Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

hao wahame tu kwa usalama wao, wapewe fidia wasepe...bwawa lenyewe tunasikia mara lina ufa kibao....wahame tu wataoga sana hapo
 
Tulionya tukapuuzwa
Hii changamoto tuipokee positively. Umeme tunautaka kama taifa, kwa ustawi wa jamii nzima wakiwemo hao wanaokumbwa na yatokanayo na mradi huo wa umeme. Sasa basi jukumu la custodian wa jamii kuhakikisha usalama na ustawi wa wahanga.
-kuielimisha jamii juu ya madhara ya mradi huo kwenye maeneo yao
-kuhamisha wakaaji wa maeneo hayo na kuwasaidia kuanzia makaazi mapya sehemu salama.
-kutoruhusu shughuli za kudumu kwenye maeneo hayo.
-............…….….
 
Umesha ambiwa hilo ni bonde bado unaenda kujenga, mtoa mada huna akili kama hao wanakijiji waliojenga bondeni.
Hivi umefanya tathmini kujua hao watu wapo hapo tokea lini? kuna mambo tusiyaangalie kiushabiki kama walikuja baada ya Bwawa kujengwa sawa wanamakosa ila kama Bwawa limejengwa wao walikuwa hapo toka zamani basi kuna swala la kijografia hapo ule mto kama unajua vyema huwa unapotea njia sana
Maji hayapandi mlima shehe, hao wamejenga bondeni.
Najua nachokisema ndugu maana nimeishi huko ndio maana nasema hivyo.
 
Amesema tulifukiri tatizo litakwisha maana yake lilikuwepo , na sio matokeo ya mradi. Pili amesema labda ukikamilika tatizo litakwisha
Acha ujinga,ungesoma hata mada uelewe.

Tatizo lilikuwepo na mojawapo ya sababu za kujenga bwawa tuliambiwa litadhibiti Mafuriko badala yake limeongeza Ukubwa wa tatizo.

Yote hii ni Kwa sababu ya kukurupuka ,wangefanya EIA wangejua namna Bora ya kulijenga Ili li save purpose zote.
 
Yule mzee kila alipotia Mkono wake ni mabalaa, nuksi na majanga tu.
Shida yake ni mkurupukaji,hakuna jambo amewahi fanya Kwa ufanisi.

Hata mradi wa daraja la Busisi haukufuata utaratibu wa Manunuzi matokeo yake umekaa Rushwa
 
Limetengenezwa tatizo ili mradi ufe
 
Back
Top Bottom