Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Kwani ni mara ya kwanza vijiji hivyo kukumbwa na mafuriko? Wenyewe wamasema walidhani ujenzi wa Bwawa ungekuwa suluhu ya matatizo ya mafuriko yanayowakumba mara kwa mara so kwa kauli hiyo ni wazi kuwa si mara ya kwanza na hivyo tusihusishe janga hilo na Bwawa la Nyerere. Naona vita dhidi ya hilo Bwawa bado inaendelea!
Na hao wazungu wanaowazungumzia hata siku moja hawatapenda kuona tunajitosheleza/tunajitegemea. Wanataka kuona tunaishi maisha ya ombaomba. Ndio hao sasa wanatuletea mambo ya kipuuzi kama LGBTQ.
 
Pamoja na umeme kwani bwawa lililenga nini Kingine tofauti na kudhibiti Mafuriko?

Limeongeza Mafuriko Kwa sababu EIA haikufanyika,hakuna excuses hapo
EIA ilifanyika kiongozi... Na ilitoa way forward kwa changamoto zinazotarajiwa.....
 
Ukiona zaidi ya miaka 50 kitu hakijafanyika afu we unakuja kifanya jitafakari sana
Kwa hiyo hayo mafuriko ya watu au wakazi 951 ndiyo yangefanya tusijenge bwawa, ingekuwa wewe ni raisi usingejenga bwawa kisa tuu watu 951 ?!
Simple tuu lipa fidia hamisha watu hao, peleka mbali kabisa huko. Hilo eneo la mafuriko acha wazi au tafuta kitu kingine cha tija wekeza hapo, sehemu Nyingine weka mashamba ya umwagiliaji walime mpunga wa kutosha kushusha bei ya mpunga na mazao mengine jiji la dar es salaam upunguze gharama za maisha.
Bwawa li a faida kubwa mnooo tena sanaa kuliko hata hiyo hasara ya hao wakazi 951 sijui, ni suala la hao watu kulipwa fidia na kuondoka hilo eneo kodi si tunalipa watz, shida iko wapi sasa ?!
Hao hawaku jenga bwawa miaka yote hiyo 51 sababu ya kukosa hela au UOGA.
ILA MWAMBA NI MMOJA TUU MPAKA SASA HIVI HATA KAMA AMESHA KUFA NAYE NI MAGUFULI.
Unajua ni miradi mingapi mingine angejenga yule mwamba ambayo watangulizi wake waliogopa sababu ya mabepari kama angekuwa hai mpaka sasa hivi ?!
 
Inasikitisha sana kusoma kwamba Zaidi ya Vijijini 23 Wilayani Rufiji vilivyopo kwenye blonde la mto Rufiji Vimekumbwa na Mafuriko Makubwa ya maji kutoka bwawa la umeme la Nyerere.

Vijiji hivyo viko kwenye kata 12 Zenye kaya zaidi ya 1,000 ambapo makazi,mashamba,mazao na Mali nyingine vimegaribiwa vibaya na Mafuriko hayo.

Ikumbukwe njia ya mwongo Huwa ni fupi.Wakati wa Ujenzi wa bwawa hili tuliambiwa pamoja na mambo mengine eti ujenzi wake utadhibi Mafuriko ya mara Kwa mara huko lower Rufiji basin lakini imekuwa kinyume chake kwani Mafuriko ndio yameongezeka na Haki kuwa mbaya zaidi maana maji yanakuja Kwa Wingi na Kasi kubwa.

Ni vyema ikaeleweka kwamba kabla ya kufanya mradi wowote ni vyema athari Kwa mazingira ikafanyika ila Kwa bwawa hili inaelekea jambo hili lilipuuzwa.

Ikumbukwe kwamba miradi yeyote iwe ya kiuchumi au kijamii Huwa inalenga kuleta ustawi Kwa jamii husika ila ikiwa kinyume chake haifai au njia mbadala lazima zitafutwe.

View attachment 2953636
View attachment 2953637
View attachment 2953638
---========

MCHENGERWA ATOA MIL.40/- KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Na Projestus Binamungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh.milioni 40 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko ya maji, yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na wakazi hao mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, Waziri Mchengerwa amesema analazimika kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuwatia moyo wakazi hao kurejea shambani kulima upya baada ya mazao yao kusombwa na mafuriko hayo.

“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado imejitokeza, tuendelee kuwa na Imani kwamba mradi ukikamilika uwenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” alisema Waziri Mchengerwa.
View attachment 2953643
Aliongeza kuwa “ Ninafahamu fika namna wakazi wa Rufiji mlivyokuwa mmelima kwelikweli mwaka huu, ninaomba turejee shambani tulime tena vilevile kwa kiwango kikubwa, mimi ninamkabidhi Mkuu wa wilaya shilingi milioni 40 kwa kuanzia kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu ili turejee shambani tupande tena tusije kufa kwa njaa.”

Alikadhalika Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa taasisi na mashirika ya misaada ya kibinadamu Pamoja na wasamalia wema kuguswa na hali ya Warufiji kwa kuwashika mkono kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inaendelea na ufuatiliaji na tathimini ya athari za mafuriko hayo kwa ujumla.

“Ukweli niseme kiasi hiki cha milioni 40 nilikuwa nimekidunduliza kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa na futari ya Pamoja katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kama tunavyofanya kila mwaka, lakini kwa hali hii ya mafuriko niseme tu kwamba futari si kitu nalazimika kutoa kiasi hiki kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na nitaenda kuwaomba marafiki zangu wanichangie angalau tufikishe milioni …..

My Take
Kwa hili la Rufiji, Serikali ihamishe Wananchi na iwalipe fidia kama inavyofanya Ngorongo Kwa Masai Kwa sababu maslahi na Haki zao zilikiukwa Kwa kutofanya EIA kama sheria za Nchi na Kimataifa zinavyotaka.

Tunapenda Umeme ila sio Kwa utaratibu huu.

View: https://www.instagram.com/p/C5S-mCZiN5p/?igsh=aWpqb2Vkbzl3cmFn

Mbona kama sio Tanzania?

Yaani wanafungulia maji makusudi yakalete mafuriko? Si wangewajulisha tu wananchi wahame kabisa, kwa hali hiyo nadhani wafanye hao wakazi wahame kbs ukanda huo vinginevyo tutakuja kusikia maafa makubwa zaidi.
 
Mbona kama sio Tanzania?

Yaani wanafungulia maji makusudi yakalete mafuriko? Si wangewajulisha tu wananchi wahame kabisa, kwa hali hiyo nadhani wafanye hao wakazi wahame kbs ukanda huo vinginevyo tutakuja kusikia maafa makubwa zaidi.
Haikuwa makusudi,mamitambo lijaa matope na ndio chanzo Cha umeme kukata Nchi nzima 😆😆
 
We ni wa kupuuzwa, chuki uliyonayo ni kubwa mno mpaka inakutoa akili. Kwani ndo mara ya kwanza vijiji hivyo kukumbwa na mafuriko? Faida ya Bwawa huwezi kulinganisha na hasara itokanayo na mafuriko hayo hata robo. Chuki hupunguza uwezo wa kufikiri.
Endelea kumuabudu, lkn ndo kisha kufa na mtambo umezimwa
 
kwahiyo kama hizo athari zisingpuuzwa ndio ingekuwaje? Si mlisema miti ikikatwa mvua hazitanyesha, haya , maji hayo hapo sasa
 
Na hii ndiyo imesababisha mtambo kuzimwa. Ccm huwa wanakurupuka sana.

Jiwe alikuwa hasmbiliki mshenzi yule. Yako wapi sasa? Legacy ziiiiii!!
Usiwe kama kahaba wewe, wallipozima ni Kidatu..
 
Ipi hiyo way forward?
Mradi mkubwa kama huo haiwezekani ufanyike bila EIA..... Final report huwa na mapendekezo mbalimbali. Ambapo katika situation kama hiyo Evacuation, Dredging construction of Dykes etc as a way forward.....
 
Hii utaambiwa ni fake news
Mafuriko kumbe yalikuwepo kabla.
Kwa maana hiyo bwawa la JHNPP halikusababisha mafuriko na kwamba bwawa ni dogo mpaka maji yameongezeka na kusambaa vijijini.
Suluhisho kumbe ilikuwa ni kujenga bwawa kubwa zaidi ya kuhifadhi maji kwa muda mrefu au kujenga jengine litalotumia maji mpaka kusiwe na mafuriko.
Sasa lawama iko wapi?.Huyo mto una fursa kubwa ya kumaliza tatizo la umeme na kuzalisha wa ziada ukauzwa kote Afrika.
 
... INATAKIWA KAZI YA ZIADA KUDHIBITI MAFURIKO KWA KUJENGA MATUTA-VIZUIZI KARIBU NA KILA MAKAZI YA WATU, MAENEO UNAPOPITA MTO HUO!
FIDIA KWA WAATHIRIKA NI MUHIMU INAPODHIBITIKA KUWA MADHARA YALIYOTKEA SIO NATURAL, YAANI NI YALIYOTOKANA NA UZALISHAJI WA UMEME!

NB: MAFURIKO RUFIJI SIO KITU KIGENI, MAANA HATA WAKATI BWAWA HALIJAKAMILIKA,MIAKA YA KARIBUNI KULIKUWA NA MAFURIKO KAMA HAYO, AU HATA ZAIDI !
... JE NI KWELI HAYA MAFURIKO YA SASA NI KWA SABABU YA UZALISHAJI WA UMEME? ... HAIINGII AKILINI KWAMBA KILA UKIZALISHWA UMEME BASI KUTOKEE MAFURIKO, IKIWA NA MAANA MAJI YA MTO YANAZIDI KIASI CHA KAWAIDA! ... MAANA KAMA NI KWELI UZALISHAJI UMEME UNATOA MAJI YANAYOSABABISHA MAFURIKO BASI HATA HILO BWAWA HALIWEZI KUTUNZA MAJI YA KUZALISHA UMEME MWAKA MZIMA!
💥💥💥 ... ISIJE IKAWA MVUA TU ZIMEZIDI HUKO BARA NA HILO LA MAJI YA KUZALISHA UMEME LIKAWA TU NYONGEZA NDOGO!
 
Back
Top Bottom