Vitu vingine wala havihitaji nguvu nyingi kuanza Kuvihoji au kuviwekea hisia fulani na ambazo pengine zimechanganyika na Chuki zetu kwa Rais Dkt. Magufuli au Utawala wake huu au Chama chake cha CCM. Kama leo unahoji ni kwanini Mheshimiwa Rais alikuwa wa Kwanza Kututangazia Kifo cha Ruge mbona haujahoji au huhoji ni kwanini Rais huyo huyo ndiyo alikuwa wa Kwanza Kujitolea Pesa za Kumsaidia Ruge kwa matibabu yake huko Umauti ulikomkutia?
Hakuna asiyejua kuwa Marehemu Ruge alikuwa na ' influence ' kubwa sana si tu nchini bali hata Serikalini na katika Chama chake cha CCM kutokana na umuhimu wake hasa wa Kifikra, Kiuwajibikaji na Ubunifu ambao uliweza kumfanya akubalike na aaminiwe na hata kufanywa Waziri Kivuli asiye na Wizara ' Maalum ' kwa Imani kwani kuna Mambo mengine / Vitu vingine Ruge alikuwa akivifanya ambavyo hata hao wenye Dhamana Wakuu wa Mikoa au Mawaziri hawakuweza kufanya au kuthubutu vile vile.
' Protocally ' Kitendo tu cha Mheshimiwa Rais ' Kujitolea ' vile katika matibabu ya Ruge tayari ilikuwa ni taa ya Kijani kwamba ' State House ' ilikuwa kwa 75% inasimamia kila Kitu chake na huenda hata taarifa za Maendeleo yake ya Ugonjwa zilikuwa zinaanza Kwanza kumfikia Yeye kisha ndipo zinaenda kwa Familia yake. Kwa mantiki hiyo its so obvious kwamba hata Kifo chake kilipotokea ilkuwa ni rahisi Kwake Kuutangazia Umma na nina uhakika hata Familia ya Ruge nayo ilimkabidhi Mtoto wao kwa ' State ' hali ambayo ndiyo maana hata Tangazo la Kifo chake Kilipotokea tu Mwenye Hisa mkubwa ' Tajiri ' Joseph Kusaga alianza Kwanza Kumshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali yake ndipo akamalizia Kutushukuru na Kutupa pole akina ' Kajamba Nani ' siye.
Ni Mpumbavu / Popoma tu pekee ndiyo mpaka hivi leo hawezi kujua au hajajua kuwa ' Influence ' ya Ruge nchini ilikuwa ni Kubwa kuliko hata Watendaji wengine na ndiyo maana hata taarifa ambazo niligusiwa na Mtu mwaka jana ni kwamba kama isingekuwa huu Ugonjwa wake basi Marehemu Ruge ilikuwa ama ateuliwe Ubunge ili apewe Wizara au Kuundwe Taasisi moja muhimu nchini yenye Kujihusisha na Maendeleo ya Vijana na Ujasirimali ili aisimamie. Mheshimiwa Rais alimpenda sana Marehemu Ruge.
Mwisho kabisa kwa Kukusaidia tu ni kwamba ni desturi sehemu nyingi kwa Marais ambao huwa wanastaafu hupenda Kuwaacha ' Warithi ' Wao na taarifa muhimu za Watu wa Kufanya nao Kazi ili Uongozi wao uende vyema. Hakuna asiyejua kuwa Marehemu Ruge alikuwa ni Kipenzi cha Rais Mstaafu Kikwete na hata Mafanikio mengi ya Marehemu Ruge na Taasisi yake ya CMG yalikuja kuwa mazuri na kufanikiwa sana wakati wa Uongozi wa Awamu ya Nne hivyo ilikuwa ni rahisi mno kwa Mzee Kikwete ' Kumuambukiza ' Upendo wake kwa Ruge Rais Dkt. Magufuli ambaye kwa bahati nzuri nae pia aliona Uchapakazi wa Kutukuka wa Marehemu Ruge ndipo nae akaongeza Mapenzi yake maradufu Kwake.
Kikubwa kwa sasa tuache Kumjadili Marehemu Ruge kama tabia zetu za Kiswahili Kiswahili zilivyo bali tumuombee tu Makazi mema huko atakapohifadhiwa katika Nyumba yake ya Milele, Mwenyezi Mungu amsamehe, Sisi pia tumsamehe pale alipotukosea na tumuenzi zaidi kwa yale yote mema aliyoyafanya kwani siyo Siri alikuwa na Kipaji cha Kipekee kabisa na ameacha ' Legacy ' ya Kutukuka kabisa ambayo nina uhakika itatuchukua muda mrefu kuisahau na pengo lake kuja Kuzibika ni Kazi pevu / ngumu.
Rest In Peace ' Genius ' wa Entertainment and Creative Industry nchini Tanzania ' Mtani ' wangu wa Kihaya Ruge Mutahaba. Tutakukumbuka sana na mno Kaka. Nenda Kaka umeumaliza mwendo wako vyema na tuliobaki tutajitahidi kupita mule mule ulikokuwa Wewe japo najua Viatu vyako vitakuwa ni Vikubwa Kwetu na vitatupwaya kama siyo kutupwelepweta tu.