Inasikitisha sana kusoma kwamba Zaidi ya Vijijini 23 Wilayani Rufiji vilivyopo kwenye blonde la mto Rufiji Vimekumbwa na Mafuriko Makubwa ya maji kutoka bwawa la umeme la Nyerere.
Vijiji hivyo viko kwenye kata 12 Zenye kaya zaidi ya 1,000 ambapo makazi,mashamba,mazao na Mali nyingine vimegaribiwa vibaya na Mafuriko hayo.
Ikumbukwe njia ya mwongo Huwa ni fupi.Wakati wa Ujenzi wa bwawa hili tuliambiwa pamoja na mambo mengine eti ujenzi wake utadhibi Mafuriko ya mara Kwa mara huko lower Rufiji basin lakini imekuwa kinyume chake kwani Mafuriko ndio yameongezeka na Haki kuwa mbaya zaidi maana maji yanakuja Kwa Wingi na Kasi kubwa.
Ni vyema ikaeleweka kwamba kabla ya kufanya mradi wowote ni vyema athari Kwa mazingira ikafanyika ila Kwa bwawa hili inaelekea jambo hili lilipuuzwa.
Ikumbukwe kwamba miradi yeyote iwe ya kiuchumi au kijamii Huwa inalenga kuleta ustawi Kwa jamii husika ila ikiwa kinyume chake haifai au njia mbadala lazima zitafutwe.
View attachment 2953581
---
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh40 milioni kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wilayani Rufiji, ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko yaliyotokana na maji yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP).
Tathimini ya awali imebaini kuharibiwa kwa nyumba 58 na wakazi 951 wameondolewa katika maeneo yao, huku zaidi ya hekta 28,374.74 za mazao ya kilimo na bishara ikiwamo mahindi, mpunga, ufuta na migomba vikiathiriwa na mafuriko hayo.
Waziri Mchengerwa ambaye pia ni mbunge wa Rufiji mkoani Pwani, pia amefanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo.
“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado hali hii imejitokeza.
"Tuendelee kuwa na imani kwamba mradi ukikamilika huenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” amesema Waziri Mchengerwa.
Mchengerwa ameyasema hayo jana Jumanne Aprili 2, 2024.
Chanzo: Mwananchi
My Take
Kwa hili la Rufiji, Serikali ihamishe Wananchi na iwalipe fidia kama inavyofanya Ngorongo Kwa Masai Kwa sababu maslahi na Haki zao zilikiukwa Kwa kutofanya EIA kama sheria za Nchi na Kimataifa zinavyotaka.
Tunapenda Umeme ila sio Kwa utaratibu huu.
View: https://www.instagram.com/p/C5Tw0qNNsU8/?igsh=MmlnNndieDNvdzc0