Rufiji: Vijiji 23 vimekumbwa na mafuriko makubwa kutoka Bwawa la Umeme la JNHPP. Je, Tathmini ya athari kwa mazingira ilipuuzwa kabla ya ujenzi?

Mradi mkubwa kama huo haiwezekani ufanyike bila EIA..... Final report huwa na mapendekezo mbalimbali. Ambapo katika situation kama hiyo Evacuation, Dredging construction of Dykes etc as a way forward.....
Mbona bwawa linaleta Mafuriko kama hayo yalifanyika?
 
Moja ya sababu za kujengwa Kwa bwawa ni kudhibiti Mafuriko downstream lakini Sasa bwawa limeongeza Mafuriko.

Hii ni matokeo ya kupuuza EIA,Sasa hivi watalazimika kuhamishia watu na maeneo ambayo yangefaa kwa.kilimo.kufa Kwa sababu bwawa limegeuka acceleror na sio controller

Hata mimi navyojua kwamba Dams ni moja ya Flood Control sasa inakuwaje effect imekuwa kubwa baada ya kujenga JNHPP? Kuna kitu hawakuzingatia hao mainjinia ,wangetafuta kampuni iliyojenga TVA - Tennessee Valley Authority.
 
Mbona bwawa linaleta Mafuriko kama hayo yalifanyika?
Mafuriko hayakuwa ni malengo ya mradi.... Lakini nisehemu ya matokeo ambayo hayakutarajiwa.... Au kinga haikutiliwa mkazo..... Lakini changamoto hiyo haiondoi umuhimu wa mradi....
 
Inasikitisha sana kusoma kwamba Zaidi ya Vijijini 23 Wilayani Rufiji vilivyopo kwenye blonde la mto Rufiji Vimekumbwa na Mafuriko Makubwa ya maji kutoka bwawa la umeme la Nyerere.

Vijiji hivyo viko kwenye kata 12 Zenye kaya zaidi ya 1,000 ambapo makazi,mashamba,mazao na Mali nyingine vimegaribiwa vibaya na Mafuriko hayo.

Ikumbukwe njia ya mwongo Huwa ni fupi.Wakati wa Ujenzi wa bwawa hili tuliambiwa pamoja na mambo mengine eti ujenzi wake utadhibi Mafuriko ya mara Kwa mara huko lower Rufiji basin lakini imekuwa kinyume chake kwani Mafuriko ndio yameongezeka na Haki kuwa mbaya zaidi maana maji yanakuja Kwa Wingi na Kasi kubwa.

Ni vyema ikaeleweka kwamba kabla ya kufanya mradi wowote ni vyema athari Kwa mazingira ikafanyika ila Kwa bwawa hili inaelekea jambo hili lilipuuzwa.

Ikumbukwe kwamba miradi yeyote iwe ya kiuchumi au kijamii Huwa inalenga kuleta ustawi Kwa jamii husika ila ikiwa kinyume chake haifai au njia mbadala lazima zitafutwe.

View attachment 2953636
View attachment 2953637
View attachment 2953638
---========

MCHENGERWA ATOA MIL.40/- KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Na Projestus Binamungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh.milioni 40 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko ya maji, yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na wakazi hao mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, Waziri Mchengerwa amesema analazimika kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuwatia moyo wakazi hao kurejea shambani kulima upya baada ya mazao yao kusombwa na mafuriko hayo.

“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado imejitokeza, tuendelee kuwa na Imani kwamba mradi ukikamilika uwenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” alisema Waziri Mchengerwa.

View attachment 2953643

Aliongeza kuwa “ Ninafahamu fika namna wakazi wa Rufiji mlivyokuwa mmelima kwelikweli mwaka huu, ninaomba turejee shambani tulime tena vilevile kwa kiwango kikubwa, mimi ninamkabidhi Mkuu wa wilaya shilingi milioni 40 kwa kuanzia kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu ili turejee shambani tupande tena tusije kufa kwa njaa.”

Alikadhalika Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa taasisi na mashirika ya misaada ya kibinadamu Pamoja na wasamalia wema kuguswa na hali ya Warufiji kwa kuwashika mkono kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inaendelea na ufuatiliaji na tathimini ya athari za mafuriko hayo kwa ujumla.

“Ukweli niseme kiasi hiki cha milioni 40 nilikuwa nimekidunduliza kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa na futari ya Pamoja katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kama tunavyofanya kila mwaka, lakini kwa hali hii ya mafuriko niseme tu kwamba futari si kitu nalazimika kutoa kiasi hiki kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na nitaenda kuwaomba marafiki zangu wanichangie angalau tufikishe milioni …..

My Take
Kwa hili la Rufiji, Serikali ihamishe Wananchi na iwalipe fidia kama inavyofanya Ngorongo Kwa Masai Kwa sababu maslahi na Haki zao zilikiukwa Kwa kutofanya EIA kama sheria za Nchi na Kimataifa zinavyotaka.

Tunapenda Umeme ila sio Kwa utaratibu huu.

View: https://www.instagram.com/p/C5S-mCZiN5p/?igsh=aWpqb2Vkbzl3cmFn

Kwani hakukufanyika tathimini ya athari ya mazingira (environmental impact assessment (EIA))?
Kwa mradi mkubwa hivyo na ambao unaathari za moja kwa moja kwenye mazingira lazima EIA ifanyike. Pili hao wananchi hawakupewa mrejesho wa tathmini?! Maana kama walipewa mrejesho lazima waliambiwa bwawa litafika wapi, na kwa hiyo waathirika waondeke kabla utekelezaji haujaanza.
Na kama hawakuambiwa, kwa nini?
 
Hata mimi navyojua kwamba Dams ni moja ya Flood Control sasa inakuwaje effect imekuwa kubwa baada ya kujenga JNHPP? Kuna kitu hawakuzingatia hao mainjinia ,wangetafuta kampuni iliyojenga TVA - Tennessee Valley Authority.
Mvua mwaka huu ni nyingi sana kupitanl kiasi, pita hapo ruvu darajani au wami dakawa ujionee, huko malinyi na mlimba,ifakara hakupitiki, ni mafuriko mwanzo mwisho,kwa hiyo bwawa sio sababu bali mvua ni nyingi
 
Sawa mkuu.
 
Mambo ya kulazimisha vitu kwa lengo la kutafuta sifa na 10% haya ndiyo matokeo yake.
 
Kwahiyo zile disasters zinazotokea kwenye Vinu vya nuclear Urusi na Japan na kuleta madhara Kwa raia, inamaana na wao hawakufanya tathimini.
Mwaka 2000 kemikali za viwandani zilingia kwenye vyanzo vya maji huko minnesota, USA na kuathiri raia zaidi ya 170000 na wao kumbe wajinga kama sisi hawakufanya tathimini.
 
Kwa mtazamo wangu naona hao wanavijiji walipwe fidia na kuhamishwa kutoka eneo hilo. Faida za mradi huu ni kubwa sana ukifananisha na hivyo vijiji 23. Wapewe chao wahamie sehemu nyingine mradi uendelee..

Tatizo la umeme ni kubwa na mradi huu utasaidia sekta nyingi sana za uchumi tofauti na watu tunavyosema humu kuhusu hivyo vijiji.

Hakuna maemdeleo bila side effects.
 
Hii ndio Tanzania Chiembe wa CCM analia na mafuriko ya Rufiji huku makamanda wa Chadema wakimshangilia kiumbea Zaidi

Ni Chiembe na Chadema waliolalamika Sana kwamba Rufiji itakuwa na Ukame Baada ya Magufuli kukata Miti milioni 20 na kujenga Bwawa la umeme

Makamanda ni Malalamuko FC 🐼

Mlale Unono 😄😄
 
Mvua mwaka huu ni nyingi sana kupitanl kiasi, pita hapo ruvu darajani au wami dakawa ujionee, huko malinyi na mlimba,ifakara hakupitiki, ni mafuriko mwanzo mwisho,kwa hiyo bwawa sio sababu bali mvua ni nyingi
Miaka ya nyuma mafuriko yalikuwa yanatokea huko rufiji kabla hata ya hilo bwawa kujengwa. Kwa mvua zilizoanza kunyesha novemba mwaka Jana hadi sasa ni nyingi sana (Elnino) na pengine kilichochelewesha haya mafuriko huko rufiji ni ujazaji maji kwenye bwawa hilo vinginevyo mafuriko yangetokea mapema kabisa huko rufiji.
 
Inasikitisha sana kusoma kwamba Zaidi ya Vijijini 23 Wilayani Rufiji vilivyopo kwenye blonde la mto Rufiji Vimekumbwa na Mafuriko Makubwa ya maji kutoka bwawa la umeme la Nyerere.

Vijiji hivyo viko kwenye kata 12 Zenye kaya zaidi ya 1,000 ambapo makazi,mashamba,mazao na Mali nyingine vimegaribiwa vibaya na Mafuriko hayo.

Ikumbukwe njia ya mwongo Huwa ni fupi.Wakati wa Ujenzi wa bwawa hili tuliambiwa pamoja na mambo mengine eti ujenzi wake utadhibi Mafuriko ya mara Kwa mara huko lower Rufiji basin lakini imekuwa kinyume chake kwani Mafuriko ndio yameongezeka na Haki kuwa mbaya zaidi maana maji yanakuja Kwa Wingi na Kasi kubwa.

Ni vyema ikaeleweka kwamba kabla ya kufanya mradi wowote ni vyema athari Kwa mazingira ikafanyika ila Kwa bwawa hili inaelekea jambo hili lilipuuzwa.

Ikumbukwe kwamba miradi yeyote iwe ya kiuchumi au kijamii Huwa inalenga kuleta ustawi Kwa jamii husika ila ikiwa kinyume chake haifai au njia mbadala lazima zitafutwe.

View attachment 2953636
View attachment 2953637
View attachment 2953638
---========

MCHENGERWA ATOA MIL.40/- KUSAIDIA WANANCHI WA RUFIJI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Na Projestus Binamungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji mkoani Pwani Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh.milioni 40 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu kwa zaidi ya wakazi 1,000 wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Rufiji ambao mali, mashamba na makazi yao yameathiriwa na mafuriko ya maji, yaliyofunguliwa kutoka bwawa la uzalishaji umeme la Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na wakazi hao mara baada ya kufanya ziara ya kukagua athari ya mafuriko hayo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, Waziri Mchengerwa amesema analazimika kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuwatia moyo wakazi hao kurejea shambani kulima upya baada ya mazao yao kusombwa na mafuriko hayo.

“Hili ni janga letu sote mimi na nyinyi, tuliamini kwamba ujenzi wa JNHPP utakuwa mkombozi wa mafuriko ambayo yamekuwa yanatukumba mara kwa mara lakini kwa bahati mbaya bado imejitokeza, tuendelee kuwa na Imani kwamba mradi ukikamilika uwenda changamoto hii ikawa imetatuliwa” alisema Waziri Mchengerwa.

View attachment 2953643

Aliongeza kuwa “ Ninafahamu fika namna wakazi wa Rufiji mlivyokuwa mmelima kwelikweli mwaka huu, ninaomba turejee shambani tulime tena vilevile kwa kiwango kikubwa, mimi ninamkabidhi Mkuu wa wilaya shilingi milioni 40 kwa kuanzia kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mbegu ili turejee shambani tupande tena tusije kufa kwa njaa.”

Alikadhalika Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa taasisi na mashirika ya misaada ya kibinadamu Pamoja na wasamalia wema kuguswa na hali ya Warufiji kwa kuwashika mkono kwa namna moja au nyingine katika kipindi hiki ambacho serikali ya wilaya inaendelea na ufuatiliaji na tathimini ya athari za mafuriko hayo kwa ujumla.

“Ukweli niseme kiasi hiki cha milioni 40 nilikuwa nimekidunduliza kutoka kwenye mshahara wangu kwa ajili ya kuhakikisha tunakuwa na futari ya Pamoja katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kama tunavyofanya kila mwaka, lakini kwa hali hii ya mafuriko niseme tu kwamba futari si kitu nalazimika kutoa kiasi hiki kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na nitaenda kuwaomba marafiki zangu wanichangie angalau tufikishe milioni …..

My Take
Kwa hili la Rufiji, Serikali ihamishe Wananchi na iwalipe fidia kama inavyofanya Ngorongo Kwa Masai Kwa sababu maslahi na Haki zao zilikiukwa Kwa kutofanya EIA kama sheria za Nchi na Kimataifa zinavyotaka.

Tunapenda Umeme ila sio Kwa utaratibu huu.

Pia soma - Mkuu wa Wilaya ya Rufiji: Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere limepunguza athari za mafuriko Rufiji
Ripoti hii inaeleza kwamba hata Bwawa kubwa kama hili haiwezi kuondoa kabisa Magufuli Kwa sababu , watu wanatabia ya kuja kujenga karibu ya Bwawa mvua zinapopungua , hivyo mvua zinapo nyesha kama za Mwaka huu.

World Wildlife Fund
https://files.worldwildlife.org › ...PDF
THE FACTS AND RISKS OF BUILDING STIEGLER'S GORGE HYDROPOWER ...
 
Back
Top Bottom