TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Hahaha kwani hata asingefariki sasa angefariki tu siku nyingine, lakini keshafariki kwanini promotion za msiba wake haziiishi?! Wanataka arudi au wantafita wa kumlaumu?! Kudanja hakatiwi rufaa wange tafuta dawa kuponya wagonjwa walio hai badala kudeal na marehemu.
Ok iwe ameuliwa, then what?!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuzaliwa pekee yake hakukufanyi kuwa raia wa nchi flani

Kuna taratibu nyingine nyingi za kufuatwa ili uwe raia

Japo kuzaliwa inakufanya iwe rahisi kuwa raia wa nchi husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hizi taarifa sijui mnazitoa wapi

Kaka mkubwa alikuwa Immunocompromised siku mingi hata matatizo yanayoeleza ni zao la lake na matibabu yake baada ya muda mrefu.
 
Mkuu hapa napinga kama hakutubu ni mdhambi tu, haimaanishi kwakua aliwasaidia wengi dhambi zake zimefutwa, Hapana Haijawahi kuwa hivyo na kamwe haitakua hivyo, kutubu ni lazima kwani imeandikwa "watakaofungiwa Duniani na mbinguni pia wamefungiwa"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ata huo uwepo wa KATEKISTA wameistahi familia ya Profesa, na huo ni utaratibu wa kawaida maeneo mengi ya wakristo (Katoliki, Anglican na Lutherani) endapo hukuwa mshiriki katika yaliyo ya msingi

Kanisa huanzia nyumbani (familia), linakuwa kwa kujumuisha wanajamii wa mahalia (jumuiya ndogo ndogo) ziunganapo zinafanya kanisa kubwa (jengo) waendapo sali pamoja

Yapo maswala ya msingi usipotekeleza UNAJITENGA NA KANISA na sio kanisa linakutengaa

shauku ya kuzikwa na taasisi ya kidini sio njia ya kufika peponi.....matendo yako na kufuata misingi ya imani yako ndo salama yako
 
Hili la kutubu ni moja ya maeneo makubwa sana yatakayo wapeleka Wakatoliki motoni.

Bwana wetu Yesu Kristo alitusisitizia "usihukumu, usije ukahukumiwa"
Who are you kuhukumu?.

Ukifanya dhambi unamkosea Mungu, hivyo kama ni kutubu, ni kutubu kwa Mungu na sio kwa mwanadamu.

Toba ya kweli ni baina ya mkosaji na Mungu wake, ili kufanya toba ya kweli huhitaji kwenda kuungama kwa Padri, hata ukitubu wewe mwenyewe tuu, tena kimoyomoyo, toba yako inafika, ndio maana Bwana wetu Yesu Kristo alitusisitizia, "tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo" . Nani alikuwako moyoni mwa Ruge zile siku zake za mwisho za uhai wake?.

Kanisa Katoliki linataka matendo, Yesu amefundisha mambo ya moyoni, who are they to judge?.

Ingekuwa Mungu Baba anatoa daily list ya wanaiongia mbinguni na motoni, kuna wengi mngekuwa surprised na kupigwa na butwaa pale mnapoona wale wakamilifu wetu, maaskofu, mapadri na viongozi wetu wa dini wakitupwa motoni, huku wadhambi wakiingia mbinguni. Yesu alikuja kwa ajili ya wakosefu na sio wakamilifu. Alisema" wote wenye mizigo, nitawapumzisha". Ruge aliishakabidhi mizigo yote kwa Yesu mwenyewe na sasa amepumzishwa. Nyie endeleeni na kuwategemea binaadamu, mtafanywa kuni...
P
 
Yes,kutoshiriki jumuia kwake kulilikosesha kanisa mapato,ndiposa wakamsubiri dakika za mwisho ili kumwonyesha,ili liwe funzo kwa wengine wasiotii kanisa
 
Hili kanisa limegubikwa na kashfa dunia nzima ya maaskofu wake kubaka watoto miaka na miaka, mpaka juzi askof mkuu wa marekani kavuliwa uaskofu. Ni barani Afrika tuu vijana waliolelewa ndani y kanisa na seminari zao hawajajitokeza kulishitaki kwa kulawitiwa wakiwa mashuleni, etc Nadhani ni sababu ya mila za kiafrika, hatusikilizi wanyonge. Lakini mtu mwenye kujielewa hatajihusisha na hili kanisa. Hatujui matakwa ya Ruge yalikuwaje. Hatujui uhusiano wao na huyo aliyeendesha misa. Watazania tujifunze kumind our own business..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…