Ruby Aamua Kuacha Muziki wa Bongo Fleva na Kumrudia Yesu

Stara, ray c walikimbilia kule na wakashindwa kuishi maisha ya kiroho ikabidi warudi walikotoka. Sasa yeye ataweza? Ni mzee makassy na chidimule tu ndio tunaona wamedumu muda mrefu wokovuni tangu watoke kwenye miziki ya kidunia. Mzee yusuph alikimbilia kwenye uislam wake ila baadaye akarejea kwenye taarabu zake za kidunia, snura naye alikimbilia kwenye uislam wake hatusikii kama amerejea kuimba miziki ya kidunia
 
Ni miaka mingi anaimba.Nilikuwa namuona akiwa TOT nadhani kuanzia mwaka 1988 hivi.Hiyo "1960" ni kunogeaha tu.
Kitambo sana, atakwambia yeye kipaji hakizeeki. Hapo nimestushwa na wewe kwanza kabla yake, yaani mzee wa miaka 80 upo humu unakinukisha kama vijana under 25😁¡
 
Kitambo sana, atakwambia yeye kipaji hakizeeki. Hapo nimestushwa na wewe kwanza kabla yake, yaani mzee wa miaka 80 upo humu unakinukisha kama vijana under 25😁¡
Tunashindana na watoto wetu huku tumevaa kininja.Mola atubariki sana!
 
Nje ya mada kidogo!

Ruby ni mwanamziki mzuri, napenda nyimbo zake.

Japo sivutiwi naye kimapenzi.

Ningekuwa na uwezo ningemuoa maua sama, yule ni wife material kabisa.

Au kama Kwa kula Bata basi Linah Sanga anamaliza shida zote .
Sawa:...'ila badooo siyo mbaya..."By Ruby..
 
Vijana wengi humu hamnazo!
Kweli na hamnazo wa aina nyingi tu;
-Akili
-Pesa
-Aibu
-Nguvu za kiume
Ni nyie tu kuchagua penye ahueni. Sasa huyu yeye ni hamnazo wa nini labda !
 
Sisi ambao tunamjua vizuri hatushtuki.
Ruby ni church girl Tangu secondary. Enzi izo akisoma Salma kikwete sec, alikua akiimbisha kusifu na kuabudu kipindi cha dini.

Kwaio, tunaomjua tunasema KARUDI KUNDINI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…