TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Acha amwagiwe sifa, Ruge ana mchango kubwa Kwa Taifa na hasa Kwa vijana.

Ruge kafanya kipi kwa vijana mkuu,

Taifa hili limekuwa la hovyo hovyo kwa sababu ya wanafiki kama ninyi,

Ruge alikuwa ni mfanyabiashara tu na itakuwa sahihi zaidi tukisema jamaa alikuwa ni mjasiriamali mashuhuri

Miaka yote wasanii wamelia sana wananyonywa hamkuyayema hayo mazuri leo amelala ndo mnayasema mazuri

Acheni unafiki
 
Wenzio wanajuana......

Tukio la kifo cha "mwenzao" huyo kwao ni "ibada" yao muhimu kuliko unavyofikiri......

They know exactly hata utaratibu wa kufa kwake. Kulia kwao kote huko ilikuwa ni machozi ya mamba ya kuwafanya wasio na ufahamu wa mambo haya wapumbazike na waamini kweli kuwa kuna mtu kafa na kuna msiba pale....!

Wenye macho ya "kiroho" waliliona hilo, wakakataa kushiriki "ibada hiyo haramu ya sanamu"....

Hatuombi na wala sitamani lakini niseme kama sehemu ya mjadala huu, kwamba, miongoni mwa watu waliogusa maisha ya wengi hapa Tanzania ni mzee Reginald Mengi...

Ikitokea huyu mzee aitwe leo, trust me hatapata treatment ya mazishi ya "kiserikali" kama alivyopata huyu ndugu yetu Ruge kwani kwa vipimo vyote hawezi kulingana hata chembe tu na Mzee Reginald Mengi ktk mchango wake wa kuigusa jamii kwa namna ile au hii...!!

Scenario hii ni similar na inawahusu pia watu sampuli ya kina Mzee Bakheresa, Mo Dewji na wanaofanana na hao.....

Why?

Hawana shirika nao katika ulimwengu wa kwao (spiritual world) zaidi ya kuwa walipa kodi wao tu!!
[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shida kubwa nchi yetu ipo katika mfumo ambao mkuu akishaonekana yupo upande gani basi woooooooooooooooote nao huonekana upande huo huo ilimradi ionekane mawazo yao ni mamoja, mfano upo kwa maadui nao pia wamejichanganya kusifu lakini wengine wameenda mbali zaidi mpaka kumuita kaka yote haya dhamira ni ile ile tu mkuu kapendezwa.

Lakini imagine kama mkuu angepotezea basi amini usiamini hili zogo looooote usingeliona
[emoji122][emoji122][emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Roho ipi Mkuu..roho ndio uhai wenyewe..ikifa nawe unakufa na hapo ndio mwisho wa hadithi..
Hapana ndugu, kuna maisha baada ya kifo, na maisha hayo huandaliwa mtu akiwa hai, pale tunapofariki tu kinachofuata ni hukumu (Waebrania 9:27). Haijalishi kuwa utazikwa mazishi kifahari, au utafanyiwa dua na sala zote, kama hukutengeneza maisha yako ukiwa hai ni kazi bure. Hivyo basi ndugu yetu Ruge Mutahaba, yeye ameshamaliza safari yake; kama alitengeneza maisha yake akiwa hai basi ataurithi uzima wa milele (mbinguni), lakini kama hakutengeneza, Biblia ipo wazi kuwa kinachofuata ni hukumu (Moto wa milele); Mungu ndiye anayejua alipo kwa sasa, na si mwanadamu. Kitu cha muhimu zaidi, ni kwetu sisi tuliobaki hai, inatupasa tufikirie upya kuhusu jinsi ambavyo maisha yetu yatakavyokuwa baada ya kifo. Tumpe Yesu maisha yetu (tuokoke, Warumi 10:9), tuache dhambi, tutende matendo mema, tuwe raia wema hasa kwa kulipa kodi kikamilifu kwa serikali yetu iliyo madarakani, kwa kuwa kwa mujibu wa Biblia, mamlaka hii imetoka kwa Mungu hivyo tuitii na kulipa kodi stahiki kikamilifu (Warumi 13:1-7).

Lakini pia tukumbuke kuwa, Mungu ndiye anayejua maisha ya mtu, kwa maana unaweza ukamwona mtu ni mbaya na mwovu sana hapa duniani, lakini wakati wa mwisho wa uhai wake, akapata neema ya kutengeneza mahusiano yake na Yesu Kristo, hivyo mtu huyu mbinguni atakwenda, kama alivyokuwa kwa yule jambazi aliyesurubiwa pamoja na Yesu pale msalabani (Luka 23:39-43). Vilevile mtu anaweza kuonekana mwema sana duniani lakini ndani yake ni mwovu, hivyo kamwe hawezi kwenda mbinguni. Neno la mwisho ni hili, tengeneza maisha yako sasa, baada ya kufa ni hukumu wala sio kesi, maana kwenye kesi huwa unapata nafasi ya kujitetea.

Mungu akubariki sana ndugu.
 
Majeruhi Lissu
- Anamsimamo kwa mambo anayoyasimimamia, kama kuyumba ni kwa asilimia chache.
- Tofauti ma majeruhi wengine wa watu wasiojulikana mfano Ulimboka, hajakatisha harakati zake.
- Mengine ni makamanda wanaweza kusaidia

Hayati Ruge
- Harakati zake zimegusa mamilioni ya watanzania katika biashara, burudani, sanaa, afya na uchumi.
-Ameinua tasnia ya habari, chombonchake clouds fm nimewahi kukiona ndani ya top ten ya redio bora afrika.

etc wadau mnafahamu mengi zaidi.

nani unadhani anastahili kuwa kaka wa taifa?
 
Ruge kafanya kipi kwa vijana mkuu,

Taifa hili limekuwa la hovyo hovyo kwa sababu ya wanafiki kama ninyi,
Kama wewe huoni mchango Wa Ruge ni wewe usilazimishe sisi tulioona mchango wake tuseme hatujaona. Neno unafiki siku hizi naona linatumika ndivyo sivyo, yaani kwamba Mimi kama nimeona mchango wake nikisema alikuwa Na mchango mkubwa hiyo inakuwa ni unafiki, Ila wewe ukisema hukuona mchango wake hiyo inakuwa sio unafiki. Pathetic!!!
 
Huo mchango wake unausema leo mwamba akiwa amelala?

Kwanini hukunyanyua kinywa kusema kwamba mnamuonea Wakati akipakwa tope akiwa hai?

Yaani leo akiwa amelala mchango umeonekana na anatetewa ila wakati yu hai watu wanalalamika mlikaa kimya huo ndo unafiki sasa.
 
Kama wewe huoni mchango Wa Ruge ni wewe usilazimishe sisi tulioona mchango wake tuseme hatujaona. Neno unafiki siku hizi naona linatumika ndivyo sivyo, yaani kwamba Mimi kama nimeona mchango wake nikisema alikuwa Na mchango mkubwa hiyo inakuwa ni unafiki, Ila wewe ukisema hukuona mchango wake hiyo inakuwa sio unafiki. Pathetic!!!
Acha kujibizana na huyo taburasa
 
Ruge kafanya kipi kwa vijana mkuu,

Taifa hili limekuwa la hovyo hovyo kwa sababu ya wanafiki kama ninyi,

Ruge alikuwa ni mfanyabiashara tu na itakuwa sahihi zaidi tukisema jamaa alikuwa ni mjasiriamali mashuhuri

Miaka yote wasanii wamelia sana wananyonywa hamkuyayema hayo mazuri leo amelala ndo mnayasema mazuri

Acheni unafiki
Na sisi watanzania ni wanafiki yani kila anayezaliwa tz lazima awe mnafiki tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom