Mimi binafsi hua nina questioning mind, hua sikubaliani na kila ninachoambiwa bila kujiuliza.
Kwa maelezo ya mwana familia, Ruge alifariki majira ya sa kumi jioni siku ya juzi tarehe 26.2.2019 huko kwa Mzee Mandela.
Katika hali ya kawaida najua watu wa kwanza kujua habari ya kifo ni wanafamilia pamoja na ndugu na marafiki wa karbu mapema kabisa baada ya mpendwa wao kuwatoka. Hili la Ruge limekua tofauti, baada ya kupita takribani masaa 4 baada ya kifo, taarifa ya kifo imekuja kutolewa kwa hadhara na Mheshimiwa Rais.
Najiuliza tu, ilikuaje rais ndio akawa mtu wa kwanza kuujulisha umma kifo cha Ruge. Hakuna asiejua kua Ruge ni mtu maarufu ila hakua kiongozi wa kisiasa.
Najiuliza tu.