TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Unajua wenzetu wa nchi zilizoendelea walishaona ujinga kama huu ndiyo maana wakaweka mtu anayeitwa msemaji mkuu. Sasa hapa kwetu hawa waandishi uchwara wanavamia na kumhoji mtu yoyote na wahojiwa walivyo wajinga wanaongea hovyo.
Wise
 
Watanzania kwa ujumla wetu tumejumuika katika tukio la kuomboleza kifo cha mkurugenzi wa Clouds media, Ruge Mutahaba. Nawapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Tukiweka unafiki pembeni, tukio la kifo cha Ruge limekuzwa mnoo. Ruge hakuwa mtu maarufu sana Tanzania (japokuwa amefanya mambo mengi makubwa), hakuwa mwema sana na wala hakuwa mtu muhimu sana kwa watanzania walio wengi.

Kila kitu kuhusu maombolezo ya msiba wake kinaonekana kupangwa, kuratibiwa na hata kugharamiwa kwa karibu mnoo na serikali. Tunaambiwa hata tangazo la kifo chake ilibidi itifaki ya ikulu itumike ili rais atangaze kifo chake. Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu naye waliopata taarifa za kifo chake waliambiwa wakae kimya kwanza (walifichwa taarifa?) mpaka rais alipotangaza.

Sote tunajua Ruge alikuwa ni mfanyabiashara na kila alichokuwa akikifanya kwenye jamii kilikuwa kimelenga biashara zake kwa 100% hata kama alikuwa akikifunika kwa koti la kijamii. Waliowahi kufanya kazi naye wanajua hilo, na hakuwa na mchezo mchezo katika kufanya biashara zake. Huo ndio ukweli.

Watanzania wote wanalazimishwa kusema mema ya Ruge, kushiriki kuomboleza kifo cha Ruge na kulipia gharama za mazishi yake kama msiba wa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Sidhani kama jambo hili lina afya sana kwa taifa letu huko tuendako, maana nadhani kila mtanzania angetamani naye siku moja ndugu, jamaa au rafiki yake atakayefariki njia hii hii itumike kwake ili kufuta majonzi na kumpa faraja.

Bado sijajua kwanini hili la kufa na kuzikwa kwa Ruge limelazimishwa kuwa tukio kubwa la kitaifa, lazima kuna sababu, nadhani huenda ipo siku tutaambiwa kinagaubaga.

Ruge hayupo tena, tuliompenda na waliomchukia tumeendea kuwepo, tukishamaliza kumzika turudi na kuendelea na maisha yetu.
 
Hapa ndipo ambapo mwili wa mpendwa wetu, Ruge Mutahaba utapumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Kijijini kwao Kiziru-Kabale, Bukoba, kesho Jumatatu.
 
Hapa ndipo ambapo mwili wa mpendwa wetu, Ruge Mutahaba utapumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Kijijini kwao Kiziru-Kabale, Bukoba, kesho Jumatatu.
 
Watu waliolikuza hawana taswira nzuri kwenye jamii, hivyo wametumia tukio hilo kutaka kujionyesha ni watu wema. Kwa sasa kuzikana kunaangalia itikadi, hivyo huyo kwakuwa hakuwa wa siasa za majukwaani ndio ametumika kutakatishia nyota zao.
 
Wenzio wanajuana......

Tukio la kifo cha "mwenzao" huyo kwao ni "ibada" yao muhimu kuliko unavyofikiri......

They know exactly hata utaratibu wa kufa kwake. Kulia kwao kote huko ilikuwa ni machozi ya mamba ya kuwafanya wasio na ufahamu wa mambo haya wapumbazike na waamini kweli kuwa kuna mtu kafa na kuna msiba pale....!

Wenye macho ya "kiroho" waliliona hilo, wakakataa kushiriki "ibada hiyo haramu ya sanamu"....

Hatuombi na wala sitamani lakini niseme kama sehemu ya mjadala huu, kwamba, miongoni mwa watu waliogusa maisha ya wengi hapa Tanzania ni mzee Reginald Mengi...

Ikitokea huyu mzee aitwe leo, trust me hatapata treatment ya mazishi ya "kiserikali" kama alivyopata huyu ndugu yetu Ruge kwani kwa vipimo vyote hawezi kulingana hata chembe tu na Mzee Reginald Mengi ktk mchango wake wa kuigusa jamii kwa namna ile au hii...!!

Scenario hii ni similar na inawahusu pia watu sampuli ya kina Mzee Bakheresa, Mo Dewji na wanaofanana na hao.....

Why?

Hawana shirika nao katika ulimwengu wa kwao (spiritual world) zaidi ya kuwa walipa kodi wao tu!!
 
shida kubwa nchi yetu ipo katika mfumo ambao mkuu akishaonekana yupo upande gani basi woooooooooooooooote nao huonekana upande huo huo ilimradi ionekane mawazo yao ni mamoja, mfano upo kwa maadui nao pia wamejichanganya kusifu lakini wengine wameenda mbali zaidi mpaka kumuita kaka yote haya dhamira ni ile ile tu mkuu kapendezwa.

Lakini imagine kama mkuu angepotezea basi amini usiamini hili zogo looooote usingeliona
 
Hapa ndipo ambapo mwili wa mpendwa wetu, Ruge Mutahaba utapumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Kijijini kwao Kiziru-Kabale, Bukoba, kesho Jumatatu.
 
Hili ni zaidi ya jibu.

Thread closed!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…