‘Jaribuni roho’ (1 Yohana 4:1). Sio kila anayedai ana Roho yuko sahihi . Hivyo hoja zako zinapimwa kwa maandiko si madai yako.

Kutokufanya dhambi hakumfanyi Yesu kuwa Mungu.


Biblia iko wazi: Yesu ana Mungu, Yesu ametumwa , Mungu ni mmoja

Wewe Unatumia maneno ya “uokoke kwanza” kuficha ukweli ambao maandiko yako yenyewe yanaonyesha wazi.
 
Chachu kidogo huchachua donge zima (1 Kor 5:6). Mjadala umeusitisha mwenyewe kwa sababu ya matusi yako. Mungu akusamehe bure, in Jesus Name
 
Chachu kidogo huchachua donge zima (1 Kor 5:6). Mjadala umeusitisha mwenyewe kwa sababu ya matusi yako. Mungu akusamehe bure, in Jesus Name

“Unanukuu 1 Wakorintho 5:6 lakini unaacha muktadha wake. Paulo alikuwa anakemea dhambi ya wazi ndani ya kanisa, si kutumia maandiko kujihesabia haki au kuwashambulia wengine. Biblia hiyo hiyo inasema wazi: ‘Usihukumu ili usihukumiwe’ (Mathayo 7:1).

Kama kweli unasimamia ukweli wa Mungu, basi anza na moyo wako mwenyewe. Maana imeandikwa: ‘Kwa nini unalitazama jicho la ndugu yako lenye kibanzi, lakini boriti iliyo jichoni mwako huiangalii?’ (Mathayo 7:3).

Imani siyo silaha ya kushambulia watu, bali ni mwanga wa kuongoza. Ukichagua kutumia maandiko vibaya, unajihukumu mwenyewe kwa kinywa chako. ‘Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa’ (Hosea 4:6).

Basi kama unataka kumtumikia Mungu kweli, acha kiburi na ujifunze kwanza—maana Mungu hapendezwi na maneno makali yasiyo na haki, bali moyo wa toba na kweli.”
Bado nakusubiri ukiri kwa ushahidi niliokuwekea kuwa Bwana Yesu si Mungu . Vyenginevyo lete ushahidi kupinga Aya nilizokuwekea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…