Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Inasikitisha sana kusoma kwamba Zaidi ya Vijijini 23 Wilayani Rufiji vilivyopo kwenye blonde la mto Rufiji Vimekumbwa na Mafuriko Makubwa ya maji kutoka bwawa la umeme la Nyerere.

Vijiji hivyo viko kwenye kata 12 Zenye kaya zaidi ya 1,000 ambapo makazi,mashamba,mazao na Mali nyingine vimegaribiwa vibaya na Mafuriko hayo.

Ikumbukwe njia ya mwongo Huwa ni fupi.Wakati wa Ujenzi wa bwawa hili tuliambiwa pamoja na mambo mengine eti ujenzi wake utadhibi Mafuriko ya mara Kwa mara huko lower Rufiji basin lakini imekuwa kinyume chake kwani Mafuriko ndio yameongezeka na Haki kuwa mbaya zaidi maana maji yanakuja Kwa Wingi na Kasi kubwa.

Ni vyema ikaeleweka kwamba kabla ya kufanya mradi wowote ni vyema athari Kwa mazingira ikafanyika ila Kwa bwawa hili inaelekea jambo hili lilipuuzwa.

Ikumbukwe kwamba miradi yeyote iwe ya kiuchumi au kijamii Huwa inalenga kuleta ustawi Kwa jamii husika ila ikiwa kinyume chake haifai au njia mbadala lazima zitafutwe.

Snapinsta.app_434647754_18322163737193701_2229852365959623150_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434492425_18322163719193701_2382750166466055807_n_1080.jpg

Snapinsta.app_434658403_18322163689193701_8680693180331670746_n_1080.jpg

---========

MCHENGERWA ATOA MIL.40/- KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Na Projestus Binamungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh.milioni 40 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko ya maji, yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na wakazi hao mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, Waziri Mchengerwa amesema analazimika kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuwatia moyo wakazi hao kurejea shambani kulima upya baada ya mazao yao kusombwa na mafuriko hayo.

“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado imejitokeza, tuendelee kuwa na Imani kwamba mradi ukikamilika uwenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” alisema Waziri Mchengerwa.

Snapinsta.app_434599331_18322163680193701_710138793358704332_n_1080.jpg


Aliongeza kuwa “ Ninafahamu fika namna wakazi wa Rufiji mlivyokuwa mmelima kwelikweli mwaka huu, ninaomba turejee shambani tulime tena vilevile kwa kiwango kikubwa, mimi ninamkabidhi Mkuu wa wilaya shilingi milioni 40 kwa kuanzia kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu ili turejee shambani tupande tena tusije kufa kwa njaa.”

Alikadhalika Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa taasisi na mashirika ya misaada ya kibinadamu Pamoja na wasamalia wema kuguswa na hali ya Warufiji kwa kuwashika mkono kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inaendelea na ufuatiliaji na tathimini ya athari za mafuriko hayo kwa ujumla.

“Ukweli niseme kiasi hiki cha milioni 40 nilikuwa nimekidunduliza kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa na futari ya Pamoja katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kama tunavyofanya kila mwaka, lakini kwa hali hii ya mafuriko niseme tu kwamba futari si kitu nalazimika kutoa kiasi hiki kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na nitaenda kuwaomba marafiki zangu wanichangie angalau tufikishe milioni …..

My Take
Kwa hili la Rufiji, Serikali ihamishe Wananchi na iwalipe fidia kama inavyofanya Ngorongo Kwa Masai Kwa sababu maslahi na Haki zao zilikiukwa Kwa kutofanya EIA kama sheria za Nchi na Kimataifa zinavyotaka.

Tunapenda Umeme ila sio Kwa utaratibu huu.

Pia soma:
 
Ku Sacrifice Vijiji kadhaa kwa ajili ya Nchi kupata Umeme wa uhakika mimi naona kwa mtazamo wangu sio mbaya ila tu wahamishwe na walipwe fidia yao bila kudhulumiwa hata shilingi.
Sio mbaya kwasbabu huathiriki.
 
Back
Top Bottom