Rubani wa Pili wa Ndege-vita ya Marekani F-15 E aokolewa kwa Operation Kabambe huko Iran, IRGC waangamizwa!!!!!!

Hayo maneno mengi mnayojaribu kujiliwaza, mwanzo mlisema ni uwongo, haya hivyo kimsingi Makomando wameingia kikomando ndani ya Iran wakajichukulia watu wao, hii hata itabidi itengezewe movie kabisa.
Yeah itengenezwe movie kwamba makomondo wa Kimarekani walitolewa jasho na migambo na raia
 
Basij ndio wamehusika mzee acha uongo wa takiya kwenye uhalisia. Wameonyesha RT tayar
 
Kama USA wameweza kuwaokoa wanajeshi wao wawili Kwa wakati tofauti nahisi itakuwa kazi rahisi Sana kutoka kisiwa cha kharg ....Kazi ya kukiteka hili kisiwa imerahisishwa Sana baada ya kupata uzoefu kwenye uokoaji huu, bado Iran imeonesha udhaifu mkubwa Kwanza Kabisa jeshi Lao halina chemistry ya kufanya operations.

Vikosi vya IRGC makao mkuu Tehran na miji mingine hawana muunganiko wa mawasiliano na logistics za kivita pia hata mipamgo ya kivita imeshindikana Hadi kutumiwa wananchi wa kawaida waingie site kumtafutata.
Iran inarudi kwenye stone age
 
Nini kinawashinda Wamerekani kuufungua mlango bahari wa Hormuz?
 
Hakuna rubani aliyepatikana mpaka muda huu.

Iran ilishakanusha.
 
Kwani ni kipi kingine unaweza kuandika zaidi ya hivi?Wamarekani huwa hawapigwi,hupiga wao tu.Tunyamaze,ipo siku historia itaongea.
 
Una ushahidi gani na unajuaje labda wanajeshi wao waliogopa, wewe unafikiri kupambana na Delta Force ni mchezo.
 
Hivi kwani Irani pesa yao haina nguvu kubwa?

Kwanini sio atakaempata tutampa Dinari 78,397,482.29 na sio USD 60,000
Iran haina hela ni makaratasi tu, uchumi ulishajifia siku nyingi. Hela zote walikuwa wanapeleka kwenye silaha na kufadhili ugaidi katika mashariki ya kati.
 
Hapana sio kweli, wale wanajeshi wa IRGC walishikwa na kiwewe kwenda kwenye opereseheni hatari inayohusisha Delta Force ndio wakaona wawatoe kafara (cannon fodder) Basij ambao ni kama FFU tu.
 
Kuna watu wanaripoti unaweza ukadhani wapo iran, yaani wairan wangekuwa jf hata wao wangeshangaa ripoti za members humu.
 

Kuingia kwa wanajeshi ardhini mwa Iran ni ishara tosha kuwa Iran kazidiwa.

Licha ya kuzima internet. Ila wanajesh wa USA waliweza kuwasiliana na Ruban wao. Wakatambua alipo na wakamfuata kumchukua.
 
Bro Iran katoa taarifa kuwa ni basiji ndio walihusika na opereshen ya kumkamata
Nakwambia kwenye hali kama hiyo watu wanashikwa na unafikiri mchezo. Ingekuwa wanapambana na nchi size yao kama Turkiye au Iraq hao IRGC ndio wangekuwa wa kwanza kufika eneo la tukio wala wasingewatuma hao FFU wa Basij.
 
Iran wamezembea hapa.

Hawa marubani wote wawili ilitakiwa wawe mateka kitambo sana

nadhani haya mashambulizi yamedhoofisha mamlaka za Iran.

T14 Armata zitto junior Kichuguu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…